NINASIKITIKA KUWATANGAZIA KIFO CHA MAMA YANGU MZAZI ADELINA MAPANGO KILICHOTOKEA IFAKARA MOROGORO TAREHE 29/05/2008 NA MAZISHI YALIKUWA TAREHE 02/06/2008 KATIKA MAKABURI YA UKOO WA CHAHALI HAPA IFAKARA.
NAWASHUKURU NYOTE AMBAO KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE MLIUNGANA NAMI KATIKA KUMUOMBEA MAMA APONE LAKINI BWANA AMEMPENDA ZAIDI NA HATIMAYE KUMREJESHA KWAKE.
UKOO WA CHAHALI NA MAPANGO UNAWASHUKURU SANA KWA USHIRIKIANO WENU.
BWANA AMETOA BWANA AMETWAA,
JINA LA BWANA LIHIMIDIWE MILELE.
EVARIST CHAHALI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2008

    Pole sana kwa msiba wa mama yenu,je huyu mama ni mama yake raphael mapango?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 06, 2008

    R.I.P Adelina.
    Pole sana Evarist kwa kuondokewa na Mama yako mzazi."Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi....(Zab 5:?)

    ReplyDelete
  3. POLENA SANA NA CHIVEMBO (MSIBA) EVARIST NA WENGINE KWA NIABA YA MZEE EGIDIUS LIAMPAWE WA VIWANJA SITITI TUMAWAPAPOLE.nimeguswa sasna maana mama yangupia anaitwa Adelina (liampawe). Na alitununulia kiwanja hapo kibaoni ifakara.

    ReplyDelete
  4. Pole Mlongo wangu Evarist

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 06, 2008

    kaeni mkiamini, na wakati ukifika mataonana tena.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 06, 2008

    " SISI WOTE NI WA MWENYEZI MUNGU NA KWAKE TUTAREJEA" Pole sana Evarist kwa kuondokewa na mama yako mzazi nakuombea mungu akupe nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.

    ReplyDelete
  7. Pole sana kwa msiba wa Mama Mkuu!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 07, 2008

    BWANA ALITOA NA BWANA AMWTWAA,JINA LA BWANA LIBARIKIWE..POLENI WAFIWA..KWA MSIBA MKUBWAA

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 07, 2008

    Pole sana ndugu yangu. Yote ni kazi ya Mungu na kazi yake haina makosa.
    Nimepokea taarifa hizi nikiwa nafanya kisomo cha Mama Chuma kweli nimehuzunika sana tena sana.Mungu awape faraja na kubwa ni kuiombea roho ya Bibi(yangu)ipumzishwe kwa Amani.
    Chuma.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 09, 2008

    Raha ya milele umpe ee bwana na mwanga wa milele umwangazie! Apumzike kwa amani mama yetu mpendwa!! Amen. Poleni sana wafiwa (Chahali) na familia yote kwa ujumla. Freda - Shoreditch

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 09, 2008

    poleni sana!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...