Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Mzee Kassim Mpenda akionesha picha Mpya rasmi ya JK (shoto) itakayotumika kitaifa kuchukua nafasi ya ile ya zamani (kulia). Picha hii mpya imepigwa na mpigapicha mahiri Zahur Ramji wa Moonlight photo studio wakati ile ya awali ilipigiwa studio ya Akber zote za Dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 27, 2008

    inaelekea atakuwa anabadilisha picha kila mwaka,nini sababu ya kubadilisha hiyo ya awali?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 27, 2008

    Amecehmsha sana sana. Bush anavaa nyekundu au bluu kwa sababu zipo kwenye bendera yao ya taifa. Kikwete kama kashauriwa kubadilisha tai ni bora ngevaa kijani nyeusi bluu au njano. Hwaezi kurepresent. Kosa dogo lakini maana yake kubwa na hasara yake kubwa. Kwa yeye hapo hiyo tai nyekundu ina maana Danger! Anamtisha nani? Wapinzani?
    Analyst of non verbal communications,USA

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 27, 2008

    What is the logic of doing so, au deal ya watu sasa wauze picha zao maana ni biashara nzuri sana kwa Tanzania nzima! sijaelewa kabisa.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 27, 2008

    HUYU JAMAA JK NI KIBOKO.
    TUENDELEE KUSUBIRI MABADILIKO!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 27, 2008

    Tofauti zake ni nini na kwanini inabadilishwa? Kubadilisha picha si habari, habari ni kwanini inabadilishwa, mnatulisha madudu mengi sana jamani ndio maana tunakuwa wavivu muda mwingi tunadaijesti, Mtanipinga ila mwanaHabari mnachangia sana upotezaji wa muda na urudishaji maendeleo nyuma, bosi wangu anasoma magazeti masaa mawili, si uwendawazimu huo!
    Mtu km mimi sioni kwanini picha ya rais ibadilishwe tena ndani ya msimu mmoja! KWa TZ sishangai kusikia KUNA MTU ANA PASENTI YAKE KATIKA PURODAKISHENI YA HIZO PICHA Vipi mtatuuzia tena maana najua ni biashara au hizi mtagawa bure? Picha imepigwa na nani inasaidia nini? Biashara eeeh!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 27, 2008

    Kwanini imebadidilishwa???Au Rais kanenepa sana kwa hiyo wana-Update(Natania).Michuzi,Sisi wenye ofisi binafsi tungependa kujua gharama ya hiyo picha mpya,tungependa na sisi kuibandika ukutani

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 27, 2008

    huyu rais wetu ni bishoo sana, kioo kinamdanganya kuwa bado ni kijana ndiyo maana anabadilisha picha.

    Kuna mambo makubwa ambayo anatakiwa ayashughulikie hapa nchini badala ya hii ya kuuza sura. Kuna maswala kama ya Muungano,Mfumuko wa bei, Ufisadi, Mpasuko wa kisiasa wa Zanzibar, na hata kuweka mabo sawa ndani ya chama chake mwenyewe. Ukweli ni kwamba sisi watanzania hatujui tunakokwenda kama nchi hata yeye mwenyewe ukimuuliza hajui. Viongozi wote wamekuwa Wasanii, je hapa wanajenga Taifa la nani?
    Nimetoa dukuduku langu kwa uchungu Kama Mzee Michuzi ukiamua kuibania shauri yako lakini HABARI NDIYO HIYO. Michael J. Laiser - Dar

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 27, 2008

    Watanzania wenzangu, jee kati ya picha hizo 2 kuna tofauti yeyote iliyosababisha kubadilishwa kwa picha ya wali? Idara ya habari maelezo tusijipendekeze kwa Rais. Perosnally, sioni creativity yeyote ile katika picha hii mpya - MLIPA KODI

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 27, 2008

    This Country!!!!!!!!!!! We have a long way to go. Yaani Mtu anaitisha Press conference kutangaza Rais kabadilisha Picha? Haka ni Ka-Mchezo ka kula hela za Watu. Bei yake wameitangaza TZS 15,000/- each!!! This is ridculous. Sasa wanataka waanze tena kuvuna hela za watu. Si ajabu wameweka na Deadline ya kuondoa zile za mwanzo.. Haya ngoja tuone, kama ni kufuata mambo ya Bush basi baada ya muda na size ya Noti zetu itabadilishwa!! yetu Macho.

    Ni Hayo tu!!!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 27, 2008

    Huyu jamaa hajaacha 'ubrothemen'? Mbona umri umekwenda sana? Afterall what is the essence of this change? Yaweza kuwa 'dili', ile ya zamani kuna sehemu ilikuwa ikiuzwa tshs 150,000/=

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 27, 2008

    Yes. I thank God kwamba at last the JK Photo has been changed because for the first time I saw that photo I noted some mistakes. JK was not straight seen in that photo the photo was taken by the side not from infront. Am not a photographer but Brother Michuzi might help. With the first photo one ear was not seen am not so sure with the second but I think it is better compared to the first one. I did not know where to air my views but I think now am relieved. At least they have noted the mistakes and rectify. I know the President's photo is affordable but the issues is whether the former photo will be replaced with the new one in time. Am afraid we'll keep havign the old one in our offices... Anyway at least they have changed it.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 27, 2008

    Mimi pengine sijaelewa vizuri na ninaomba wanblog wenzangu mnielimishe. Kwani kutoka kwa hizi picha mpya ina maana zile za zamani tulizonunua tayri hazitotumika tena? kutokana na malalamiko ya wanblog wengine napata hisia kuwa tutalazimika kununua hizi mpya na watu wanaifeel hiyo gharama.nielimisheni plse. Kuhusu rangi ya tai mimi hata sioni kama kuna tatizo hapo, mbona Nyerere alikuwa havai hata tai kwenye picha zake? ndio kwanza kaachia na kifungo au kavaa kaunda suti yake, mimi nafikiri JK anakwenda na mapigo ya sasa ambayo nimeona wanaume wengi wanavaa red.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 27, 2008

    sababu ya kubadilishwa: mpya kavaa miwani na ya zamani hajavaa,kwenye leseni yako ya gari ni lazima picha unayoibandika hioyeshe kama huna matatizo ya macho, kama ukipiga picha umevaa miwani,basi ni lazima uendeshapo gari uvae miwani, sasa mkulu wa kaya macho yanamfanyia matatizo ndiyo maana kaamua kuweka picha kuelezea hali aliyonayo.KAMA ASINGEKUWA NA UBOVU WA MACHO, BASI NCHI HISINGEKUWA KAMA ILIVYO SASA

    kijiwe

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 27, 2008

    Heee! Huyo aliyeshika hizo picha mbona kakunja uso hivyo, au hizo picha ni nzito sana.???

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 27, 2008

    Ile ya kwanza ni ya MRENGO WA KUSHOTO (Sawa na Mkapa) - Yaani hataki kufananishwa na uozo wa MKAPA; Hii ya pili ni ya MRENGO WA KATI - Yaani hata Kina KABWE wanaweza kuingia katika Baraza la Mawaziri. Ngojeeni Mabadiliko mwezi wa nane mwanzoni.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 27, 2008

    Ok mwanzo aliuza sikio la kulia sasa ni zamu ya sikio la kushoto maana tushaianza nusu ya pili,pengine sikio la kushoto lina bahati,yangu macho

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 27, 2008

    Kwa heshima kubwa, mzee Kassim. Vipi Jafari na Shaffi wanaendeleaje? Nakubaliana na wadau hapo juu, ukweli kama mkurugenzi, sidhani kama kuna umuhimu wa kubaidilisha picha. Namkumbuka saaana marehemu Nyerere, kwani aliona Kaunda suit, ni vazi zuri sana, maana huhitaji kubadili tai au kubaidili mashati kila leo. Nafikiri lingekuwa vazi zuri kwa viongozi wa Kiafrika, ila watu wa magharibi ndivyo haswa wanavyotaka, kuona kwamba kila kitu chetu kizuri na tulichovumbua kinatokomea, mila utamaduni na mengine ya asili, ili watutawale ki akili. Mzee Kassim, nakutakia maisha mema na familia yako yoote.

    Mchangiaji

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 27, 2008

    wabongo bwana..waosha vinywa sana..sasa kuvaa tai nyekundu kuna ubaya gani?

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 27, 2008

    jamani tofauti hamuioni ni ndogo sana mbona baba wa watu mlimpa hii kazi ya uraisi akaipokea akiwa na macho yake mawili mazima yanaona vizuri bila ya ukungu sasa baada ya kukaa kwenye hicho kiti kakumbana na mengi kama vile ya ufisadi na rushwa na vidunguli vya sangoma mpaka bungeni kiasi kwamba sasa mpaka mmempofua macho haoni mbele vizuri sasa inabidi avae miwani .....yaani mimi i feel for him jamani baba wa watu alikuwa bonge la handsome boy sasa hivi kachooooka mno duu !!pole JK na usipokuwa makini tutakumaliza kwani wewe hujui wabongo sisi ni Nuksi ?? mimi ningekuwa wewe nisingejali kitu wala mtu anza kuchukua chako mapema ukifika muda wako uwahi mbele kama waliotangulia tatizo lako wewe unajali mno nchi yako ..who cares ??? Hiyo lensi ya miwani itaenda inaongezeka kila mwaka shaurilako ...........!!!

    ReplyDelete
  20. Inasemekana kuwa ile picha ya zamani ilikuwa haidhihirishi hali/taswira yake ya kawaida. Eti inamwonyesha akiwa na msongo wa mawazo (stress)kutokana na kampeni za uchaguzi. Hivyo wametoa picha mpya inayoonyesha akiwa ametulia tele. Ndio mamabo ya ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya hayo!

    Kuhusu tai nyekundu kuna nadharia tete (conspiracy theory), kwa maelezo zaidi wasiliana na wamiliki wa uchumi wa dunia hii ambao mara kwa mara wakikutana wanakuwa wametinga tai nyekundu!Utandawazi kweli si mchezo!

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 27, 2008

    kwani watu wataambiwa watoe zile za zamani? si picha yake tuu.mbona nyerere tulikua na za kila aina...msije mkacharge watu kutoa picha za zamani na kununa mpya...

    picha tu press release.....jamani bongo mbona kazi ipo...ndo maana wanasama bongo masaa yao ni 26 kwa siku kwahiyo wana saa moja la ziada mchana kuchezea na moja usiku....time is money bro

    ReplyDelete
  22. Anonymous wa Tarehe June 27, 2008 1:45 PM umnichekesha mno una utani wa kiakili poa sana hiyo

    E bwana chambi hiyo ni kweli ila baadhi ya wabeba maboxi hawawezi kukuelewa hii inahitaji deep thinkers

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 28, 2008

    Wajameni kumbuka kuwa hii ni Bongo. Mambo yanakwenda kibongobongo. Na nyie JK amewazidi sana ndio maana hamuoni hata tofauti kati ya vivuli hivi viwili. Kwanza ni mwili, hii mpya ameweka tabasamu pana (pengine ikitukumbusha kuwa ile safari ya kuelekea maisha bora ndio tumefika katikati. Pili, mavazi, hii ya sasa ametinga tai nyekundu (ikiashiria kuwa sasa katika safari ya utandawazi - ukoloni mamboleo- ndio umenoga) si mnajua mkuu wa unyamwezini anavyotinga?. Tatu, utambulisho wa maneno katika hii ya sasa uko katika kizungu (Mungu atupe nini, debe la kunguni?) nyie mnaotaka kuendeleza uswahili kalagebaho! MUNGU IBARIKI BONGO!!!!!!

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 28, 2008

    Duuh,haya tena sisi hatuna la kusema. Ila isijekuwa Akber "HAKUWAONA" wazee (mambo ya 10%)na ndo mana picha yake imekuwa withdrawn.

    ReplyDelete
  25. Ndugu Mpaka unakumbuka Kichaka na Muungwana walivaa tai za rangi gani ile siku walipomwaga wino wa kukabidhiana vijisenti vya kupambana na VVU pale Ikula?

    Je, unakumbuka Kichaka na Burea walivaa tai za rangi gani pale walipoamua kumchangia mande Hayati Saadamu?

    Na,je, kwa nini Kichaka alipoulizwa ni kosa gani kubwa alilifanya katika siku 100 za kwanza akiwa Rais wa Yuesie alijibu kwa utani kuwa "labda ni kuvaa tai nyekundu mara nyingi"?

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 20, 2008

    Just wastage of public funds, we have no good social services to our poor people, then what is a point of changing president's picture every year, after all what is the use of the president's picture in government and private offices, not at all, I have been in most democratic western countries' offices I have ever never seen a photo of their leadrs on their walls. HUO NI UZAMANI HUSIO NA MAANA AU ULAZIMA YOYOTE ZAIDI YA UDIKTETA KUFANYA NCHI NI MALI ZAO, HAINA HAJA YA PICHA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...