warembo wakipata maelezo juu ya nyumbani kwa mwalimu butiama
chifu wanzagi akiongea na warembo butiama
mamiss na msafara wao wakipata maelezo ya nyumba za butiama
mamiss wakizunguka kuangalia mandhari nzuri ya kijijini butiama
warembo wakiweka mashada ya maua kwenye kaburi la baba wa taifa butiama
hii ziara ya butiama ni mojawapo ya shughuli ambazo watembo hawa wamekuwa wanazifanya katika ziara yao ya wiki moja jijini mwanza wakati wakijiandaa kupanda jukwaani kesho usiku kwenye ukumbi wa nssf kushindania taji la balozi wa redds. ziara hii imefadhiliwa na kuratibiwa na kilaji cha redds premium cold kinachotengenezwa na tanzania breweries limited

Mwalimu kama ninavyomuelewa angewatoa baruti. Yeye alikuwa ni mjamaa shika jembe ukalime mambo ya uzuri alikuwa haendekezi hivyo!
ReplyDeleteBwana Michuzi, naomba nikurekebishe kidogo. Hayo maelezo yanayotolewa na Chifu Wanzagi, hayatolewi "juu ya nyumba" ila ni maelezo "kuhusu nyumbani".
ReplyDeleteWote wanaonekana wamesimama chini au uwanjani na siyo juu ya nyumba.
Nashukuru kiswahili bado kinapanda pamoja na miaka hii kibao niyotokomea ughaibuni na kujifunza na kuzitumia lugha kadhaa.
Mdau.
Hahahahaha...kweli kabisa. Kwanza wasingewaza hata kufunga hiyo safari ya kwenya huko. Labda kama wangetumia kisingizio cha kwamba wanaenda kumsaidia kupalilia mashamba yake.
ReplyDeletehuyo dada kaweka goti kwenye kaburiii, au nina malienge?
ReplyDeleteAngewahenyesha shambani toka saa mbili hadi saa tisa alasili bila kupumzika wakipalilia au kuvuna "obhuyemba, amalingwa, obhukanhu" na mazao mengine, hasa ulezi!
ReplyDeleteHuyo "Muswati" wa Uzanaki anaweza kujipatia mchumba...(Cheka!
Mimi bado najiuliza.
ReplyDeleteMara ghafla mwl anafufuka hapo sijui hao warembo wangemwambia nini.Yaaani sipati picha.Nakumbuka utu tujineno wakati uleee wa nanii wakati nanihii anataka kugombea uraisi "....Yaani Tanzania,Kenya,Uganda tuwe na vikao vyetu vya maraisi.Mara inatokea udhuru kuwa samahani ndg wajumbe rais wa Tanzanai hatofika kwa sababu ana mimba.Sitaki na nimesema sitaki.Kwetu ni Butiama bwana....."yaani wewe hapo bana tu sauti itoke orijino.Yego
Majita
Kwani si alipiga hii biashara vita miaka ya sitini kutokana na maadili? Au mnataka tu kumdhihaki, tumerudi!
ReplyDeleteHivi si wanalipia hapo kwenda kupaangalia au ni bure. kama panalipiwa basi hamna hoja lakini kama ni bure na wameenda ni kumdhalilisha mwalimu. Sera yake na haya mambo ilikua kama maji na mafuta. Kwanza akiangalia kanchi bado kanajisukuma halafu leo unaleta warembo
ReplyDelete