NINASIKITIKA KUWATANGAZIA KIFO CHA MAMA YANGU MZAZI ADELINA MAPANGO KILICHOTOKEA IFAKARA MOROGORO TAREHE 29/05/2008 NA MAZISHI YALIKUWA TAREHE 02/06/2008 KATIKA MAKABURI YA UKOO WA CHAHALI HAPA IFAKARA.
NAWASHUKURU NYOTE AMBAO KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE MLIUNGANA NAMI KATIKA KUMUOMBEA MAMA APONE LAKINI BWANA AMEMPENDA ZAIDI NA HATIMAYE KUMREJESHA KWAKE.
UKOO WA CHAHALI NA MAPANGO UNAWASHUKURU SANA KWA USHIRIKIANO WENU.
BWANA AMETOA BWANA AMETWAA,
JINA LA BWANA LIHIMIDIWE MILELE.
EVARIST CHAHALI
Pole sana kwa msiba wa mama yenu,je huyu mama ni mama yake raphael mapango?
ReplyDeleteR.I.P Adelina.
ReplyDeletePole sana Evarist kwa kuondokewa na Mama yako mzazi."Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi....(Zab 5:?)
POLENA SANA NA CHIVEMBO (MSIBA) EVARIST NA WENGINE KWA NIABA YA MZEE EGIDIUS LIAMPAWE WA VIWANJA SITITI TUMAWAPAPOLE.nimeguswa sasna maana mama yangupia anaitwa Adelina (liampawe). Na alitununulia kiwanja hapo kibaoni ifakara.
ReplyDeletePole Mlongo wangu Evarist
ReplyDeletekaeni mkiamini, na wakati ukifika mataonana tena.
ReplyDelete" SISI WOTE NI WA MWENYEZI MUNGU NA KWAKE TUTAREJEA" Pole sana Evarist kwa kuondokewa na mama yako mzazi nakuombea mungu akupe nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.
ReplyDeletePole sana kwa msiba wa Mama Mkuu!
ReplyDeleteBWANA ALITOA NA BWANA AMWTWAA,JINA LA BWANA LIBARIKIWE..POLENI WAFIWA..KWA MSIBA MKUBWAA
ReplyDeletePole sana ndugu yangu. Yote ni kazi ya Mungu na kazi yake haina makosa.
ReplyDeleteNimepokea taarifa hizi nikiwa nafanya kisomo cha Mama Chuma kweli nimehuzunika sana tena sana.Mungu awape faraja na kubwa ni kuiombea roho ya Bibi(yangu)ipumzishwe kwa Amani.
Chuma.
Raha ya milele umpe ee bwana na mwanga wa milele umwangazie! Apumzike kwa amani mama yetu mpendwa!! Amen. Poleni sana wafiwa (Chahali) na familia yote kwa ujumla. Freda - Shoreditch
ReplyDeletepoleni sana!
ReplyDelete