wadau wa zenji wikiendi hii wamelamba nondozzz katka chuo kikuu cha cardiff university of wales nchini uingereza, katika mahafali ya 125 tokea kuanzishwa rasmi kwa chuo hicho.
katikati ni Abdallah Mitawi, shoto ni Mwanaharusi Ali Mohamed na kulia ni Shinuna Said Bakar Jecha, Abdallah na Mwanaharusi wamehitimu degree ya pili yaani MA katika International Public Relations na Shinuna amemaliza degree ya pili ya Uandishi wa habari MA media studies.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 21, 2008

    Ongereni sana, sasa rudini nyumbani mkajenge nchi

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 21, 2008

    Jamani tuwewaangalifu na maneno tunayotumia hasa kwa upande huu wataaluma.Kunatofauti kubwa sana kati ya degree ya pili na MA.Kwa ufupi tu ni kwamba unaweza ukawa una degree hata 3 lakini ukawa huna MA. Kwahio jaribuni kuwa kuwa waangalifu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 21, 2008

    Hongereni sana, karibuni nyumbani tusaidiane kujenga Taifa letu changa.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 21, 2008

    Anaomba wasamaria fedha za matibabu milioni 2.5/-

    2008-07-20 12:49:59
    Na Godfrey Monyo


    Ngongo Tully Japhet (23) anawaomba wasamaria wema kuokoa maisha yake kwa kumchangia fedha za kusaidia matibabu anayotarajia kuyafuata nchi jirani ya Kenya.

    Akizungumza jijini Dar es Salaam, alisema anasumbuliwa na uvimbe usoni ambao umemtesa kwa miaka kadhaa na kwamba jitihada za kutafuta tiba hapa nchini hazijaleta mafanikio.

    Bi.Ngongo anasumbuliwa na uvimbe katika sehemu ya paji la uso na tatizo hilo lililoanza mwaka 2001 na tayari amekwenda hospitali kadhaa za humu nchini ikiwemo hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Muhimbili , Ocean Road na KCMC mkoani Kilimanjaro lakini tatizo lake limeshindikana.

    Aliiambia Nipashe kuwa ugonjwa huo ulianza kumsumbua 2001 na mwaka 2002 alikwenda katika hospitali ya Rufaa Mbeya na kuchukuliwa vipimo lakini hakupata tiba ya kumponyesha .

    Alikwenda hospitali ya Muhimbili na kupimwa kisha kupelekwa Ocean Road ambapo uvimbe uliondoka baada ya kutibiwa kwa mionzi na ugonjwa huo kupona.

    Lakini alisema ulirudi tena na alipokwenda Ocean Road walimweleza kuwa hawawezi kumtibu ndipo akaamua kwenda hospitali ya KCMC mkoani Kilimanjaro nako mambo hayakuwa mazuri kwani walisema hawana ujuzi na utaalamu wa kumsaidia.

    Alisema baadhi ya watalaamu wamemshauri kwenda Kenya kwa matibabu ambayo uchunguzi umeonyesha kuwa yatagharimu karibu Sh. milioni 2.5 na kuwaomba wasamaria kumsaidia.

    Aliwaomba watakaomchangia misaada yao ifikishwe kwenye akaunti namba 2091600513 iliyoko kwenye Benki ya NMB na wakitumia jina la Ngongo Tully Japhet. Alisema fedha hizo ni kwa ajili ya usafiri, malazi, chakula, dawa, vipimo na kuwahudumia yeye pamoja na huyo atakayekwenda naye.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 21, 2008

    Wewe Monyo!
    Tuma ombi lako rasmi kwa Michuzi liwekwe kama taarifa tutakusaidia sio kuweka chini ya picha za wenzako.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 21, 2008

    Hongerani sana Watanzania wenzetu. karibuni nyumbani lakini hakikisheni mnachuma sana huko kwanza mkija huku matajiri ili mafisadi wasiwarubuni

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 21, 2008

    Nampenda hiyo degree ya Mass communication basi tu sina uwezo. Hongereni sana

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 21, 2008

    Hongereeni saanaa wahitimu.Mrusi nyumbani tuendelee kujenga Taifa letu

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 21, 2008

    Dulla, Mwanaharusi na Shinuna, Hongereni sana, am pround to see young zanziabri's / Tanzanians wameenda shule. Tunatawakia utendaji uliotukuka mukirudi TZ/znz so please musituangushe na nawaombea Mungu awaongoze kutilitumikia Taifa kwa kutumia utaamu na ujuzi mulioupata. Tunawahitaji sana - Khamis

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 21, 2008

    tunashukuru,ila mbona kila mtu anatwambia turudi,tutarud ufisad ukiisha,tunaogopa kufisadiwa

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 21, 2008

    haturudi sisi wazanzibar yakhe makaratasi mbele

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 21, 2008

    wasichana visiwani hawahitaji sumu za kuchuna ngozi ili waonekane weupe hongera kwa yote wengiwasichana wetu hapa BONGO wapate rangi kama zenu kwahiyo zitunzeni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...