Habari za leo Kaka Michuzi!



Pole na kazi lakini kaa kukumbuka ya kwamba tunaipenda kazi yako! Nimebahatika kupata article moja ya UK inayozungumzia mchezaji yosso wa kitanzania Adam Nditi, ambaye ameweza kupewa mkataba na academy ya team ya London, Chelsea football club.




Inasemekana Adam amewahi kuchezea timu ya watoto wa klabu ya Kikwajuni kabla hajaja huku UK miezi kama saba iliyopoita na kwamba baba yake Eric Nditi alikuwa mmoja wa wazee wa klabu hiyo


Kama utaweza kupost hi habari katika blog yako utakuwa vizuri sana sio tu kwa wapenzi wa chelsea ila nina uhakika kwa watanzania kwa ujumla ambao wanapenda soka na wanataka maendeleo ya game letu.

link ya hiyo article ni:
http://www.basingstokegazette.co.uk
/news/newsheadlines
/display.var.2365867.0.blue_is_
the_colour_for_schoolboy_hotshot.php
au ukisearch jina Adam Nditi kwenye google utapa article yake.
nakutakia siku njema,
Mdau Baraka.
============================================================
Someni hii linki muone kijana huyo wa kibongo alivyopata bahati ya kusaini chelsea:
/mostpopular.var.2365867.
mostviewed.blue_is_the_colour_
for_schoolboy_hotshot.php
Mdau Ezza - Chelsea Club, Helsinki

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. thanx mdau Baraka,
    Maana katika habari ya mwanzo, wananchi walikuwa wanahoji kuwa video ya BBC haikusema kuwa anatokea wapi.

    I have also come across this video here

    I am hardcore Man Utd supporter; but I am just as happy to see a Tanzanian-born make it a Chelsea. Ingawa sadly babake anasema katika mahojiano anategemea mwanae aje kuchezea Uingereza :-(

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 10, 2008

    Mdau nalitolela kila mtu ana malengo yake.babake hana kosa kusema hivyo mwanae anategemea kuja kuchezea uingereza baadae.kama hujui kama dogo atatumia uraia watanzania baadae umri wa kusign mkataba utakapofika kwa sheria za uingereza za soka hato qualify kwani sheria inataka mchezaji yeyote kutoka nchi nyingine kuchezea uingereza lazima nchi yake isiwe chini ya 70 kwenye fifa rank.
    Kama una kumbukumbu nzuri kuna mkenya alikuwa anatakiwa kusainiwa na portmouth kama sikosei lakini ikashindikana kutokana kenya hiko chini ya namba 70 kwenye FIFA rank. Kwahio tusimlaumu mzazi wake bali tuwape pongezi kuwakilisha.
    "TUKUZENI VIPAJI VYA WATOTO"

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 10, 2008

    baba yake anatakiwa kuelimishwa kuwa amuache mtoto abaki mtanzania.
    inatakiwa dua nyingi kama kina Suleiman kalou ili kupata namba.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 10, 2008

    kunani tena hapo?mbona mzazi wake amesema anataka mtoto wake achezee Uingereza...ina maana ndo bongo keshaitupa ivo....watu bwana

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 10, 2008

    wow wow wow nice man!

    wewe nalitolela instead of being happy for the kid,eti umeweka sad face.wouldnt u want to play for uingereza?taifa stars itampeleka wapi?dont be na kijiba

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 10, 2008

    kwanini asichezee uk wakati bongo mmekataa dual nationality?hawa wako wengi tu. tunaweza jaza first eleven ya taifa stars na hawa yosso. ubovu ni kwamba walishalamba makaratasi ya huku. na bongo hawakubaliki.

    ReplyDelete
  7. Anony wa July 10, 2008 1:55 AM,
    Hiyo sheria ya kusign pro contract nchi yako iwe ranked 70 or higher imeanza lini? Mbona kuna Msierra Leone (Albert Jarrett) ambaye alikuwa trainee Arsenal, akasign Pro contract na Wimbledon mwaka 2003 akiwa na miaka 19. And yet Seirra Leone wakati huo ilikuwa ranked 135-th katika FIFA rankings. Infact, toka Dec 96 hawa jamaa hawajavuka hiyo 70-th spot barrier

    Anyways, for as long as ana professional contract (ambayo tunamuombea apate akifikia umri; cause being an academy trainee is just the first step; many of them do not make the cut), then sio lazima achukue uraia wa Uingereza or nchi nyingine. He will be earning his daily bread from his club, and (hopefully) play internationals with Taifa Stars. Playing for your country is about honor and glory.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 14, 2008

    Namtakia heri kijana, lakini chelsea hawana rekodi nzuri ya wachezaji wao chipkizi ku make cut, mfano ni timu nzima ya chelsea ni john terry pekee alotokea katika academy yao. Mara nyingi huwaacha njiani (release) au huwauza kwa timu nyengine. Ni muhimu kwa hivyo baba yake awe muangalifu sana na kumpa matumaini mwanawe lakini sio matumaini makubwa kupita kiasi, na pia ajitayarishe endapo, nasema endapo kama hatopata last cut. Muhimu atapata experience nzuri na atafumbuka macho na god knows may be akiwa mkubwa ata sign professional contract na chelsea au timu yeyote ile. all the best young man

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 14, 2008

    anonymous wa July 10, 2008 1:55 AM umeropoka utumbo mtupu, kuchezea nchi nyengine na hata hapa uk hakuhusiki kabisa na rank ya nchi alozaliwa mchezaji. kuna sheria mbili tafauti, moja mchezaji kuchezea timu yeyote nchini uingereza, na ya pili kuiwakilisha uingereza kama baba mtoto alivyosema, kuwa angelipenda mwanawe kuichezea uingereza.

    ReplyDelete
  10. hata kama July 10, 2008 1:55 AM alikuwa anazungumzia suala la kuchezea timu ya taifa, bado hayuko sahihi. Kwa sheria za UK, na kwa makubaliano ya mwaka 1993 kati ya vyama vya mipira vya "Home Nations", ukipata passport ya UK, unaruhusiwa kuchezea any of the 4 Home nations, i.e. England, Wales, Scotland or N. Ireland. Hakuna kipengele chochote kinachozungumzia nafasi ktk FIFA ranking ya nchi ulikozaliwa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...