Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein na mkewe Mama Mwanamwema Shein, wakiangalia mitego ya nyuki katika kituo cha msitu wa Muganza Wilayani Kibondo wakati alipotembelea kituo hicho kwa lengo la kuona maendeleo ya mradi huo leo.
Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akisalimiana na mtoto Elius Chegecha ( 10) anaesoma darasa la kwanza katika Shule ya msingi Kakonko Wilayani Kibondo wakati alipofika katika kijiji hicho kwa ajili ya kuangalia hifadhi ya maendeleo ya mradi wa msitu wa asili wa Muganza Wilayani Kibondo leo.
Mmoja wa wazee wa kijiji cha chokabongo Wilayani Kibongo Mkoani Kigoma Bibi Hamisa Mrisho akimkabizi zawadi ya Mahotpot Mke wa Makamu wa Rais Mama Mwanamwema Shein alipotembelea katika kijiji hichi kuangalia miradi ya maendeleo leo.

Kaka michu naona hapo mke wa Mh Makamu wa rais anapewa Nyungo sio Mahot pot. Ama kibongo bongo inakuweje hapo?
ReplyDeleteMdau Ughaibuni
Jamani picha ya tatu Mrs Shein viatu vyake mbona sivielewi
ReplyDeletemichu huyu baba kwli ni mwana chukua chako mapema, kwani hawa watu kambarage ndo alikuwa anawatafuta mtizawe mke wake jamani mh baba wa watu hana makubwa
ReplyDeleteAnon. wa pili inabdidi uelewe tu kuwa huyo ni bi mkubwa wetu, sasa hivi stileto hazimfai tena,
ReplyDeletePia ni utamaduni wa wazanzibar walioupokea enzi za usultan, wa kuvaa mitarawanda na makubadhi hivyo si shani kwao viatu vya mchuchumio au dumbukiza kila wakati, na ukichunguza kwa makini wengi wa wakaazi wa huko hata ikiwa kiatu kina kisigino bado kitakuwa cha kuchomeka, na hiyo ni kwa kurahisisha kwa matembezi na urahisi wa kuvua kwa haraka anapotaka kuingia ndani ya nyumba yake au nyumba ya ibada upo hapoooo