Leo ni mara yangu kuiona website ya issamichuzi.Ni nzuri sana na sikuifahamu kabla.
Mama mmoja ambaye alipeleka kumbukumbu kwenu ya kifo cah mtoto wake SALOME amabye alikuwa leo ametimiza miaka 8 tangu afariki. Kwenye comments za watu nikaona mtanzania mmoja ambaye alituma comments zake juu ya tukio hili.
Huyu kaka yuko NETHERLANDS. Nami ninahitaji sana nipate angalau watanzania wawili ambao wapo huko NETHERLANDS ili wanisaidie kutafuta habari za kaka yangu ambaye amefungwa huko.
Kwa vile email za watu hazitokei wanapotoa comments, nimeshindwa kumuomba huyu kaka ambaye ali comment kwa kifo cha Salome leo tu ndio nimesoma nikagundua yuko Netherlands.
Tumehangaika kutuma email ubalozini mimi na ndugu wengine laki ubalozi wanasema hawaruhusiwi kutoa taarifa za mtu, due to data protection Act. Wakanishauri niutafute ubalozi wa nchi husika. Nimejaribu simu zote not in service. Na email nilizotuma mpaka leo hakuna majibu.
Huyu ndugu yangu alihukumiwa kifungo cha miezi 9, jela March,10, 2008.
Tumekuwa tunawasiliana kwa simu kwa ruhusa ya afisa magereza kila jumamosi mpaka June,07 mwaka huu ambapo alituarifu alilazwa hospital.
Kutoka hapo kila tukipiga simu haipatikani na sms zinarudishwa. Tunaomba mwenye kuweza kutusaidia afanye hivyo kwa kumtafuta kaka yetu mpenzi
Asante kaka kwa kunisaidia,
Anna
+255 713 689 665

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Pole Anna na kuwa na wasi wasi na kaka yenu. Nawaombea awe salama na muweze kufanikiwa mawasiliano saa nyingine ni kupoteana tu kwa kuwa anaweza akawa ameamishwa jela etc. ungemwomba pia michuzi aedit na atoe na email yako pia. Uwezi jua kila mtu hana uwezo wa kupiga simu kwa hiyo email inaweza saidia pia mawasiliano. Ukae katika amani na ubarikiwe. mdau DC

    ReplyDelete
  2. pOLE KWA KUMMISI BROO WAKO, ILA tUMA JINA LA GEREZA ALILOFUNGWA NA JINA LA MUHUSIKA ILI TUJARIBU, POST KWENYE BLOG HII HII

    ReplyDelete
  3. Pole sana Anna, mimi pia niko Netherlands ila niko njiani kurudi Tanzania.
    Nimetafuta watanzania wanaofanya kazi huku na Tanzania Association interim commitee ili wakusaidie, watakapokuwa na taarifa zozote watakupigia.
    Andika email kwenda kwa almondprinters@yahoo.com kwa mawasiliano zaidi.
    Tuko pamoja na Mungu atatusaidia kujua habari zaidi za kaka yetu.

    ReplyDelete
  4. huyo jamaa anaitwa nani?

    ReplyDelete
  5. Mambo vp dada Anna, pole sana kwa yaliyowakuta, ila mi naona bora uandike jina Kamini la huyo kaka yako na pia uweke email address yako kwa maana itakuwa rahisi kwa mtu mwenye info yoyote kukupa, ila ukiweka simu watu watamind kukupigia coz inagharimu sana kupiga tz, Tunaweza kukusaidia

    ReplyDelete
  6. Kaka yako anaitwa nani na kafungwa gereza gani?
    Na kabla ya kufungwa alikuwa anakaa Holand sehemu gani. labda twaweza kukusaidia tukijua hayo kwanza

    ReplyDelete
  7. Asante Issa, Blog yako kwa tuunganisha watanzania duniani.

    Pole Anna, fanya kama wengi walivyo kushauri hapo juu Mungu ataonyesha njia.

    Ushauri wangu kwa wote hasa mlioko nje. pale mlipo watumieni wazazi/ndugu namba za simu/anuani za watu (jirani:unapokaa, kazini, shuleni...etc) at least kuwe na namna ya kuwapata wengine kama wewe hupatikani ni muhimu sana.

    Mungu ibariki Tanzania, viongozi na hasa watu wake

    Grandma

    ReplyDelete
  8. Ohh masikini watanzania wamekuwa wakharimu kwenye comment yaani mpaka nimepata uchungu maana sio normal atiii.tunatakiwa tuwe na upendo kama hivi maana hata mwenyezi mungu anapenda mahala pasafi na penye upendo.mungu ibariki tanzania na watu wake

    ReplyDelete
  9. Pole Anna, wasiliana na gogimagoti@gmail.com
    Mdau AMS.

    ReplyDelete
  10. Pole Anna, wasiliana na gogimagoti@gmail.com
    Mdau AMS.

    ReplyDelete
  11. POLE SANA DADA ANGU INSHALLAH M,MUNGU ATAKUSAIDIENI MTAFANIKIWA KUWASILIANA NA KAKA ENU HIO NDIO MITIHANI YA MUNGU.MSIKATE TAMAA MTAWASILIANA KARIBUNI INSHALLA.

    ReplyDelete
  12. Ujue pale Netherlands hakuna ubalozi wa Tanzania. Ubalozi wetu ulioko Ubelgiji una cover hadi Netherlands. Hivyo jaribu kuwasiliana nao pale Brussels wanaweza pia kuwasiliana na Dutch authorities ili kuweza kumpata kaka yako tatizo hawa watu wanafatilia sana mambo ya data protection. Wanahitaji ndugu wa karibu tu kumpa information za mfungwa na sio rafiki. Hivyo iwapo ubalozi utawasiliana nao itakuwa rahisi kwa Dutch authorities ku share information na maofisa wa ubalozi.

    ReplyDelete
  13. Huyo kaka yako hana jina?

    ReplyDelete
  14. Pole sana Anna tumshukuru Mungu hii blog inafungua watu kwa machungu yao na kupata afueni na faraja.... Mungu atakusaidia at least jela za wenzetu hazina shida kama huku kwetu... be positive yupo salama tuuu..... mama Salome (Mrs B.P Makani)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...