
Mheshimiwa sana Mkuu wa Wilaya!
Natambulisha kwako kijarida chenye lengo la kuchochea mwamko wa kifikra katika jamii yetu. Kijarida hicho kinaitwa "Cheche za Fikra".
Kitakuwa kinatoka kila Jumanne na kusambazwa sehemu mbalimbali nchini bure kabisa na watu wanaojitolea.
Kwa yeyote anayetaka kujitolea kukisambaza awasiliane na mhariri(at)klhnews.com na atupatie email na namba yake ya simu kwa mawasiliano.
Natumaini katika kuchapisha kijarida hiki ambacho kitakuwa na mambo mbalimbali ya siasa, jamii, maisha na maoni tutakuwa tunachangia kwa kiasi kiduchu katika kupanua wigo wa uhuru wa mawazo nchini mwetu.
Cheche zimeanza, moto utawaka! Moto wa mabadiliko ya fikra!!!
Pole na matatizo ya bulogu yetu tunatumaini itarudi hewani mapema katika tovuti yake;
tumekimiss kwa kweli!!
M. M. Mwanakijiji
M. M. Mwanakijiji
Unaweza kuchusha na kuchapa Cheche kwa kwenda katika link hii:
klhnews.com/index.php/downloads/
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...