Pichani ni Kondakta wa Basi linalofanya safari zake jijini Dar es Salaam akiongoza magari baada ya foleni kubwa ya kwenye makutano ya barabara ya Lumumba na Uhuru.


Kujitolea kwa kondakta huyo kati ya Makondakta wote waliokuwapo hapo, ni moja ya kazi ya kila raia wa nchi kujitolea wakati jambo au mambo yoyote yanayojitokeza aidha kwa bahati mbaya, bila ya makusudio au kwa makusudio.


Kujitolea kusawazisha ya wenzako au kusawazisha kwenye kila jambo linaloelekea pabaya ni haki ya kila raia kumshauri raia mwenzako ili ndugu au jamii au kijiji au nchi isielekee pabaya.


Kwa nchi kama Uingereza wanaita "Duty of Care".


Je, huyu ni wewe?Kwa yeyote anayemjua kijana huyo (pichani) atume namba yake ya simu,



tuna zawadi ndogo tu ya kumpa ndugu yetu huyo mwenye mfano mzuri, ahsante.Na aliyepiga picha hii wa gazeti la This Day, tunampa ahsante.
Na Kaka Issa Michuzi (Happy Birthday on the 28th August 2008).
Zenjydar Community Association inawatakia Watanzania wote duniani, RAMADHAN KAREEM.
Mhariri,
Zenjydar Community Association

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hilo ni kosa la jinai kisheria.
    Anapaswa kushtakiwa kwa kujifanya Polisi.Kwa watani zetu huyo asingechukua hata dakika 5 kuswekwa lupango.Ni budi tukatafuta njia zingine za kuondoa tatizo sugu la foleni kuliko kondakta kujifanya askari.JE AJALI IKITOKEA WAKATI YEYE ANAYAONGOZA MAGARI ITAKUAJE?
    Wanasheria naomba mawazo yenu

    ReplyDelete
  2. Kama nakumbuka vizuri sheria niliyofundishwa nikiwa mwaka wa kwanza Chuo cha Nanihii... pale karibu na Makumbusho. Miaka kibao iliyopita.

    Duty of Care hutumika popote siyo tu Uingereza. Maana yake ni kwamba, Kwa kutumia busara za kawaida... Huwezi kuona jambo likiharibika au sheria ikivunjwa kwa makusudi kabisa na ukaliangalia tu.

    Mfano miezi michache ya karibuni... niliona/ nilisoma ... habari za mtu ambaye alikwenda nadhani White House...au ikulu ya nchi fulani... sikumbuki vizuri.. na kuanza kufyatua risasi akizielekeza ndani ya maeneo ya sehemu hiyo. Akatokea mpita njia ambaye alikuwa anasukuma gari la kubebea mtoto, akiwa na mtoto wake...

    Alipoona tukio hilo, akaacha mtoto wake pembeni na Kumrukia huyu jamaa mwenye bunduki, kumtupa chini na kumdhibiti mpaka askari walipofika. Huyu jamaa hakuwa polisi na wala hiyo siyo sehemu ya kazi yake... ni Duty of care/ or Duty to the Public.

    Huwezi kuona kwa mfano mtu akikusudia kuua, kusababisha janga, hasara, kuchota fungu la EPA, hata ku-commit suicide ukaacha tu kuwa haikuhusu.

    Fanya uwezalo kama ni kuiarifu mamlaka husika, au kama ni kuingia mwenyewe kama huyo konda ... n.k.

    Mdau - Ughaibuni.

    ReplyDelete
  3. Angegongwa hapo sijui nani angelaumiwa.

    Yellow vest iko wapi ...wengine hata wasingemuona huyu

    Insurance zenyewe ndio hizo za bongo

    Si mshauri mwingine kufanya hili....

    ReplyDelete
  4. Ndugu yangu wewe unayetaka avae "vest" wewe umemuonaje kuwa hajaa vest. Kwa hiyo ina maana unamuona hata bila hiyo vest.

    Ni vizuri tujenge tabia ya kulinda haki, sheria, kusaidia inapobidi.

    Mfano wewe ukimuona mwanafunzi anasukumwa au anazuiwa kupanda basi
    anapoenda au kurudi shuleni, wewe utanyamaza tu kwa vile hujavaa magwanda ya ki-polisi. Ukiona mtu anamwagia petrol nyumba au jengo, utanyamaza tu kwa vile hujavaa ki-polisi. Ukiona mtu anatega bomu, ukiona mtu anaiba mafuta ya transforma,utanyamaza tu kwa vile haikuhusu na hujavaa magwanda ........ yapo mengi.

    Huyo konda hapo alipo ukimgonga na gari utakuwa umekusudia, kwa kuwa anaonekana.

    ReplyDelete
  5. Kwa yote yaliyosemwa hapa, naona huyu mdau ni shujaa, kwa maana yeye ndio atakuwa ni chanzo sasa cha watu kukaa chini na kutatua tatizo hilo sugu. Kweli huyu kijana ni shujaa na kachangia kwenye nchi yake, kweli hiyo hiyo ndio duty of care. Kondaz oyeeee!!! Wachochezi na Wapiga domo ZIIIIIII!!!

    ReplyDelete
  6. HILI ENEO LA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA LUMUMBA NI SUGU SANA KWA MAGARI KUFUNGANA NA KUSHINDWA KUPITA LAKINI JAMBO LA AJABU SANA HATUA CHACHE SANA KUTOKA HILO ENEO YAANI MAENEO YA LILIPOKUWA DUKA LA SUKITA BARABARA YA KIUNGANI KUNAKUWAGA NA RUNDO LA ASKARI WA KAWAIDA NA TRAFIC WANAKAA PALE KUVIZIA MAFUSO YANAYO PAKIA MIZIGO KUELEKEA MIKOANI WAYATOLEE UZUSHI NA KUYAKAMUA PESA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...