


Picha na habari na mdau John Nditi, Morogoro
MCHUNGAJI wa Kanisa la Sabato la Segerea ,Jijini Dar es Salaam, Albano Mkadi (55) ni miongoni mwa watu wawili waliofariki dunia kwenye ajali ya basi la Kimambo Express iliyotokea juzi ( Agosti 25) katika Barabara kuu ya Morogoro- Dar es Salaam . eneo la Nane Nane mjini Mkoani Morogoro.
Pamoja na Mchungaji huyo kutambuliwa na ndugu zake pia mwili wa marehemu mwingine aliyefariki katika ajali hiyo umetambuliwa kwa jina la Job Ibrahim (20) ambaye alikuwa ni utingo wa basi hilo na mkazi wa NHC Igofu, Wilayani Mpwapwa , Mkoani Doddoma.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Thobias Andengenye, alithibitisha jana mjini hapa kutambuliwa kwa miili hiyo iliyochukuliwa na ndugu zao ili kufanyiwa shughuli za kuzikwa katika maeneo yao waliyozaliwa.
Alisema maiti ya mchungaji huyo, imechukuliwa na ndugu zake na kusafirishwa kwenda kuzikwa Wilayani Muheza , Mkoani Tanga, ambapo mwili wa Utingo wa basi hilo umechukuliwa na ndugu zake na kwenda kuzikwa Wilayani Mpwapwa , Mkoani Dodoma.
Hata hivyo Kamanda huyo wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, alisema majeruhi waliolazwa 36 walilazwa katika Hospitaali ya Mkoa wa Morogoro baada ya kutokea kwa ajali hiyo, 14 wameruhusiwa kwanda nyumbani na kubakia 22 wakaiwemo na wawili ambao halizao kwa juzi zilikuwa si nzuri.
Ajali hiyo ilitokea Agosti 25, mwaka huu majira ya saa 3 asubuhi baada ya basi lenye namba T 268 AQM aina ya Scania kupinduka katika eneo hilo la Nane Nane, mjini hapa na kusababisha vifo vya watu wawili na kuwajeruhi abiria 36.
Kwa mujibu wa Kamanda huyo, chanzo cha kutokea kwa ajali ni uzembe wa dereva wa basi kwa kugonga gari lililokuwa mbele yake yenye namba za usajili T 352 AHP aina ya Toyota mark II iliyokuwa ikiendeshwa na PC Jamal iliyokuwa inakatisha kulia na dereva wa basi hilo, Fulmence Masawe (32) mkazi wa Mpwapwa, Mkoani Dodoma bado anashikiriwa na Polisi.
Katika hatua nyingine, waumini wa 14 wa Kanisa la Tanzania Asembles of God , (TAG) ilililopo Kata ya Mazimbu, Manispaa ya Morogoro wamenusurika kufa baada ya ukuta wakanisa hilo kuwaangukia wakiwa katika ibada ya Jumapili na kuwajeruhi sehemu mbalimbali za miili yao.
Tukio hilo lilitokea Agosti 24, mwaka huu majira ya saa 8 mchana wakati wakiwa katika maombi , ambapo wote walipatiwa matibabu na kuruhusiwa kurudi nyumbani.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro , hakuna muumini aliyeumia zaidi katika tukio hilo la kuanguka kwa ukuta huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...