Mwimbaji wa bongo flava Ali Kiba ambae alitua Marekani wiki iliyopita kwa kishindo kwa maonyesho mbali mbali hapa Marekani,atafanya onyesho lake la kwanza kwenye bashi la ubwete la Watanzania Washington Dc jumapili august 31 kwenye ukumbi wa
Mirage,
4401 university blvd,
Hyattsville Md 20783.

Onyesho litaanza saa 4 usiku.

Ali Kiba ameahidi kufanya mambo makubwa,wapenzi wa Washington Dc na vitongoji nyake kaeni chonjo,usingoje kuhadithiwa,njoo kwenye onyesho la kwanza na uwe wa kwanza kucheze CINDERELLA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Nadhani watu wa DC wanatakiwa kuwa makini wanapotuma hizi posti. Watasemaje onesho la kwanza wakati wameshasema alitua Marekani na kufanya maonesho kadhaa?
    Anyway. Enjoy Cinderella

    ReplyDelete
  2. Dogo ulianza na unaendelea vizuri sana - ANGALIZO 'Usibweteke,usidharau na unachokifanya ni kazi(ofisi yako)usije geuka ukawa kama kina nanihi waliojisahau na unafahamu wako wapi hivi sasa'

    ReplyDelete
  3. ebana hiyo address mbona haipatikani mapquest? Ndiyo sina GPS.I have to cover all the bases.Najuwa wabongo tulivyo.

    ReplyDelete
  4. Ndugu Michuzi hawa watu wanatoa habari wapi?Hili ni onyesho la kwanza.Kitu kimoja ambacho wadau tuache ni kuongea maneno ambayo hatuyajuwi,hivi huyu bwana akiulizwa wapi alifanya hilo onesho atasema?.Acheni kualibu mambo mazuri.Watanzania tusapotiane,wapuuzi na wadau kama hawa ndiyo wanarudisha maendekeo nyuma.

    ReplyDelete
  5. hakuna mambo mengine ya kufanya wabongo,ni starehe tu ,leo kaja ALI KIBA kesho MR NICE,hatuta endelea milele tutaishia hivyo tu na starehe zetu,asante kaka MICHUZI

    ReplyDelete
  6. Wewe unayesema hatuna mengine ulegee...wewe huoni bongo wanvyoserebuka halafu huku watu wakitaka kupumua kidog basi imekua taabu

    Hebu nagalia picha ya chini ya hii tu itakusuta...Waziri mkuu wanaserebuka baada ya bunge....

    waachie wenzako waserebuke baada ya summer unajua watu walikua wanapiga job masaa mangapi ili wapate tuition fees?

    Waachie watu wajimwage soon tutakua winter hasara tupu


    Huko DC enjoy to the fullest angalieni tu hao wachawi wapiga picha wasije wakapiga picha na kuwaweka kwenye site zao wanazozijua wenyewe

    ReplyDelete
  7. Basi dogo akirejea Bongo hata kutembea mwendo atabadili, kisa STAA, kafika hadi kwa Bush.

    Maana mastaa wa Bongo wanapenda kusotwa vidole.

    ReplyDelete
  8. Mmh lakini hii JEANS aliyo vaa mbona ina utata...what the heck is that??? Please watu wa DC muwe na good sound system...sio yale "mavi" ya OHIO tena!!

    ReplyDelete
  9. Tunaomba tupewe taarifa akitoka DC anaelekea wapi tunamsubiri maeneo mengine ya US, tupo dogo kukuunga mkono na kupata tunayoyamiss, tuko mbali na nyumbani,masaa tutapiga na starehe tunapata, sie Wabongo na tunajua tunafanya nini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...