Kaka Michuzi,
Mimi ndiye niliyeleta picha na ile habari za Vingunguti Dktzzzzzzzzz
Ukweli tangazo lenyewe liko Muhimbili na mwenyewe yupo Vingunguti Relini.
Haya ni maajabu mengine labda wateja wake wengi wapita mitaa ya Muhimbili
Lakini pia kwa kuweka Tangazo karibu na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (ambayo mimi ni mdau wake) lenye maandishi "USIKUBALI KUKATWA MGUU" anataka kuwaambia nini madaktari bingwa wa Mifupa ambao wakati mwingine hutoa ushauri wa kukata mguu??
Ni kweli lazima waganga binafsi waheshimiwe maana wana mchango kwa jamii na ni wa muhimu lakini labda matangazo mengine yawe yanahakikiwa kabla ya kubandikwa
Hiyo elimu ya kuunga mifupa kwa kutumia mionzi ya jua ni vema tukajifunza ili kupunguza gharama jua ni la bure.
Je wako tayari kufundisha watu??
Kama inalipa nakwambia si muda mrefu hatutakuwa na watu waliokatwa miguu katika jamii yetu.
Napenda sana kupata hiyo technology
Kuna mdau mwingine alisema X-ray haitibu ni kweli nadhani nilipitiwa katika kuandika
X-ray ni kipimo tu HAITIBU.
Nawashukuru wadau kwa kuendelea kuchangia
Mdau Obed
Muhimbili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 19, 2008

    wewe mheshimiwa uliyeleta tangazo hili shukrani na pongezi.
    lakini napenda pia nikukosoe kwamba naona ume apologize kwamba ulikosea kwa kusema x-rays inatnatibu.NIKWELI HUKUKOSEA,labda tu hapo ulipo hakuna hiyo technology,lakini ukweli nikwamba x-rays katika dozi maalum hutumika kutibu kwa kuziua cells zisizo hitajika.na ktk dozi fulani hutumika kwa diagnostic purposes.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 19, 2008

    Mimi naona ni uhuru wa biashara tumeshakua capitalist country kwa hiyo mwachieni na yeye afaidike...

    Hiyo hospital kama inatibu basi watu hawatajali hili tangazo na huyu babu kama keshawasaidia watu basi angeweka hata ref number zao....Na pia kama nilitibiwa nikapona na mimi nitamshauri mtu aende huko lakini kama hajaponyesha mgonjwa hata mmoja basi atatangaza mpaka achoke.


    Ila matangazo ya vitambaa mimi ndio wala simfagilii.....Huo ni uchafu wa mazingira ...angetafuta bango la kulipia na kuweka matangazo yake kama ni mganga mwenye kueleweka

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 19, 2008

    ebwana e,nyie ni madokta?sidhani kama hapa wanamaanisha x rays but they actually mean radiative substances.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...