

Moja kati ya watu waliothibitisha ushiriki wake katika LABOR DAY BASH litakalofanyika mwisho wa juma la mwisho wa mwezi huu (Aug 29-31) ni DJ Joe ambaye ameahidi kufanya "makamuzi" ya haja kwa wale watakaohudhuria.
Katika kutaka kumfahamu kwa undani, tulimsaka na kuweza kujua ni nani, ametoka wapi, anafanya nini na anaamini anaelekea wapi.
DJ JOE aka The CATDADDY ( www.djjoe202.com) ni mmoja kati ya wa-Tanzania wanaoweza kujivunia juhudi zao kuelekea katika mafanikio ya kazi zao za kila siku huko Washington DC .
Akiwa mmoja kati ya ma-Dj wanaofanya vema katika kituo kinachoongoza kwa kuwa na wasikilizaji wengi katika eneo hilo cha WKYS 93.9 Kiss FM (www.939wkys.com) , Dj Joe ambaye jina lake halisi ni Joseph anaeleza mchakariko wa kutafuta mustakabali wa maisha yake kama Dj, kazi na fani aliyoipenda tangu utotoni.
Joe amesema amekuwa akipenda saana shughuli za kuchanganya muziki tangu akiwa kijana mdogo (takriban miaka 14) , lakini kama ilivyo kwa wazazi wengi wa jamii yetu nyumbani Tanzania , waliona hiyo kama kazi ambayo ingemuwezesha kuendesha maisha yake kwa mafanikio hivyo kutopata ushirikishi mwingi toka kwao.
Lakini baadae ilipoonekana kuwa ana uwezo wa kufanya hivyo, mama yake alianza kumsaidia kumnunulia vifaa na miziki iliyomsaidia kuendeleza kipaji chake kwa sharti la kufanya vema kwenye masomo yake.
Akiwa sekondari, Dj Joe aliendeleza makamuzi kila alipopata nafasi huku akipata msaada wa kiujuzi toka kwa wakongwe kama Dj SUDI ( R.I.P) wa Club ya Shilam Dodoma, Super Deo wa YMCA na VISION pamoja na Dj John na Young Millionare wote wa YMCA na VISION zote za Dar.
Baada ya kumaliza elimu ya sekondari, Joe alipata nafasi ya kuelekea nchini Marekani mwaka 1993 na kufikia maeneo ya Washington DC ambako pamoja na kazi nyingine za kusaka maisha, pia aliamua kuendeleza kipaji chake cha u-Dj akijikita zaidi katika miziki ya kiafrika ambayo hata hivyo anasema kuwa haikupokelewa vema na jamii ya wa-Tanzania kama alivyotegemea hivyo kukumbana na kigingi kingine katika njia yake kuelekea kwenye mafanikio.
Kutokana na mapokezi finyu ya mahadhi aliyokua akitaka kujishughulisha nayo katika kazi yake, Joe aliamua kubadili mtazamo wa kazi na kuingia katika kuchanganya miziki ambayo ina washabiki wengi hapa nchini ( Hip Hop, R&B na Reggae) ambapo kwake hiyo ilikuwa hatua mpya iliyofungua pazia kuelekea mafanikio.
Kutokana na kipaji, utundu na ubunifu alionao katika kazi yake, Dj Joe aliweza kukubalika na kuanza kuona uwezekano wa kugeukia kazi ya u-Dj kama njia kuu ya kumuingizia kipato na kumuendeshea maisha yake na familia yake.
Baada ya kujenga uaminifa ndani yake na kazi yake, Joe aliamua kujiingiza kwenye mashindano ya kumsaka mkali wa ku-Dj kati ya mwaka 1997 na 1999 ambapo aliweza kujinyakulia vikombe kadhaa, hatua ambayo ilimpa uzoefu na ujuzi zaidi wa kazi na kumpa nafasi ya kwenda kufanya Showcase iliyomkubalisha ndani ya 93.9 FM WKYS.
Kituo kinachomilikiwa na TV na Radio one ambao pia wanamiliki vituo vingine 37 katika majimbo 37 nchini Marekani na baadhi ya vipindi ambavyo Dj Joe hushiriki huunganishwa na vituo vyote hivyo kufanya kazi yake isikike majimbo 37 nchini Marekani.
Mwaka 2000 Dj Joe aliamua kufanya kazi na u-DJ kama kazi kamili ya kumuendeshea maisha yake ambapo mbali na kupiga katika radio, pia amefanya kazi ama amepiga katika klabu kubwa na zivumazo maeneo ya Washington DC za Love (zamani Dream), Platinum na H2O na pia kumbi za DC Live na VIP (ambazo zimefungwa) ambazo pia hushirikisha wasanii mbalimbali maarufu wajao kufanya maonesho yao.
Kwa kufanya kazi katika kituo kikubwa cha Radio na kumbi kubwa, Dj Joe ameweza kuwapigia wasanii maarufu na pia kukutana na kufanya mahojiano na wasanii wengi nyota kama Mary J Blige, Jay Z, Beyonce, G-Unit (aliofanya nao mahojiano mara baada ya kurejea nchini Marekani kutoka Tanzania ambao waliisifia saana nchi yetu), L.L Cool J, Fat Joe na wengine wengi.
DJ Joe anatoa shukrani kwa wengi waliomsaidia kwa namna moja ama nyingine kufika hapa alipo na pia wale wanaoendelea kumuunga mkono ktk shughuli zake za kimuziki. Pia anamshukuru saaana Uncle Steve Mgaza ambaye alikuwa chachu yake kubwa katika kazi za redioni.
Kuhusu makwazo na magumu kuelekea tutakako, Joe anasema kuna ugumu mkubwa katika mafanikio lakini lazima watu watambue kuwa vikwazo tukutanavyo katika kazi zetu ni changamoto (challenge) kuelekea mafanikio yetu hivyo hakuna haja ya kukatishwa tamaa na kuyumbishwa na makwazo ya aina mbalimbali ambayo tunapambana nayo kwenye pilika zetu za kila siku.
Anakubali kuwa ana mafanikio kulingana na usawa aliokuwa wakati akianza kujishughulisha na kazi hii, lakini pia anasema ana mwendo mrefu kuelekea mafanikio halisi ambayo amekuwa akiyafanyia kazi na kuyapanga kwa muda mrefu.
Unaweza kutembelea tovuti yake Dj joe ambayo ni
kuona picha na video zake zimuoneshazo Dj aki-spin “vibaya mbaya” ndani ya studio za WKYS 93.9 FM.
ReplyDeleteNASIKIA dc WANANDAA PATI YA LABORDAY....SOMENI HILI ONYO KABLA HAMJACHUKUA DAYS OFF KAZINI.....WATU WA DC WANAJIAIBISHA SANA NA MAMBO YAO YA MITANDAO YA KIPUMBAVU...KUNA WATU AMBAO WANACHUKUA PICHA ZA WATU HALAFU WANAZIPHOTOSHOP ILI MTU AONEKANE YUPO UCHI AU ANAFANYA NGONO, THEN WANAZIPOST KWENYE BLOG FULANI FULANI ZA KISHENZI...CHA AJABU WATU WA DC WALIVYUKUWA WAPUMBAVU WANAANZA KUTUKANANA MATUSI YA NGUONI..HUWEZI KUAMINI VITU VINAVYOANDIKWA KUHUSU WAZAZI WETU..NI JAMBO LA AIBU SANA HASWA UKIZINGATIA KUWA WATU NYUMBANI TANZANIA WANATEGEMEA KUWA WATU WAMEKWENDA NJE KUELIMIKA NA KUWA NA BUSARA, LAKINI MATOKEO YAKE WANAKUWA WAPUMBAVU SANA NA KUJISHIRIKISHA ZA HIZI BLOG ZA KISHENZI NA KUTUKANA WAZAZI NA NDUGU ZA WATU....HIVI MAMBO YANAYOANDIKWA HUKO UKIYASOMA UTASIKITIKA SANA, HUWEZI KUAMINI KAMA YAMEANDIKWA NA MTANZANIA....SIKU HIZI TUKIKUTANA NA WAKENYA WANATUCHEKA SANA ....AIIIBU. KWA HIYO WATU WA STATE ZINGINE NAWAOMBA SANA MSIJE DC OTHERWISE NA NYIE MTAANDIKWA KWENYE HIZO BLOG ZA AJABU JABU NA PICHA ZENU KUBADILISHWA ILI MUONEKANE MKO UCHI NA MNAFANYA NGONO....hili ni onyo la pili....WAACHENI WATU WA DC NA MAMBO YAO YA KIPUMBAVU....NAOMA WATU WENGI TIKA USWAHILINI WANAISHI DC
Wewe ulioweka comment hapo juu. unachokiandika akileti maana kama wewe hutaki kwenda huko Dc kwenye party basi. Sisi tunakuja kama kawaida tumekuwa tunakuja kwa miaka kama kumi kila mwaka na hatujawahi kuandikwa. Kama wewe siku hiyo unaenda kupadilisha wazee nepi, Basi anza tu kwa utaratibu wako. Watu wangapi wanapigwa risasi mitaani au wanakabwa... basi tungekuwa hata kazini hatuendi kwa ajili ya kuogopa kwamba tutakabwa au kupigwa risasi.
ReplyDeleteKwanza jionye wewe na tabia yako ya kichawi. Kalee wazee, wacha watu tule starehe!!!!!!!!!
KWANI MTU KUONEKANA UNAFANYA NGONO NI KITU KIPWA? WEWE TITI MWENYEWE WAZAZI WAKO WANAJUA UMEVUNJA UNGO NA UNAKAA NA HAWALA SASA HIYO SI TICKETI KWAMBA UNAFANYA MATUSI NA UKIWA UNAFANYA MATUSI LAZIMA UWE UCHI? SASA KIPI KIGENI,MIMI NAONA MTOA HOJA BI TITI ANAHASIRA TU NA HIYO PARTY HATA TUKIMWULIZA MICHUZI SI AJABU HAJAWAHI KUZIONA HIZO PICHA NA YEYE NI BINGWA WA BLOG??!! TITI INAWEZEKANA ULIPIGA KWELI PICHA ZA UCHI AMA UNAOGOPA WASHKAJI WA MBALI WASIJE NA KUKUONA UMECHUJA SANA, KUANZIA SURA HADI TABIA AMA UMECHUKULIWA BWANA NINI? HIZO PICHA ZA UCHI UMEZIONA WEWE NA NDUGU ZAKO PEKE YAKO? MBONA WENGINE TUSIZIONE? UTAJIJU WEE KAA NDANI HIYO SIKU SISI TUTAKUWEPO KUPIGWA PICHA TENA KABLA HAWAJAZIBADILI MIMI NITAKUWA WA KWANZA KUJIPIGA UCHI NIKUTUMIE NA WEWE UWATUMIE NDUGU ZAKO. KAMA HUNA CHA KUANDIKA KAA KIMYA LA SIVYO TUTAKUCHAMBA HUMU HUMU BLOGINI HAYAWANI MKUBWA?
ReplyDeleteBravooo!!! Dj joe can't wait to see you. labour day bash
ReplyDeleteOngera Dj joe kwa kupata mafanikio yako katika fani hii ya mziki. Tutakuja kukuchungulia kwa labour day weekend.
ReplyDeleteHehehehehe makubwa hayo mbona kazi.
ReplyDeleteNa nilichogundua watu wengi tu wanajifanya wanaishi DC kumbe la. Sijui watakua lini. Mtu anakwambia ninaishi DC halafu hata haoni aibu anakupa numba ya nyumbani ya simu 301. Halooo kwanini usiseme tu kama unakaa MD na labda unakazi DC? Kwani kuishi DC ndio nini?
We mpumbavu, area yote ya VA,MD and DC is called DC Metro area.
ReplyDeleteNdio maana mtu akiwa anakaa VA,MD anasema DC Nyau we!
Wewe mdau unayelalamika watu wanasema wanakaa dc kumbe md unamatatizo madogo madogo ambayo yanakunya unajali sana kitu kama hicho.imekuwa hivyo kwa mda mrefu sana watu wanarefer tu hivyo na wameichukua.watu wa dmv wote familia moja sio kwamba wanaona kutaja d.c ni bora zaidi kuliko m.d kwanza watz wanaoishi d.c sasa hivi ni wachache mno sema ndio huko shughuli zao zote wanafanya mpaka starehe.
ReplyDeleteHuyo wajuu kabisa anayesema kwamba watu wasiende d.c kisa wanatoana kwenye blog za matusi ni na swali moja tu,je umewaona wangapi wamebandikwa picha zao na je hio ndio hidadi yote ya watu wanaoishi dmv? Respect ur self plus others and people will respect u hio ndio swala muhimu unapokuwa unaishi sehemu au unaenda sehemu.
VIRGINIA(NORTHERN), MARYLAND(PG AND MONTGOMERY COUNTIES), AND PART OF WEST VIRGINIA, ARE CONSIDERED DC METRO AREA, U CAN GOOGLE IF U WANT. THATS WHY METRO BUSES AND METRO TRAINS STRECH TO VA AND MD. DC IS NOT A STATE FOR GOD SAKE, WATU MNAISHI AMERICA HATA HAMJUI.
ReplyDeletehttp://en.wikipedia.org/wiki/Washington_Metropolitan_Area
U GO BRO JOE....MAMBO YA SHILAM (KWA SHILLA) NA N.K YAMEZAA MATUNDA....THOSE DAYS ULIKUWA UNAVUNJA MIFUPA KAMA HAUNA AKILI VIZURI...KEEP UP THE GOOD WORK. LOVE U HANE! MMWAAAH!
ReplyDeleteYeah, huyo mshamba anayelalamika kuhusu DC hajui analolingea, bonge la mshamba. Joe bwana mimi nilishamuonaga H2O lakini usiku, kumbe siyo handsome sana. Lakini mtu mzuri maskini, favour aliyotufanyia na marafiki zangu siku hiyo siwezi kuisema hadharani ataning'amua halafu itakuwa noma..lol
ReplyDelete