Chifu wa Unyanyembe, Msagata Ngulati Fundikira (kulia), na Ifuma Fundikira wa ukoo wa chifu huyo wakitoka kwenye ukumbi wa bunge mjini Dodoma leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2008

    Chifu gani mtoto wa mjini namna hii? Vaa kama akina Kwa Zulu Natal, mbavu nje, pekupeku, mkuki mkononi, usinga kiunoni, n.k. Nyie mnaleta ubitozi wa tai na suti?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2008

    Asante. Umewaza kama mimi...sasa vazi gani la chief na Tai? Huyo Bitozi tu...!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 22, 2008

    mdau wa kwanza apo umenena,machifu wa sa iv mabitoz

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 22, 2008

    Anon wa kwanza baambie, baelesee batalokota benyewe kulunyavu,Ndio tabu hiyo, ya kutawazwa chienyeji cheenyeji, kama kudumisha mila eleweka kisawasawa, usilete maridadi sana maridadi sana tai shingoni ngwabi na skuna.xsizj

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 22, 2008

    Machifu, walikuwa zamani, na kwa sasa baadhi nchi za kusini mwa Afrika na Magharibi. Mdau juu hapo yupo sawia kabisa, haya yamezuka lini tena? Zamani machifu walikuwa wana sauti kubwa, labda kama ma gavana wa maeneo yao, sasa huyu brazaman yeye ni kama nani kule Tabora? Au ndio anatumia jina apate ulaji. Maana baada ya uhuru mambo haya yakawa hamna. Vaa kibwaya, ngozi, mapembe, manyoya kama babu zako, au ndio modern chifu? Tuacheni jamani, na mie itabidi nilitembelee bunge maana babu yangu marehemu Pazi Kibasila, nae alikua chifu.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 22, 2008

    kha...umangi na uchief si ulifutwa jamani? Inakuwaje leo bunge linamruhusu huyu kutembelea bungeni? Kha...kweli hili ni kofi kwenye shavu la wachagga!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 22, 2008

    Samahani wadau naomba nitofautiane na watu wanaopenda Uchifu, binafsi nachofahamu Mwalimu Nyerere ali-abolish Uchifu, sasa huyu Chifu Bungeni ameenda kufanya nini?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 22, 2008

    Machifu wengine waliotawala Unyenyembe ni Katwanga, Mputa, Mpopo, Kabundi, Nsonso, Mmanywa, Mgalula, Swetu, Fundikira I, Mwasele, Kiyungi,Isike, Nyaso, Kalunde I, Said Fundikira, Kiyungi II, Mkasiwa, Fundikira II na Abdallah Said Fundikira III.
    Ifuma Rashidi Kihiga (Alichaguliwa kwa zengwe desemba mwaka jana, kabla ya mahakama kuu Tabora kutengua uteuzi wake mwezi uliopita na kumkabidhi, huyo yanki pichani)

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 22, 2008

    Ndio ulifutwa na wakina Mwinyi na Mkapa wakaurudisha kwa Azimio la Zanzibar, kimya kimya kwa sababau hawakuamini ndoto hiyo ya kutokomeza u-Chifu!

    Eti, wanatuhubiria wana"muenzi Mwalimu"!

    Waache kutudanganya!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 22, 2008

    Uchifu ni Mawazoni na busara na namna unaishi na watu sio tai wala shanga kiunoni

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 22, 2008

    Waheshimiwa naomba nielimishwe. Hivi hawa ni watoto wa marehemu Fundikira? Just curious...

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 22, 2008

    Hebu acheni ushamba nyie!tunajua rangi yenu nyeusi kama polish ya viatu lakini kwani akili yenu pia nyeusi?watoto wote wa machifu yanasoma kule usa na wanapata elimu boro...nyie mnazubaa kubeba maboksi na kututumia picha zenu za kijinga kijinga...mie nasema bora tuwarudishe machifu kifaragha ili waiokoe nchi hii kutoka kwenye makucha ya wajinga!!!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 22, 2008

    Mwalimu alizuia uchifu lakini cha kushangaz anyumbani kwake kwenyewe kuna machifu, si mnaona unafiki wa mzee kifimbo cheza na udikteta humo humo? Kweli mwalimu aliongoza zama za wajinga ndiyo waliowao. Alikuwa msomi msiri sana ndiyo maana Tanzania haitaendelea.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 23, 2008

    Naomba kuuliza. Hiyo ni kidude gani kichwani mwa chifu?

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 23, 2008

    Hicho kidude kichwani ni taa ya dakitari wakati wa upasuaji ili aone vizuri!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 23, 2008

    Anon 23 july,1:18 umekosea, umekosea, hiyo ni taa ya kuingia nayo mgodini kwenda kujichimbia mwenyewe kwa mkono wake ....

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 23, 2008

    kadude kichwani kanaitwa SHING'WANDA

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 23, 2008

    anon wa July 22, 2008 4:30 PM, sidhani kusema kumuenzi baba wa taifa ina maana tufanye au tukubaliane na kila alichofanya. Imefika muda muafaka sasa ambao inabidi tukae na tumkosoe katika mambo flani flani. Sio kumsifu tu kama makondoo...kha! Kitu kama siasa ya ujamaa ilituumiza sana! Kuvunja u-chief imetuleta pamoja lakini ukumbuke mila na desturi zetu lazima tuwe nazo pia. Sababu kuu za kuvunja u-chief ni katika ku-'consolidate' urais wake. Machief wangefanya kitu isieleweke humu...duh...Unafanya mchezo...kudadadeki? We mchagga amezoea kupata maagizo kutoka kwa mangi mkuu, leo unakuja kumwambia nyerere kasema hichi na kile...atakuelewa?...hehehe! lakini kama wazungu wasemavyo...there are many ways to skin a cat...sasa mimi nadhani hakufuata njia sahihi, katika kutatua hili tatizo. Angeweza kutumia njia nyingine tofauti za kuleta nchi iwe pamoja pasipo kuua uchief kwa makabila baadhi baadhi tu na kubakiza katika mengine!
    Nawakilisha

    mtoto

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...