MPIRA UMEISHA SASA HIVI NA CAPE VERDE INATOKA NA USHINDI WA 1-0 DHIDI YA TAIFA STARS KWENYE MCHEZO WAO WA MGUU WA KWANZA KUWANIA TIKETI YA KUCHEZA KOMBE LA DUNIA.
HAWA CAPE VERDE WALIPIGWA 2-0 NA CAMEROUN HUKO YOUNDE WIKI MBILI ZILIZOPITA NA MCHEZO UNAOFUATA WA STARS NI DHIDI YA CAMEROUN KATIKA MTANANGE UTAOCHEZWA NESHNO JIPYA DAR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 07, 2008

    Haya wadau. Maximo ametumia wiki nzima hii kuwafundisha wachezaji wa kibongo kukwamisha mpira wavuni. Leo kwa mara nyingine tena wameshindwa kukwamisha mpira wavuni.
    Toeni tena lawama kwa Maximo.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 07, 2008

    mmmmh, kwa hiyo kama cape verde walifungwa na cameroon halafu na leo wakaja kutufunga ina maana taifa stars kwa usalama wao inabidi wajikakamue na wamfunge cameroon ili kubalance mambo kitu ambacho kwangu mimi ni kama naona ndoto vile. Anyway, kila la kheri taifa stars dhidi ya cameroon wiki ijayo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 07, 2008

    Niliwaambia mkasema ohhh sijui hivi na hivi kazi hiyo sasa maana nilisema hizi droo wanazotoa nyumbani je away watashinda??Sasa ndio hapo ukisikia unatoka bila mafanikio yoyote yale ndio hayo haya sasa tuone kama watashinda nyumbani.....

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 07, 2008

    Duh jamani! Taifa Stazi walemavu au nini?labda wadosi wenzangu waisalimishe nchi hii...kweli!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 07, 2008

    wenzetu Harambee stars wamemwasha Guinea 2-0

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 07, 2008

    Wabongo na washauri mbase kwenye kucheza ngoma za asili(kukatika)mpira nadhani ni too foreign kwetu nichoshwa kila siku sisi tunalazwa tu

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 07, 2008

    Msiwe na Munkari watanzania kwani ndiyo kwanza tumeanza kujipanga upya kisoka hivyo msitake matokeo mazuri kwa muda huu mfupi tangu tuamke usingizini. Katika mafanikio ya kweli hakuna fomula ya mkato, inabidi tuwekeza muda pamoja na pesa ili soka la bongo liweze kuonekana. nadhani miaka michache ijayo kama tutaendelea na nguvu kama hii basi tutapata majibu mazuri na Tanzania kuwa kati ya nchi zinazotisha kisoka Afrika. Tuwalaumu akina Rage, Ndolanga, Wambura n.k kwa kuharibu vipaji pamoja na kutupotezea muda wetu kwa ku endekeza ufisadi. Safari hatua na tumeshaianza, tuna ndoto na tutazitimiza kama tutakuwa wavumilivu, tupeane moyo na kuwapa muda watalaam wa soka kwaandaa vijana.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 07, 2008

    Hehehe matokeo haya hayawamizi kichwa TFF. Wapo busy na mapato. Walishaanza kulifikiria kiigilio cha STAZ vs Cameroon, Hata kabla staz haijanyanua mguu kelekea Cap Verde. Sasa kitumbua ndio hicho kimedoda.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 08, 2008

    Binafsi nishachoka na timu hii wala sio kosa la mtu yoyote ila ni kosa la sisi wenyewe kutopenda kusikiliza wazee wetu.Mzee Mwinyi alishatuambia Tanzania ni kichwa cha mwenda wazimu sasa tushapoteza points 5 tayari ukijumlisha na 6 za Cameroon jumla 11!Je kuna uwezekano huko?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 08, 2008

    The population of Cape Verde in 2003 was estimated by the United Nations at 463,000, which placed it as number 162 in population among the 193 nations of the world.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 08, 2008

    Mliua UMISETA mkajiona wajanaja,sasa naangaika kutafuta washambuliaji mnakosa.Jana tena.Stars wanafika golini lakini kutumbukiza mipira nyavuni olaa!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 08, 2008

    Labda mi nisiingie kwenye ku-comment kuhusu matokeo,..ila najiuliza inakuaje kwenye mtandao wa fifa unakuta taarifa ya mchezo ina list ya wachezaji ambao hata hawakucheza (kama inavyoonesha hapa chini) na mabadiliko (substitutions) hata hayakua kama hivi....tatizo liko wapi? ndo majina waliyotoa TFF kwa waamuzi? mambo ya ajabu
    kabisa...

    (-82') (GK) Ivo MAPUNDA 1
    Meshack ABEL 2
    Amir MAFTAH 3
    Nadir HAROUB 4
    Salum SWED 5
    George OSSEY 6
    Emanuel GABRIEL 9
    Athuman IDDY 10
    (-65') Nizar KHALFAN 12
    Kelvin YONDAN 14
    Uhuru SELEMAN 18
    Substitute(s)
    Deogratius BONEVENTURE 6
    Danny MRWANDA 7
    (+82') Shaban DIHILE 13
    (+65') Kigi MAKASI 16
    Ulimboka MWAKINGWE

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 08, 2008

    TFF:Tusife90% ya comment za wanablog hapo juu zinaonyesha jinsi gani watu walivyo na Imani kwamba one day we will make.Karibu zote ni positive comments.
    Serikali:No short-cut,hata tusipofanikiwa kwenda 2010 twaweza kujipanga kwa ajili ya 2014(Nayo iko karibu).
    Ghana:Baada ya akina Abedi pelle,Tony Yeboah,walipotea kwenye soka,walikuwa wanaandaa vijana ambao tunawaona kwa sasa.tuwe na plan za mbele hata kamam hatutakuwepo,jana PM wa Uk alikuwa anaogelea U.K kuandaa World cup 2018,yeye atakuwa siyo PM tena by that time!TUENDELEE KUPAMBANA HATUWEZI KURUDI NYUMA,HATUNA PROFESSIONAL PRAYERS.THAT'IS NOT A GOOD EXCUSE'

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 08, 2008

    Timu Ya TAnzania na England Huwezi kufananisha Ila Kuna Tabia zinafanana, UWengereza Mdomo Mwingi alafu kila siku hawakumbuki vijana wadogo wak uwataarisha 2010 sawa na hii Taifa Stars.

    1. TFF wanajali sana pesa za uwanja wa Taifa naelewa ndio zinazosaidia usafiri wa wachezaji na mshahara ila wachezaji hasa midfield onesheni hazi ya Taifa.

    2. Taifa Stars waanze kuweka vijana wadogo wenye kiwango tusibague tuende mikoani tuende Visiwani wachezaji wazuri tu sio kila siku top 3 za ligi kuu.

    3. Nakubaliana na 2014 sio mbali ila tufanye kweli sasa hivi, Maximo wewe Manager mzuri lakini plz mtoe mapunda golini mrudishe Yule Dogo mwengine.

    Cape De Verde ni Nchi ndogo Nzuri sana ila kimpira Africa Rankin ni Kama wa Mwisho Aibu hii najuwa wamezaliwa wachezaji wazuri huko kama NAni wa MAnchester United.

    England nailaumu sana katika kipaji cha East Africa, tizama France na Ureno wanavyochukuwa wachezaji wa sehemu walizotawala,

    UK mnaharibi soka Yenu na Soka Yetu jamani wacheni ubaguzi njooeni mchukue vijana huku.

    Muchacho LFC.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 08, 2008

    Timu Ya TAnzania na England Huwezi kufananisha Ila Kuna Tabia zinafanana, UWengereza Mdomo Mwingi alafu kila siku hawakumbuki vijana wadogo wak uwataarisha 2010 sawa na hii Taifa Stars.

    1. TFF wanajali sana pesa za uwanja wa Taifa naelewa ndio zinazosaidia usafiri wa wachezaji na mshahara ila wachezaji hasa midfield onesheni hazi ya Taifa.

    2. Taifa Stars waanze kuweka vijana wadogo wenye kiwango tusibague tuende mikoani tuende Visiwani wachezaji wazuri tu sio kila siku top 3 za ligi kuu.

    3. Nakubaliana na 2014 sio mbali ila tufanye kweli sasa hivi, Maximo wewe Manager mzuri lakini plz mtoe mapunda golini mrudishe Yule Dogo mwengine.

    Cape De Verde ni Nchi ndogo Nzuri sana ila kimpira Africa Rankin ni Kama wa Mwisho Aibu hii najuwa wamezaliwa wachezaji wazuri huko kama NAni wa MAnchester United.

    England nailaumu sana katika kipaji cha East Africa, tizama France na Ureno wanavyochukuwa wachezaji wa sehemu walizotawala,

    UK mnaharibi soka Yenu na Soka Yetu jamani wacheni ubaguzi njooeni mchukue vijana huku.

    Muchacho LFC.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 08, 2008

    Jamani tusiwalaumu wachezaji wala Maximo, tatizo la Michezo tanzania linaanzia na Viongozi kutokuwa na Nidhamu na Maarifa ya jinsi ya kwenda mbele.
    Sasa Wazazi wakiwa hawana nidhamu unafikiria mtoto atakuwa na nidhamu.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 08, 2008

    OMBI KWA TFF!
    1:- KWA HESHIMA NA TAADHIMA NINAOMBA TENA NINAOMBA SANA MTAFUTE WATUMISHI WA MUNGU IWE MAASKOFU, WACHUNGAJI, PAMOJA NA MASHEKHE NA WA HINDU MWENDE NAO PALE UWANJA MKUU WA TAIFA MKASALI MAANA HUO UWANJA SIJAONA KAMA ULISHAFUNGULIWA KWA SALA TULIKURUPUKA TU TUKACHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA UGANDA CRANES SASA RUDINI NYUMA MKUMBUKE KUWA KILA KITU NI MUHIMU KUMTANGULIZA MUNGU MBELE BILA YA HIVYO TIMU ITAKUWA NA MATOKEO MABOVU, JIFUNZENI HATA WAKATI WA KUMUAPISHA RAIS WA NCHI KUNA VIONGOZI WA DINI WA MADHEHEBU YOTE WANAKUJA KUFANYA SALA... ZINGATIENI HILO MSILIPUUZIE


    2:- KAMA TIMU ITASHINDWA KUCHEZA ANGALAU AFRICAN CUP OF NATIONS KWELI KABISA TUNAOMBA MUWAJIBIKE KWA SABABU TIMU HAINA MATOKEO MAZURI KWA MIAKA MITATU SASA TOKA MMECHUKUA UONGOZI WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU TANZANIA.

    3:- HIVI NI KWA NINI MNATUWEKEA VIINGILIO VYA AJABU KIASI HICHO? MNAPATA UDHAMINI MKUBWA SANA TIMU INAMATOKEO MABOVU ALAFU NYINYI MNAKUJA KUTUKAMUA WAVUJA JASHO KWA KUTUWEKEA VIINGILIO VYA AJABU HIVI HII NI HALALI?? KAMA SI UFISADI WENU NA NDIO MAANA MNAOGOPA KUMREJESHA RAGE KUNDINI KUTOKANA NA MISIMAMO YAKE, HAKIKA ANGELIKUWEPO RAGE MSINGETUFANYIA UPUUZI MNATUFANYIA SASA,, NI KITU GANI MNAKIKOSA NYIE TFF MPAKA MPANGE VIINGILIO VIKUBWA NAMNA HII, HIVI UKIWEKA KIINGILIA CHA JUU KABISA 15,000/=TSH THEN CHA CHINI KABISA UKAACHA 3,000/=TSH HUO UWANJA UTAACHA KUJAA?? NA MKASHINDWA KUPATA PESA YA MAANA HAPO KWA HIINGILIO HICHO?? INAUMA SANA KWA JINSI MNAVYOKIANGALIA NYIE NA MATUMBO YENU NA FAMILIA ZENU NA WATU WALIO KARIBU NANYI MNAWAPA TICKET ZA BUREE.. HEBU PIGENI PICHA KAMA NA NYINYI MNGEKUWA MNALIPISHWA 50,000/= TSH KUJA KUANGALIA TIMU YAKO YA TAIFA MNGEKUBALI KWELI NYIE?? ACHENI TAMAA NA ULAFI USIO NA MSINGI.

    3:- KUMBUKENI WATU WANAOKUWA NA MOYO WA KUSHANGILIA NA KUIMBA MUDA WOTE WA MECHI NI WALE WANAOKAA KWENYE VITI SI ZAIDI YA 10,000.-TSH HUKO KWENYE 20, 40, 50, NI KUKAA KIMYAAA UPUUZI HUU MNABOA SANA.

    MWISHO NASISITIZIA TENA TIMU IKISHINDWA KUCHEZA AFRICAN CUP MUWAJIBIKE KUAZNIA WEWE TENGA, MWAKALEBELA, KAIJAGE ,A HIYO KAMATI NZIMA TAIFA STARS TUMECHOKA NA TUTACHOSHWA ZAIDI KAMA MTASHINDWA KUPATA NAFASI YA KUCHEZA MASHINDANO HAYO KWENYE KUNDI HILI AMBALO LINAONEKANA NI DHAIFU.

    AHSANTE...

    WILLY UDSM.... wilpac24@......com

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 08, 2008

    jamani nadhani imefika time sasa ambapo watanzania inabidi tukubali kwamba, tz kwa kandanda bado labda kucheza ngoma na imani za kichawi. Huyu maximo ni choka mbaya hana jipya na hamna alilofanya la ajabu mpaka sasa hivi. anayebishwa manake kuna mijitu mingine haina inachojua ila kubishana tu, basi na akae chini na kufanya tathmini mechi ilizocheza taifa stars tangu ilipokuwa na maximo je imesghinda ngapi? kiwango cha mpira hadi sasa kikoje. any way mpira tanzani bado labda kuanzia sasa tujenge timu ya miaka 10 ijayo.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 08, 2008

    Mie najua Watanzania hatutakosa visingizio. Asingekwenda Gabriel ungesikia mengi sana kuhusu timu hii. Leo utasikia watu wanasema angekuwepo Haruna Moshi au Kaseja mambo yasingekuwa hivi, lakini nawahakikishia kwamba bado mambo yangebaki doro.

    Kwa sasa hivi hatuna washambuliaji waliokuwa wameandaliwa tangu udogo wao. Maximo amejitahidi kwa kweli kulea wachezaji kama Tegete na Kiggi Makassy ambao wakiingia uwanjani unaona kabisa mpira tofauti.

    Licha ya jitihada za Maximo, kocha wetu wa vijana (Tinoco)ana michuano ya Copa Coca Cola pekee katika kupata vipaji vipya. Ni juu ya TFF kupitia makampuni kuanzisha michuano ya mingi zaidi ya vijana kiasi kwamba tunapata kuona vipaji vikiibuliwa na kuendelezwa.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 08, 2008

    Mimi sioni kwamba hiyo ni news hata kidogo... kwani kuna jambo gani waTanzania tunaweza zaidi ya Big Brother "na ngono"

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 08, 2008

    Je ni kwanini TFF haishughuliki kuandaa timu ya vijana baada ya kumaliza kifungo cha miaka 2 CAF?

    Juzi juzi tumepangwa kwenye ratiba ya michuano ya vijana, TFF ilichungulia ikaona wapinzani wetu kwa U17 na U20 ni DRC na Sudan wakaamua kujitoa. Sasa nasema kama ujanja ni kukimbia basi ni bora kukimbia hii michuano mikubwa kuliko ile ya vijana.

    Siku zote timu nzuri ya Taifa hujengwa kwa muda mrefu.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 08, 2008

    --Mapunda sio Kipa
    --Boban ni muhimu, muache Maximo na Kiburi chake... hawa wachezaji wawili watamkost

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 08, 2008

    kama uzalendo ndo hivi mimi sio kabisa siwezi kumvumilia maximo kadiri siku zinavyokwenda mbele matumaini yanakuwa zero hatuwezi kuvumiliana zaidi ya hapa maximo toookaaa soka ya bongo bwana eti steven mapunda anarudi kiwanjani aibu

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 08, 2008

    Duh! Kina Eto'o hawatanii. Habari kutoka tovuti ya bbc zinasema wametoa kipondo cha 3-0 huko huko Mauritius. Sitaki kufikiria maswaibu yatakayowakumba wote watakaoenda Yaounde.
    Hao kina Bikey ndio wikendi ijayo wanapitia pointi tatu hapo Dar es Salaam. Tutaweza kuzidhibiti zisiondoke? Hizi ni dalili za kutofika Angola... pointi 12 ni karibu uhakika wa safari, yaani ushindi wa mechi nne. Tumebakiza mechi nne.
    Tuongeze bidii kwa ajili ya CHAN, ACN ngoma nzito.
    Hao FIFA sijui wametoa wapi hao wachezaji kama Ossey. Ingekuwa ni mashindano ya vijana ningesema tumerudia mambo ya vijeba.
    Wadau, kuna mtu ametambua chombo kinachoonyesha mechi hizi kwa wadau walioko ughaibuni? Msaada kwenye tuta.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 08, 2008

    Mr Maximo inabidi aonyeshwe mkanda wa video wa mechi ya Simba na zamalek ya mwaka 2003 klabu bingwa ya africa ili aweze kuona jinsi Kaseja alivokuwa akicheza na jinsi alivyoookoa zile penalti zilizoifanya simba isonge mbele kwenye yale mashindano. Asiseme eti umbo lake ni dogo, lazima aangalie na ujuzi wake vile vile akiwa golini.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 08, 2008

    Tatizo ambalo timu yetu ya taifa inakabiliana nayo ni ukosefu wa mbinu za kimchezo. Wachezaji wetu wanacheza mpira sio wa kufundishwa ila kwa kutumia vipaji binafsi; matokeo yake na hayo tunayoyapata siku zote, Je mchango wa Kocha uko wapi?
    Njia nyingine mbadala ni kwa serikali yetu kuanziasha shule maalum kwa ajili ya kuendeleza vipaji vya vijana toka wakiwa wadogo kama nchi nyingi duniani na klabu nyingi zinavyojiandaa katika kuimarisha soka.
    Kwa vile kwa hivi sasa hatuna mbinu hizi mbadala na Maximo naye aendelea kupokea ushauri wa wadau wa soko; sisi ndio tuna uchungu na kuona kila siku timu yetu haifanyi vizuri. Aelewe kwamba siku tukisema basi ni basi aende akabebe maxosi kwao kwani kwao hana timu ya kufundisha huyo.
    Unauma sana tiku kutoa sare daima

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 08, 2008

    pamoja na kulaumu mr maximo pamoja na timu nzima ya taifa, embu na tuangalie tu kwa ujumla vile vile kwa nini africa magharibi ni nzuri kisoka kuliko africa mashariki. Nimekuwa nikisoma hii article na nimeona niipost hapa kwa blog ya michuzi ili wote tuweze kuelewa tatizo hasa lipo wapi. Unaweza kuclick hapa chini ili kuona article.

    http://www.guardian.co.uk/football/2004/feb/01/sport.comment

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 09, 2008

    Summary ya comments zote hii hapa:
    Tunahitaji timu za vijana kuanzia miaka kama 10 hivi kuja juu(Football academies)ndiyo tutapata timu nzuri ya Taifa.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 09, 2008

    Of all the Teams in the World,hata Cape Verde nayo itufunge?Population 500,000; kiwango cha FIFA iko nafasi ya 162 kati ya 193 (2003)?.Hebu tuone aibu kwanza.Timu ivunjwe kabisa na Kocha atembee!La sivyo TFF IVUNJWE hatuwezi kuwa na TFF ambayo haituletei mafanikio katika soka la kimataifa.Watawezaje hilo sisi halituhusu.Waliomba kazi lazima waonyeshe uwezo wao.Hapendwi mtu katika soka,ni matokeo tu yatakayo kunusuru!Leo asubuhi namsikia Kiongozi mmoja katika Tai akiunguruma bila ya haya,'Mtu akija kuchezea Taifa Stars,aje anajua soka hapa,asitegemee atakuja fundishwa kufunga magoli na Kocha wa Taifa Stars'.'Kufunga magoli mtafundishwa huko huko kwenye Klabu zaenu'.Maneno ya Kiongozi mzima hayo.WHAT NONSENSE?.Soka litaendelea hapa nchini kwa mtindo huu kweli?Kocha duniani kote lazima aajiriwe kwa mkataba wa muda mfupi,miaka miwili au mitatu.Matokeo mazuri yatafanya mkataba ule urefushwe uwe na miaka mingine miwili tena au mitatau zaidi.Akifurunda anafungasha virago.Vivyo hivyo kwa wachezaji.Timu ikiendelea kufungwa mchezaji mbovu au wachezaji wabovu wanaondolewa katika Timu ya Taifa.Lakini kwetu sisi watanzania katika kila tatizo tayari jibu lake tunalo.BONGOLALA.eti bongoland!Ya Waaaapi?Mwenye jukumu la kwenda kusaka vipaji mawilayani na katika vyuo na shule za sekondari ni nani?Klabu za Mpira ziitafutie Taifa Stars wachezaji wenye vipaji,siyo?Tumesha chezea shilingi chooni.Kombe la Dunia Afrika ya Kusini tusamehe.Tuendelee na Taifa Stars hiyo hiyo na Kocha Maximo huyo huyo.Kwani kuna hasara gani?Siku zote Mambo Poa tu au vipi!Umefungwa na timu ndogo kama ya Cape Verde leo unatamka Cameroon tutawaonyesha kazi tu,we subiri,hawa tutakufa nao,we si utaona?Yalivyo kuwa Majinga yanaitikia tu,aah kweli hawa Cameroon safari hii lazima tuwafunze adabu nyumbani kwetu!Wengine wanaitikia,kweli bwana,kama wao Cameroon wameweza siye tushindwe tuna nini?Wanaitikia,si hapo bwana,na sisi tunashangaa Cameroon watatufungaje hapa nyumbani kwetu?Mze wa Konoooooooz unayasikia hayo?ONENI AIBU KWANZA.Hiyo mechi uwanja wa Taifa mtaicheza usiku wa manane au alfajiri?Maana sielewi.

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 09, 2008

    Kuna haja ya kuandaa timu za watoto (football academies) kama tunataka kufanikiwa kisoka. Suala la Juma Kaseja, Haruna Moshi na wengine wengi hawawezi kuisadia timu ya Taifa. Tatizo la wachezaji wetu ni kwamba wengi wamekosa msingi. Kuna mdau amezungumzia Maximo aonyeshwe mkanda wa Simba vs Zamalek ili amuone Kaseja, sio vibaya pia akionyeshwa mkanda wa Simba vs Enyimba ule wa aggredate ya 7-1. What I want to share with you ni kwamba tuzungumzie set up ya mpira wetu sio individuals!

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 09, 2008

    HI,
    Maximo kweli tumekuvumilia vya kutosha,please kama unaendelea na ubaguzi,chuki binafisi kwa wachezaji ondoka right away.
    Wapi J.Kaseja, Haruna Moshi...??!!Eti Umbo...!!Please Maximo dont Judge the book from its cover,open and read it with care.......!!!!!!.
    Mdau,
    USA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...