wadau wa zenji wikiendi hii wamelamba nondozzz katka chuo kikuu cha cardiff university of wales nchini uingereza, katika mahafali ya 125 tokea kuanzishwa rasmi kwa chuo hicho. katikati ni Abdallah Mitawi, shoto ni Mwanaharusi Ali Mohamed na kulia ni Shinuna Said Bakar Jecha, Abdallah na Mwanaharusi wamehitimu degree ya pili yaani MA katika International Public Relations na Shinuna amemaliza degree ya pili ya Uandishi wa habari MA media studies.


Ongereni sana, sasa rudini nyumbani mkajenge nchi
ReplyDeleteJamani tuwewaangalifu na maneno tunayotumia hasa kwa upande huu wataaluma.Kunatofauti kubwa sana kati ya degree ya pili na MA.Kwa ufupi tu ni kwamba unaweza ukawa una degree hata 3 lakini ukawa huna MA. Kwahio jaribuni kuwa kuwa waangalifu.
ReplyDeleteHongereni sana, karibuni nyumbani tusaidiane kujenga Taifa letu changa.
ReplyDeleteAnaomba wasamaria fedha za matibabu milioni 2.5/-
ReplyDelete2008-07-20 12:49:59
Na Godfrey Monyo
Ngongo Tully Japhet (23) anawaomba wasamaria wema kuokoa maisha yake kwa kumchangia fedha za kusaidia matibabu anayotarajia kuyafuata nchi jirani ya Kenya.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, alisema anasumbuliwa na uvimbe usoni ambao umemtesa kwa miaka kadhaa na kwamba jitihada za kutafuta tiba hapa nchini hazijaleta mafanikio.
Bi.Ngongo anasumbuliwa na uvimbe katika sehemu ya paji la uso na tatizo hilo lililoanza mwaka 2001 na tayari amekwenda hospitali kadhaa za humu nchini ikiwemo hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Muhimbili , Ocean Road na KCMC mkoani Kilimanjaro lakini tatizo lake limeshindikana.
Aliiambia Nipashe kuwa ugonjwa huo ulianza kumsumbua 2001 na mwaka 2002 alikwenda katika hospitali ya Rufaa Mbeya na kuchukuliwa vipimo lakini hakupata tiba ya kumponyesha .
Alikwenda hospitali ya Muhimbili na kupimwa kisha kupelekwa Ocean Road ambapo uvimbe uliondoka baada ya kutibiwa kwa mionzi na ugonjwa huo kupona.
Lakini alisema ulirudi tena na alipokwenda Ocean Road walimweleza kuwa hawawezi kumtibu ndipo akaamua kwenda hospitali ya KCMC mkoani Kilimanjaro nako mambo hayakuwa mazuri kwani walisema hawana ujuzi na utaalamu wa kumsaidia.
Alisema baadhi ya watalaamu wamemshauri kwenda Kenya kwa matibabu ambayo uchunguzi umeonyesha kuwa yatagharimu karibu Sh. milioni 2.5 na kuwaomba wasamaria kumsaidia.
Aliwaomba watakaomchangia misaada yao ifikishwe kwenye akaunti namba 2091600513 iliyoko kwenye Benki ya NMB na wakitumia jina la Ngongo Tully Japhet. Alisema fedha hizo ni kwa ajili ya usafiri, malazi, chakula, dawa, vipimo na kuwahudumia yeye pamoja na huyo atakayekwenda naye.
Wewe Monyo!
ReplyDeleteTuma ombi lako rasmi kwa Michuzi liwekwe kama taarifa tutakusaidia sio kuweka chini ya picha za wenzako.
Hongerani sana Watanzania wenzetu. karibuni nyumbani lakini hakikisheni mnachuma sana huko kwanza mkija huku matajiri ili mafisadi wasiwarubuni
ReplyDeleteNampenda hiyo degree ya Mass communication basi tu sina uwezo. Hongereni sana
ReplyDeleteHongereeni saanaa wahitimu.Mrusi nyumbani tuendelee kujenga Taifa letu
ReplyDeleteDulla, Mwanaharusi na Shinuna, Hongereni sana, am pround to see young zanziabri's / Tanzanians wameenda shule. Tunatawakia utendaji uliotukuka mukirudi TZ/znz so please musituangushe na nawaombea Mungu awaongoze kutilitumikia Taifa kwa kutumia utaamu na ujuzi mulioupata. Tunawahitaji sana - Khamis
ReplyDeletetunashukuru,ila mbona kila mtu anatwambia turudi,tutarud ufisad ukiisha,tunaogopa kufisadiwa
ReplyDeletehaturudi sisi wazanzibar yakhe makaratasi mbele
ReplyDeletewasichana visiwani hawahitaji sumu za kuchuna ngozi ili waonekane weupe hongera kwa yote wengiwasichana wetu hapa BONGO wapate rangi kama zenu kwahiyo zitunzeni
ReplyDelete