PARTY PIPO

The Event You have been waiting in Mid-West's Finest (614),
COLUMBUS,
OHIO.
Wabongo's Official City the original Bashment was Born.


THE OLD SKOOL WEEKEND

July 3rd - July 6th.3 Nights, 3 Different Venues,
Plenty of Daytime Activities, Sports Events(Simba v/s Yanga), BBQ
BROUGHT TO YOU J&T Ent., Oldies Gold Productions & Lups Ent.
FRIDAY JULY 4th,
MAISHA NIGHT @ COMFORT INN & SUITES,1213 E. Dublin Granville RD, Columbus, OH 43229Doors Open 10pm - 5am, Cover $10


MAIN EVENTSaturday July 5th,OLD SKOOL PARTY @ THE GATHERING PLACE,847 E. 11th Ave. Columbus, OH 43211Doors Open @ 9pm - 7am, Cover $10 B4 Midnight
Special Appearance By DJ Bonny Luv, T&T Jackson, surprise DJ from UK, and Own Zone The Mix Master Dj Luke....
Check out hotels @
http://www.kayak.com

For more Information -
http://www.oldskoolnjoo.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 27, 2008

    Uchumi wa marekani unaenda pabaya wahamiaji mtakuwa na maisha mgumu kupita kiasi huko mbeleni. Mtanyang'anywa nyumba na kufukuzwa kwenye apartments zenu mkifanya mzahamzaha. Tafuteni makaratasi yenu acheni kufuata mkumbo hayo mambo ya Columbus Old Skul yamepitwa na wakati. Fanyeni fund rasing kusaidia yatima badala ya kununua suti za Walmart na kuwatajirisha Macy's, Holiday Inn, na Rental cars. Vijana chapeni mzigo mjikomboe pigeni shule mjikomboe acheni ushamba wa kunywa pombe ovyo. Iwe heinken iwe Martini iwe Konyagi Ulevi nchi za watu hauna mpango. Kanyweni pombe kwenu mlikotoka.Tafuteni kilichowaleta na kama ni vistarehe visivyo na mbele wala nyuma basi endeleeni kucheza na maisha. Wamarekani wanawachora tu. Si mnakumbuka Hammer na Range Rovers za Wazungu wa chips wa Houston?
    Iweje mnahangaika na July 4th wakati December 9th wala hamna time nayo. Kujikomba huko? Mnapata nini? kufukuzwa? Akili kichwani Wabongo mliopo majuu Party People! nendeni Holly Wood! Toka lini party ya Bongo celebrity ikawa Columbus!! Nendeni Migomigo au Manzese mkafanye hiyo party yenu acheni kujifanya hamjui kuwa bei ya mafuta dala tano. Kwa usawa huu bado mnacheza tu!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 27, 2008

    Nyie Watu mliokulia Third World na kuja Marekani Ukubwnai Naona mnakosa malengo!!Bora Mngebaki kule Afrika mpambane na Mugabe! Hivi Columbus ndio wapi?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 27, 2008

    duh we annon wa kwanza kweli noma mbona unaua sana mkubwa? ila ndio ukweli wenyewe huo hahaha we uko wapi kwani

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 27, 2008

    Used Hummers na second hand Range rovers ziliwatokea watu puani! Nyie chezeni na wakati.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 27, 2008

    Anon wa kwanza kabisa ninakuunga mkono 100%. Huku tumekalia kuwaza starehe tu wakati nchi yetu inadidimia na eti tunaomba misaada kwa mastaaa wa Marekani wakati pesa ambazo zitamwagika Columbus zingeweza kabisa kusaidia hata kuanzisha kituo cha watoto yatima huko nyumbani kwetu TZ. Watu bwana, ila nimegundua kuna watu wengi sana kazi yao kufuata mkumbo.... hao mimi huwa ninawaita " bibi kisimpite" au "bwana kisimpite" maana wanaona wao wasipojitokeza nikama shughuli haitafanyika wasijui kuwa wanajidhalilisha tuu na mambo yao ya ajabu ajabu badala ya kusawazisha maisha yao kwanza. Nyumbani watu hawajengi, kazi kuparty tuuuu ndio maana hatuendelei. Tamasha kama hili lingekuwa linafanyika kwa ajili ya ile wanaita "Upatu" ili kumsaidia mmoja mmoja anufaike, mbona ingekuwa raha sana. Sasa ni starehe ambazo utasikia wengi wao wakitoka hapo wanaishia jela kwa ajili ya kulewa na kuendesha gari. Its a shame. I mean big shame. Tufunguke macho na tusisubiri tarumbeta zitupigie masikioni kuona ya mbeleni. Mungu ibariki Tanzania na Watu wake.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 27, 2008

    msipende kuingilia maisha ya watu,kila mtu na maamuzi yake.wewe unakanda kama vile maisha yako ni bora wakati kiukweli we binafsi unajua kwenu choka mbaya ndio maana unahasira.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 27, 2008

    NOT EVERYBODY WHO PARTYIN' IS IRRESPONSIBLE!!!!!,KAMA HIVYO I INGEKUWA WATANZANIA WA HUKO NYUMBANI WANA STAREHE 7 DAYS A WEEK KWENYE BARS THERE ARE MOST IRRESPONSIBLE NA KWA SABABU WANAZIONA SHIDA HAPO NYUMBANI KULIKO WATU WALIO MBALI.(WHICH I DONT THINK THERE ARE,COZ ITS HUMMAN NATURE TO MAKE URSELF FEEL GOOD IN ONE WAY OR ANOTHER.
    MY ADVICE KWA WALE WANAOENDA KWENYE HIYO PARTY YA COLUMBUS IS -JUST PARTY RESPONSIBLY, ANGALIA UWEZO WAKO , DONT FORCE KITU WHICH U CANT AFFORD, IF U CANT STAY HOME KAMA UNA AFFORD ITS ALL GOOD FOR U , NOT TOO BAD ONCE IN YEAR TO DO THAT!!.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 27, 2008

    Ushauri wa bure kwa wale wakinadada wa Columbus angalieni msje mkaishia kuiba tena Marcy!tunasubiri tuone itakuwa zamu ya nani kwenda kizimbani!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 27, 2008

    Unadhani hata Watanzania wenywe wana hela au jeuri yoyote? Wanajitutumua tu! Wakitoka hapo wanarudi kwenye kazi za suluba. Kwa maana hiyo hawajaweza kujikomboa kimaisha kikazi au kielimu. Party sio tatizo kabisa tatizo ni kwamba watu hawana maendeleo na hawatafuti makaratasi au kazi za maana. Matokeao yake Watanzania wengi wanadharauliwa na mataifa mengine ya Afrika Magharibi na Mashariki. Mtafanya kazi za dala 12 mpaka lini? Jikomboeni kwanza,party zipo kila mahali kila siku.Hako kamji kenyewe ka Columbus kako huko Bush hamna maendeleo. Watu kibao hawana makazi, viwanda vimekufa, nyumba hazina watu, high foreclosure rate, high unemployment rate, high low class. Acheni ulimbukeni partini kwa wakati wenu lakini msifanye big deal about it. we've been there we've done that it's not worth it!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 27, 2008

    hahaha awwwwwwww pipo neve ceased to amaze me...so wewe Anon hapo juu mbona kuna matangazi kila siku kwenye blog kuhusu watu huko Tanzania ku have fun kila siku na watu hawasemi kitu ila watu wa majuu wakisema wa have fun basi mtarusha kila aina ya maneno...This is so amazing to see how low class of period...if you aing got none better to say then don't say it...just shut up!...Nani kasema bei ya mafuta ipo juu marekani tuu?Bei ya mafuta tena kwa taarifa yako its more higher in Tanzania than America remember nyie huko mnatumia liter and America wanatumia Gallon na gallon moja ni4.15 cents and how much is a liter unalipa?..You are definetely paying like $9 for liter moja...so don't bullshity a bullishter dude...Toa kwanza boriti kwenye jicho lako ndipo utaona kibanzi kwenye jicho la mwenzako...

    Handle yours dude!..

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 27, 2008

    Duu!!! watu wana hasira humu kwenye blog utafikiri wamelazimishwa kwenda kwenye party!,IF U CANT AFFORD JUS SHUT THE HECK UP!,waache wenye uwezo wakale raha hakuna mtu aliyelazimishwa kwenda huko, watanzania mlioko huko if u can afford nyie kaleni rahaa, msiwasikilize wabangua korosho we chuki na hasira mbele!!!,ALL THE BEST NA PARTY YENU HUKO!!,
    Mlioko bongo nimeona kuna party somewhere ime postiwa kwenye michuzi(BEACH BASH PARTY-CINE CLUB),anybody has comment about that,kuhusu kwamba watu mlioko bongo wasile raha?

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 28, 2008

    Anonymous wa June 27, 2008 9:21 PM:

    Angalia data zako kabla hujaaza kuropoka kama mlevi.

    Columbus ni the 15th largest city in the US. There are more Colleges and Universities in Columbus Ohio kuliko Tanzania. Hata Hospitali or public libraries.

    Kuna more companies hapa kuliko Tanzania nzima.

    Kwa taarifa yako OHIO ni moja ya richest state hapa USA.

    OHIO hauwezi kulinganisha na nchi yoyote ya Africa.

    Plato alisema ukweli:
    "“Wise men speak because they have something to say; Fools because they have to say something.”

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 28, 2008

    Shenzi type kama wewe ni maskini wa kila kitu wacha kusema wenye hela zao wakale raha hata kama sio milionea lakini hizo nilizonazo zinatosha kustarehe mimi napaa kutoka London kwenda kula raha Columbus sasa wewe mwenye wivu wewe jinyonge tu na comment zako za ajabu halafu tuone wewe usioenda kama utajenga nyumba kwa kusevu vihela ambavyo ungetumia kwenye party na mshindwe vyote wenye roho mbaya ngoja tukaparty sie.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 28, 2008

    Aisssseeee - Watu wana issues. Juilize umesha wahi kuchukua likizo? Life is too short, jiulize siku yako ikifika who will care? Enjoy Life Babu!

    Kila mtu duniani ana lengo lake kwenye maisha. FUN comes in many forms, could be one of those things that some people use to rejuvinate themselves. DONT HATE...

    Wewe focus ku improve maisha yako. Usipoteze muda kwa kumwaga senseless pumba. Kama wewe you have been there and done that lakini haukunufaika then fanya kitu kingine.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 28, 2008

    Hivi nyie mnaijua kweli Marekani au mmetembea mkaona dunia? Raha itakuwa Columbus? Huwezi kulinganisha bei ya mafuta ya Tanzania na Marekani hata kama Tanzania ni dala 11 kwa gallon sio tatizo sana kama Marekani ikiwa dala 7 kwa gallon. Mimi naijua Marekani kuliko unavyodhani hata kama niko Bongo hakuna kinachonibabaisha kuhusu Marekani mnayoibabaikia. Na kama mnaona mna afford hicho kiparty chenu cha ya Columbus na hayo ni mafanikio na maendeleo ya kujivunia mbele ya watu,nendeni mkaliwe badala ya kula starehe. Nyie kama wajanja kafanyeni party yenu Manhattan sio Columbus!!! Sisi tulikuja huko na kufanya party yetu Sheraton Manhattan. Nendeni mkalale kwenye hoeli za dala 15,000 kwa usiku mmoja. Si mnajidai mnajua kustarehe. Acheni mchezo tafuteni maisha party zipo kila pahali kila siku starehe zipo kila pahali kila siku sio Columbus tu. Mnamualika Michael Jackson au bendi ya tatu nane na njenje ooo njenje njeee ooo njenjenje una kipala ng'ondo njenje. ahahaha. Haya Old Skul party,use your senses.Pigeni madogoli achana na kuiga kina Lil Wayne na T pain. Hata Old skul yenyewe mtapiga nyimbo za Kimarekani sasa hapo ndio utashangaa. Kama mnafanya Sindimba party au Mdundiko party Old Skuli ntawaelewa.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 28, 2008

    Wenye uwezo wa kutanua hawaendi Columbus! Msijidanganye. kila mtu na uamuzi wake ila ujinga ukizidi tushtuane.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 28, 2008

    Acheni ushamba. Marekani sio kama Bongo raha zipo Dar tu. Ukienda mkoani like Morogoro au Arusha ni bush hakuna kitu.

    Marekani raha ipo sehemu yoyote. Hata kwenye small town like Jefferson City in Missouri.

    Marekani raha ni pesa yako tu. Mbona kuna ma billionaire kama Lex Wexner(Founder wa Victoria Secret) bado wanaishi Columbus, Ohio?

    Raha haziko Manhattan tu.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 29, 2008

    Hivi kweli watanzania tutaendelea kweli? sasa hapa tatizo ni nini? ni kwamba watu wasi party au nini?
    Watu wa Tanzania wanaparty 24/7 kila siku vishiguli wanafanya harusi za kifahali barabara ni mbovu maisha magumu, kwanini msiwalaumu watu kama hao badala ya kufanya sherehe za kifahali hizo hela singesaidia kujenga shule na mahospitali?
    hii Shughuli ya Columbus haijawahi kutoke hii ni mara ya kwanza sasa tatizo liko wapi?

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 29, 2008

    Unajua Tatizo la ndungu zetu wa Bongo(baadhi) ni kama vile enzi zile za UJAMAA, kijiji kikipeleka watoto shule mjiji hawataki kusikia hata wame fika Kariakoo basi.. wakae shule tuu....ndio haya sasa.. wewe ukiwa nje ya nchi basi uwe shule au ubebe mabox tuu hakuna kingine ... fun is every where people..

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 29, 2008

    mie ni old school na nimekutana na comments kama hizi miaka kabao iliyopita.
    Jamani, kwenda out (disco, party, picnic au ugenini) sio ufahari ila ni kutanua mawazo, kuburudika na kukutana na watu tofauti. Hii ni part and parcel ya maisha yetu hapa duniani. Proportinal, naamini mbeba box pamoja na show-off yake anatumia %ndogo ya income yake kuliko afsa wa kati bongo akienda out.
    Good time inaongezea watu maisha.
    Wekeni majina yenu au nick names tufuatilie mawazo yenu. Wengine mnataka charity funds mkajidai nini?
    Blackmpingo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...