mdau lilly majuzi alitembelea mikoa ya kusini na kutuletea picha hizi akisema siku hizi barabara ya kuelekea huko ni mkeka tu. yaani mtu sasa unaweza kwenda na teksi bila matatizo na kwa muda mfupi tofauti na zamani. hakika bongo inazidi kuwa tambarare....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Kaka michu, huyo lilly anataka kupotosha jamii, kwasababu kuna kipande bado kichafu sana kinaitwa " km 60" au ndundu - somanga. hicho kipande ni noma tupu, ikipiga mvua moja tuu unakesha.
    Mdau wa sauzi - chingaboy

    ReplyDelete
  2. kwanini wanaweka mstari mweupe katikati instead ya wanjano?mweupe ni kutenganisha barabara mbili zinazoelekea upande mmoja,hapo katikati inatakiwa wa njao na sio mweupe

    ReplyDelete
  3. Chingabao naungana na wewe kiaina, baada ya daraja la Mkapa Rufiji kuna kipande kimoja cha barabara kibovu ajabu, hukai kwenye kiti maana unarushwa mpaka unagusa juu ya basi. Ila huku kwengine kwa kweli tunashukuru kuzuri sana.

    ReplyDelete
  4. Serikali kuu mbona imeisahau mkoa wa zanzibar!!

    ReplyDelete
  5. Anonymous wa August 14, 2008 11:03 AM unapaswa uelewe kuwa hakuna universal way ya kufanya mambo inategemea na system ya nchi husika, ndio maana kuna nchi wanaendesha kushoto mwa barabara na nyingine wanaendesha kulia, kuna nchi wanatumia umeme 120v wengine 220 volts just to list a few

    ReplyDelete
  6. Anony wa 11:03 AM rangi za barabara zinatofautiana from one jurisdicition to another.

    Kwa urahisi tu angalia hapa:
    http://images.google.ca/images?hl=en&client=firefox-a&rls=org.mozilla:en-US:official&hs=meM&q=road+lines&um=1&ie=UTF-8&sa=X&oi=image_result_group&resnum=1&ct=title

    Nadhani upo N. Ameica au sio? Sisi system yetu tumerithi UK. Soma hapa kwa mfano
    http://www.walthamforest.gov.uk/index/transport/parking-roads/env-road-markings/env-road-markings-yellow.htm

    ReplyDelete
  7. Ndanda mpaka Somanga bado. Hii ni kilometre 60 lakini inachukua masaa mawili ukienda kwa speed ya kasi ya 30km/h. Jamani mbona huyu dada hasemi ukweli. Majuzi tu serekali ilisaini mkataba na mkandarasi M/s Kharafi ili ajenge hicho kipande. Mimi kinaniboa sana maana kwasasa siwezi endesha benzi langu mpaka kijijini kwetu karibu na Kipatimu, Kilwa.

    ReplyDelete
  8. anon wa pili nadhani upo marekani ama nje ya tz.Kwa taarifa yako kila nchi ina kanuni na staili yake.Kwa bongo mapigo yetu ni mstari mweupe.

    ReplyDelete
  9. KATIKA KITU AMBACHO WAKAZI WA HILI ENEO BARABARA YA KIBITI LINDI WALICHO LAANI NI KUJENGWA KWA HII BARABARA KWANI IMEWAONDOLEA KITEGA UCHUMI CHAO KIKUBWA KILICHOKUWA KINATEGEMEA UBOVU WA HII BARABARA, KWANI WAKATI WATU WAKIKWAMA NA SAFARI ZAO WAO NDIPO BIASHARA ZAO ZILIKUWA ZINA SHAMIRI.SASA WATACHUKUA MUDA KUPATA BIASHARA MBADALA.

    ReplyDelete
  10. Mstari mweupe ni katikati kam UK, sisi tumerithi sheria za UK as our former masters, na mstari mweupe ni kweli unatenganisha barabara mbili zikeelekea mbande opposite, na ukiona upo moja kwa moja yaani si dash dash ina maana hapo hurusiwi ku-overtake na ukiuona dash dash unaruhusiwa ku-overtake, na mstari wa njano pembeni ukiuona ina maani ni mwisho wa barabara kwa magari na pia una maana huruhusiwi ku-park gari hapo. ukitumia google.com unaweza kupata habari hizi zote nchi kwa nchi.

    ReplyDelete
  11. Anonymous wa August 14, 2008 11:03 AM
    Tatizo lako unakremu vitu. Be wise visualize, Systems duniani ziko tofauti sasa naona unataka kuona kwamba wamekosea au hawajui IoI kumbe wewe bado....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...