Mjadala kuhusu mchango wa magazeti ya “Udaku” katika kujenga au kubomoa jamii una historia ndefu sana. Ni mjadala ambao ulikuwepo,upo na utaendelea kuwepo labda mpaka hapo itakapotokea kwamba maisha na watu watapotea katika sura ya ulimwengu.

Binadamu anabakia kuwa kiumbe mdadisi anayependa kupata habari,kujua kinachoendelea na pia hata kujua alichokifanya jirani yake jana usiku kama sio alichokifanya au anachokifanya mkuu wa nchi awapo mapumzikoni.

Nchini Tanzania, baada ya mapinduzi ya habari na mawasiliano,yaani baada ya kuvuka kile kipindi ambacho kulikuwa na magazeti matatu na kituo kimoja cha redio, paliibuka magazeti ambayo baadaye tumekuja kuyaita “magazeti ya udaku”. Hapo ndipo nasi tulipoingia rasmi kwenye mjadala wa; Je magazeti haya yana mchango gani katika jamii? Yanajenga au yanabomoa?

Hivi karibuni tulipata fursa adimu ya kufanya mahojiano na Abdallah Mrisho Salawi (pichani) Meneja Mkuu wa kampuni inayoongoza kwa uchapishaji wa magazeti ya “udaku” nchini Tanzania ya
Global Publishers.

Pamoja na mambo kadha wa kadha kumhusu yeye binafsi, Abdallah Mrisho anajaribu kueleza kuhusu kazi zao kama wanahabari na mchango wao au ubomoaji wao wa jamii.Hiyo itatokana na unavyoona wewe hasa baada ya kusoma alichotuambia Abdallah Mrisho. Mambo yote hayo na mengine nenda http://bongocelebrity.com/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 09, 2008

    Hongera ndg Salawi na watu wote wa GPL,kazi yenu ni nzuri na tunazikubali. Ila zina maadui wengi. Pia tunaomba nanyi msiangukie ktk ufisadi. Mfano ni kwako. Kuna mtu aliniambia kuwa fremu tupu za miwani kama hizo ulizovaa zinauzwa sio chini ya shs 450,000/=. Hapo bado vioo(glasses),Sasa sijui kama ni kweli au la. Mimi simo najitoa!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 09, 2008

    magazeti ya udaku yanamaliza brain cells za vijana wetu. Ingekuwa vyema kama tungekuwa na magazeti mengi yanayoandika makala zilizoenda shule (makini), ili vijana wetu wasome. Inashangaza sana kuona sikuhizi mtumishi mkubwa wa serikali akiwa kwenye Shangingi VX na anasoma gazeti la udaku. There need to be a nationwide revolution regarding reading, hasa hasa vitabu na sio udaku. Waste of time.
    Msoffe,
    Vienna

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 10, 2008

    I can't stand the demonisation that exists in those rubish(Udaku), i remember when Shigongo was accusing Gen. Ulimwnengu when he was trying to coment on those kind of Udaku and saying he is trying to envy him....i felt disgusted and ashamed because though in business sense Shigongo had a point but still Gen. Ulimwengu had a valuable point compared to Shigongos'.
    Normally Ulimwengu were writing the Issues that are beneficial to the society compared to Udaku which normally is writing about speculations "majungu" and evil mind things...they are selling because of the problems the World is in where moral decay is nolonger an issue.
    Udaku is selling more but is killing alot of young guys and middle aged minds...to me is like selling cocaine. You get alot of money for the expense of ruining others.
    So i'm not in favour of udaku like not being in favour of cocaine....

    "Udaku" is flourishing because now the World is full of bad people controlled in moral decay and because of their abudance, they represent normal and those who abide to the moral behaviour look abnormal....that's why Mr. Salawi is happy because he is part of something bigger in demonising our society.

    But my brother you could thing how many young life you've ruined...you couldn't allow your pic being displayed........The difference of you with cocaine dealer is because you have been let out to be legal though the damage you are making to the society is enormous.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...