Wadau tangu jana ninaigiza katika sinema, Edge of Darkness, hapa Boston. Stelingi wake ni Mel Gibson na Robert DeNiro.

Ninacheza kama askari polisi wa kike (background). Nitaitwa mara kwa mara kuigiza kwenye background hadi wanapomaliza ku-shuti mwezi Desemba.

Nilipatwa na butwaa nilipopigiwa simu wiki mbili zilizoipita na kuambiwa kuwa nimechaguliwa na mwongoza sinema, kuwa askari kanzu wa kike. Na tena si kwa siku moja tu.Haturuhusiwi kupiga picha kwenye set hii nimepiga mwenyewe Dressing Room.

Ninavaa bastola bandia na madude mengine wanaovaa polisi wa Boston.Mel Gibson mtu poa sana, jana alikuwa anatuchekesha kwenye set, leo alikuja kula lunch kwenye meza tuliyokuwa tunakula. Kaongea vizuri tu na sisi. Tulishangaa kuona mtu "A" list kama yeye anafanya hivyo. Mara nyingi wanaenda kula kwenye trela au hoteli lakini siyo na extras.

Haya nitawapa updates.

Mcheza sinema, Gbenga Akkinabe (The Wire) mwenye asili ya Nigeria anaigiza kwenye hiyo sinema kama mpelelezi. Nimeongea naye kidogo, alisema kuwa ana marafiki wengi kutoka Tanzania huko New York.

Habari na picha kutoka:
-------------------------------------------------------
Hongera sana da'chemi kwa mafanikio yako ambayo yanakuja taratiiiiiiiibu. iko siku tutasikia wewe ndiye stelingi. ukija bongo tutakuwa tunakugombea kama kina will smith. he, mbona watani wa jadi watatukoma! iko siku dada, kaza buti tu
-michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. hahahahah watatukoma sana tu watani wetu halohalooo,da chemi hongera na umependeza na nguo hizo.

    ReplyDelete
  2. kaka michuzi nimeona maada kwa da chem kuwa mtoto alazimwishwa kufanya mapenzi na mbwa,itakuwa uzuri ukaitoa kwako ili ijadiliwe,inasikitisha sana

    ReplyDelete
  3. Michuzi,

    Asante sana.

    Na ninakutakia Happy Birthday!

    Chemi

    ReplyDelete
  4. Inatia moyo na kufurahisha sana kuona watanzania sasa mambo yetu safi pande hizo nice mysister do it .

    ReplyDelete
  5. Dada Chemi!!

    A hero is an ordinary individual who finds the strength to persevere
    and endure in spite of overwhelming obstacles."

    Well done! and keep it up.

    Yasini - UKerewe

    ReplyDelete
  6. Tulikuwa US tunajua kwa nini dada chem umechaguliwa. Majority ya security guard wapo kidogo kwenye watch list na ma diet physician.

    ReplyDelete
  7. Huyo NDO Dada Chiku.. Kama umesoma zile sorded stories za Mapenzi..

    Holla!

    ReplyDelete
  8. Chemi hakuchaguliwa kutoka kwenye group of secutity guards. Amepata nafasi kutokana na her acting resume na fit kwenye position aliyotakiwa kucheza. Hongera dada yetu and keep it up!

    ReplyDelete
  9. nampongeza mtanzania mwenzetu chemi che mponda,maana tukiitizama movie hiyo pia tutapata cha kuonyesha kwa wenzetu kuwa huyo naye ni mtanzania. hongera chemi.
    MZEE YASIN -UKEREWE napenda mimi niongeze definition yangu ya a hero!!nikizingatia neno lenyewe na matumizi yake maranyingi.
    - a hero in most cases is an individual dare to act stupidly whose stupidity turn out with postive rewards either to him/herself or to others,otherwise when he/she doen't make it out he/she apears to be a fool and stupid one!hahaha
    DOUBLE 'P'

    ReplyDelete
  10. Da-Chemponda, hilo jicho, mashallah. Mwanamke jicho eeh!!!!!

    ReplyDelete
  11. He watani wetu wa jadi wamekua kwenye extras za movies tangu zamani . Kwa mfano Out of Africa hata sisi wabongo pia tulikua extras.

    ReplyDelete
  12. jamani kawaambieni yeye yuko kama extras siyo actor

    ReplyDelete
  13. Anony 5:27 Background ni sawa na extra.

    Hongera Dada Chemi tunagojea kwa hamu kusikia una role kubwa. Unaanza chini na kupanda kwenda juu! Kwa sisi wabongo umefika mbali.

    Kuna shombe fulani huko Hollywood wala hasemi asili yake ya TZ! Anaona haya! Wee Dada Chemi unatangaza Tanzania. Asante.

    ReplyDelete
  14. Wadau wenzangu. Huyu dada ni mwanachama wa Screen Actors Guild. Hicho ni chama kikubwa sana huko Marekani akina Denzel, Halle Berry, Angela Bassett wamo. Mafanikio yake si madogo ingawa kwa sasa anaigiza kama extra. Navyoelewa kuna watu ambao wanajitahidi miaka kuingia kwenye hicho chama lakini wanashindwa. Hongera sana dada yetu.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 31, 2013

    Hongera kwa kuendeleza kipaji chako cha kuigiza na kuandika habari.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...