JK akilakiwa na bosi wa kitengo cha elimu cha shirika la misaada ya kimataifa la marekani USAID Dr.Sarah Moten alipotembelea jana. katika mkutano wao Dr Moten alitangaza msaada mpya kusaidia ununuzi wa vitabu vya sayansi kwa shule za sekondari nchini wenye thamani ya dola milioni 1.5 za kimarekani
JK akihutubia katika makao makuu ya shirika la misaada la marekani USAID huko washington
waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa mh. bernard membe na mkurugenzi wa wakala wa biashara na ushirikiano wa kimataifa wa marekani (USTDA) mama leocadia zak wakimwaga wino wa mkataba wa makubaliano ambapo wakala huo utaipatia bongo dola 600,000 za kimarekani kuipiga tafu sekta za umeme, mafuta na gesi huko washington, kwa mujibu wa mdau freddy maro aliyeleta picha na habari hizi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Habari za leo wadau?!
    Jamani mimi ninakwazwa na huu uvaaji wa huyo festi leidi kwani hana nguo nyingine kama suti zaidi ya vivo vitenge?sasa imekuwa too much kila mahala?!hata pasipohitajika?!simaanishi asivae ila nafikiri kuna umuhimu apunguze ili kuendana na mahali,manake kila siku vilemba nadhani hapo mtakuwa mmepata aidia ya ninachokizungumzia.

    ReplyDelete
  2. WHY TANZANIAN ARE ALWAYS ASKING FOR HELP????
    LAKINI KWANINI WATANZANIA TUNAOMBA MSAADA SANA?????

    MADINI TUNAYO, CHAKULA TUNAWEZA KULIMA, ELIMU TUNAYO..
    TUACHE KUOMBA NA TUANZE KUFANYA KAZI KWA BIDII.
    KUOMBA OMBA TUNA KUWA MASKINI..

    TANZANIA ni third world.. masikini.. lakini watu wanafanya kazi masaa nane tu.. alafu wanakaa chini.. angalia wahindi au wachina..

    Tuachane na kuomba omba ni aibu

    ReplyDelete
  3. Viva mama KJ: jasiri haachi asili
    kula kitu roho napenda, be your self mama wa kwanza, vazi limetulia na linaendana na umbo na asili yako.waache waseme kitenge ni mavazi ya kikwetu na kilemba suna mamitu, achana na suti au pedopusha zao si utamaduni wako, mamaaa viva hapo umeonekana haraka wewe tuu, tunakupenda mama.

    ReplyDelete
  4. Go President! Go President! Go all the way, Go the American way! Help to keep Tanzania secure,safe and prosper.
    It is now a show and tell time for the President. What a great picture Dr.Sarah Moten! Mmm.... a symbol from Swahili President and hooray for the Swahili women. Now should we all be impress? Maybe the President will learn something from the American women. Sorry, no cosmetic changes for swahili women they never work. It is not only how many women you appoint in your government Mr. President. It is the culture, the patriarchal system. How amazing that both the former President Mkapa and Judge Warioba say that patriatchal system brings poverty to women. But who cares the President does not require swahili women's vote, they live mostly in urban areas. It is the women from the rural areas that put the President in power who are enjoying all the benefits. Nani ata wasikiliza si wa Tanzania tu? Na wewe maskini je? Ngoja uwabiwe! Any changes in Tanzania will also be contributed by Tanzania-Americans and Tanzanians around the world. Lets learn from the Asians.

    ReplyDelete
  5. Ninaungana na anony wa 29, 2008 10:27 AM hapo juu. Kwa hakika niliposoma hii habari nimesikitika na kucheka kicheko cha masikitiko. Kweli Tanzania ya karne ya 21 inakwenda Marekani kuomba au kupewa msaada wa vitabu vya sekondari vyenye thamani ya dola milioni 1.5 na hilo linakuwa tukio kubwa la rais wetu kupigwa picha na kutangazia dunia nzima wakati huku nyumbani wezi wa mabilioni ya PESA ZA UMMA wanapewa msamaha!!!! Ninachotaka kusema ni kwamba Watanzania inabidi tufike mahali tuseme kwamba huu utamaduni wa kuwa OMBAOMBA tuuzike kwa sababu tuna uwezo wa kujitegemea KAMA NIA INGEKUWEPO. Na nia ikiwepo basi serikali itawezesha uzalishaji wenye tija na wakati huo huo kuwabana MAFISADI.

    ReplyDelete
  6. Utamaduni wakuomba sio tatizo kama ninavyoliona tatizo la wasomi ambao badala ya kurudi kusaidia uchumi wa kwao na kubuni mambo kwa kadri ya elimu zao, wao wanabaki kuosha barabara na kubeba box kwamiaka. Inasikitisha kwani usomi wao ndio ungekuwa chachu ya maendeleo home but utakuta engineer anabaki kuwa postman na cleaner or security . Sometimes najiuliza kama kweli walikuwa wanajuwa maana ya kusoma kwao. WHY mtu ugraduate as business admin or enterpreneur useme nyumbani hakuna ajira??? so hiyo degree yako kwanini isikusaidie kuanzisha ajira?? unabaki unaomba kama JK.

    Let us use our skills for the future of our people then hatutaomba.

    G7
    UK

    ReplyDelete
  7. Hivi mlisomeshwa bure na Nyerere ili mje kuiuza nchi na kutuletea wazungu wa kuindesha nchi? Hakika inauma sana. Tunaelekea kubaya zaidi ya Mkapa ambaye alikiuka usia wa Nyerere akabinafsisha kila alichotaka kubinafsisha na akafanya biashara Ikulu akiipinga kauli iliyomfanya aende Ikulu kwamba yeye ni Clean hatofanya biashara Ikulu. Nyiyi mnataka uraia wa nchi mbili ili iweje sasa? Rejeeni katika misingi ya utaifa na mtathamini uraia wenu na utanzania wenu. Hizi fikra mlizonazo zitatumaliza.

    ReplyDelete
  8. Mimi nakubali na hayo maoni kabisa
    Watu wanasoma ulaya alafu wanaajiriwa kuosha vyombo au kuwa security.
    Mimi nasema kabisa kama watu wanaosoma huko wangekuja nyumbani na kusaidia uchumi..
    LAZIMA TUWE NA WATU KAMA KONYAGI .
    KAMA KILA MTU AKIPELEKA BIDHAA ZA NYUMBANI ULAYA ... UCHUMI WETU UNGEKUWA MBALI NA KAZI VIWANDANDI ZINGEJAA..

    Mimi nilivyoona Konyagi ipo marekani sikuamini..
    Sasa hata mimi nataka kwenda huko usa...
    TUACHE KUOMBA..

    OMBA OMBA UFA MASIKINI!!!!!

    ReplyDelete
  9. "BURE GHARAMA"
    Ni Hilo tu

    ReplyDelete
  10. Mtukufu Rais,kwenda kuomba msaada wa vifaa vya elimu kwangu si kosa,
    Mbona Mandela(Madiba} kila Mwaka anachangisha wazungu eti B.day nyinyi hamwoni??Wewe unaye chonga! mnaziona hizi ni changi umeweka ngapi?ktk Mfuko wa Nyerere Foundation???Ninacho amini Mtukufu Rais ni Mtu wa Mifano: atakusanya hilo fungu na litawafikia wanao husika.siyo kama viongozi wengine mafisadi wangelipa hilo fungu wangejifungulia akaunti zao U.S.A kimya kimya au ingeletwa bongo nusu.Kama wabongo tutashindwa kumwelewa Mtukufu Rais J.k Basi umerogwa!!!

    ReplyDelete
  11. Tatizo la baadhi yetu wabongo ni kufikiri kuwa kujenga taifa lako au kuonekana unachangia katika ujenzi wake ni sote kubanana hapa hapa bongo. Kumbukeni nchi zilioendelea na zinaoendelea watu wake huwa wako tayari kuacha mazalio yao na kwenda kufanya kazi yo yote mahali po pote na kuleta mavuno yao nyumbani. Kama mtu hawezi kutofautisha kati ya kufanya kazi nchi ya nje na kwenda kuomba msaada nje ya nchi basi huyo hakuna jinsi anavyoweza kusaidiwa. Kawaulize wataalamu wa uchumi ni mchango gani (sio rasmi)wa kifedha katika uchumi wa nchi unaotokana na watanzania ambao wanaishi na kufanya kazi nchi za nje. Wabongo tubadilike jamani, tuachane na fikira mgando!!!!

    ReplyDelete
  12. Ungeelewa problem sio kubaki na kufanya kazi nje. Problem nipale graduate unapoacha profession yako nakubaki ukifanya kazi ambazo zinadhalilisha kizazi chako na wewe mwenyewe compared na kama ungejitutumua na kujiimarisha kwenye kutumia elimu uliyopata. Mfano umegraduate ni IT specialist then unabaki kuosha vyombo.. wazungu wanakucheka sema hawakuambii. wanakushangaa why ulisomea hicho kitu.. ndio hapo inafikia hatua unakaa years bado unaishia kuomba benefits.. mtu umekaa several years ukipatwa na tatizo dogo unaomba uchangiwe.. mtu amekaa several years hana servings at all. zote nikwamba tunabweteka na vibarua pipi wakati dunia inaenda. then tunatukana home tuuuu kila siku stress mtu hachangamkii..

    G7
    UK

    ReplyDelete
  13. G7, hoja nzuri. Watu tukishasoma turudi tukajenge taifa. Swali langu kwako ni hili, wewe wafanya nini UK? bado ni Mwanafunzi? kama ndivyo, Je utarudi mara tu ukimaliza? au utakaa kidogo kama miaka kumi hivi kujitayarisha?

    Mdau
    postgraduate - UCL - London

    ReplyDelete
  14. Well good question, I always answer direct question with true answer.
    Sijasema watu warudi home if they have reasons to stay! well mimi nitarudi soon and kifupi by december 27th I will be in dar through british airways.
    But nieleweke nikwakuwa I have a reason to be home, my brother will remain here because he has a reason to be here too. but natumai in two years naye atarudi home because together we have the project to implement at home.

    So Londonor usihofu just plan ur future and learn not to forget that u strived for ur degree make use of it.

    G7
    Uk

    ReplyDelete
  15. Thank you G7

    Mdau
    Postgraduate - UCL - London

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...