Mkurugenzi wa Idara ya Mikutano na Masoko wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC) Bwana James Mwifunyi Natthan Mgani amefariki dunia. Bwana Mgani alifariki dunia siku ya Jumamosi tarehe 16 Agosti, 2008 katika hospitali ya AICC kutokana na ugonjwa wa Ini.

Hali ya afya yake ilianza kubadilika mara tu baada ya mkutano wa Leon Sullivan, ndipo akapelekwa India kwa matibabu zaidi. Alirudi Arusha kabla ya kufikwa na mauti.

Marehemu alizaliwa katika Kijiji cha Kasanga Wilaya Mufindi tarehe 17 Julai 1959. Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Kasanga kabla hajajiunga na Sekondari ya Forodhani ya mjini Dar es Saaam. Baadaye shule ya Sekondari ya Mirambo Tabora alikomaliza kidato cha sita mwaka 1981.

Mnamo mwaka 1987 alihitimu shahada ya kwanza kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadaye kupata shahada ya pili mwaka 1997.

Marehemu alijiunga na AICC mwaka 1990 kama Afisa wa Kitengo cha Utalii. Kabla ya kifo chake Bwana Mgani aliwahi kushika nyadhifa mbali mbali katika shirika hadi kufikia cheo cha Mkurugenzi wa Mikutano na Masoko

Ndugu Mgani alihusika katika kutoa mchango mkubwa katika sekta nzima ya Utalii wa Mikutano Tanzania na katika uhamasishaji wa kuanzishwa kwa kituo kikubwa cha mikutano (Convention Centre) hapa Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Duhhh amenikumbusha sana nyumbani arusha kama vile tulisha kumbana sana pale mbayuwayu.
    P.I.P

    ReplyDelete
  2. Kaka mzuri kweli!!! katuachaa??? salala! mungu iweke roho yake pema peponi tutakutana huko huko kama nimekukosa duniani nitakupata Ahera. Amen

    ReplyDelete
  3. INDIA INAONGOZA DUNIANI KWA KUUZA "VIUNGO VYA BINAADAMU" KILAKITU KINAPATIKANA HUKO KUANZIA "FIGO" N.K (PESA YAKO TU)

    ReplyDelete
  4. Jamani poleni sana Dada Julie, na watoto Joel & Jackie; Mary Omari, Peter Omari Jenny Mwanri na wengineo wotee... Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi...Amen!

    ReplyDelete
  5. Jamani marehem amefariki tangu 2007,tangazo linatoka leo!mlikua wapi?

    ReplyDelete
  6. du alifariki zamani 16 August 1997! ulikuwa hujaanzisha globu yako nini? almost mwaka ndo taarifa yake unatoa leo, kweli umemkumbuka!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...