waziri mkuu mh. mizengo pinda na mai waifu wake mama tunu pinda wakiongoza mduara katika hafla ya kumalizika kikao cha bunge usiku huu hapa dodoma. nyuma ya mama tunu pinda ni mh. spika samwel sitta akifuatiwa na naibu wake mama anna makinda na waziri wa nchi ofisi ya rais mh. philip marmo. bunge linaahirishwa rasmi leo baada ya kudumu kwa takriba miezi mitatu ya bajeti na mijadala mizito
dj too short wa clouds 88.4fm alikuwemo ndani ya nyumba na malavi davi yake
mama tunu pinda na mh. martha mlatta wakicheza twisti
mh. spika samwel sitta akiongozana na mh. al-shaymaa kwegir kwenda kuchukua zawadi yao kwa kuibuka washindi wa kucheza bongo fleva katika hafla hiyo
wah. wabunge wakiserebuka
mkuu wa wilaya ya tegeta ambaye amesherehekea besdei yake ya kuzaliwa hakujivunga kwani aliunganisha sherehe yake na hafla hiyo na akisaidiwa na wadau athumani hamisi, juma dihule na selemani mpochi
mkuu wa wilaya ya nanihii akiwa na kikosi kizima cha wana njenje ambao walikubali kuja dodoma kusherehekea besdei yake ya kuzaliwa
wah. na wafanyakazi wa bungeni wakiyarudi mambo
babu njenje (shoto) na keppy kiombile wakiwa na mc wa shughuli hiyo sakina wa lyoka toka clouds 88.4fm
"walumba mpoooo...." anaimba nyota waziri wakati njenje walipoduarisha wah. wabunge usiku huu
--------------------------------------
Happy birthday to you*2
Happy birthday dear Issaaaaaaaaaaa
happy birthday to you!
How old are you now*2
Happy birthday dear Michuziiiiiiiiiiiiiiiii
happy birthday to you!
Sasa mkuu wa wilaya ya nanihiiiiiii ndio nn cku ya besdei kuvaa suti na t-shirt?? Mi naona hiyo haijakaa vizuri.Au ndio umetufanyia sapraizi?????????????????????????????
Mdau Naomi
----------------------------------------------
asante mdau naomi na wengine wote mlionitakia besdei njema. shati lilikuwa halijakauka ikabidi nipige ze fulanzzzzz. si unajua tena?
-michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Bwana michuzi vipi katika mipango ya haki za wanamuziki, hizo cd vipi mpango wake au kwa sababu bungeni wazee wa taswira hawawezi kuvamia.

    ReplyDelete
  2. Hey....Hey...Hey...Just wait a minute......Nilimsikia vizuri kabisa muheshimiwa spika wakati anawakaribisha hawa ndugu kwenye huu mnusa aliwaambia dress code iwe....CASUAL-SMART.....yaani tuseme hawakumuelewa au ndo mambo ya kikulima mpaka bungeni?.....Khaa!....sasa wewe unayejichora hapo na suti nyeupe....tukisema ...mnasema ni majungu....BADILIKENI BWANA!!!!

    ReplyDelete
  3. Duhh kweli ubunge raha,
    hawa jamaa itakuwaje sasa bale msasani jumamosi hii kama wako domu au ndio kkusema siku hizi pale hawapigi tena au??

    ReplyDelete
  4. faza

    hepi besdei....ngoma miaka mingapi mbona hutaji

    ReplyDelete
  5. Wabongo kweli nomaaaa, hebu chekini hizo cd za 2 short yani zote za kucopy hakuna original hata moja..! Jamani tujifunze kununua original maana akina 2 short ndio wanadidimiza mziki wa kibongo...!

    ReplyDelete
  6. mh! huu ukumbi wa wapi? unaonekana mkubwa ila sakafu...

    ReplyDelete
  7. Anony wa 5:48 PM suala la ku-pirate sio wabongo tu. Mi niko nje and some of my friends (not Tanzanians) are DJ-ing in clubs here na kwa kudownload na kuburn ndio wenye. Pia saa nyingine unakuta DJ katengeneza mix tayari so that he doesn't have to change songs every 5 minutes when playing, hivyo inabidi aziburn ktk CD

    ReplyDelete
  8. mtafitikolo umenena. mie mwenyewe binafsi nikinunua CD original nai-copy halafu natumia copy ili ile original isichakae. inasaidia ku-keep collection live, otherwise utajikuta unanunua hiyo hiyo CD zaidi ya mara mbili. otherwise tusingekuwa na zilipendwa, old school etc

    ReplyDelete
  9. ha na we michuzi na huo m-tisheti wako unatuboa sasa kah. yaani hadi ndani ya suti!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...