Jumuiya ya Watanzania waishio Ujerumani imepatwa na msiba mzito baada ya kuondokewa na mmoja wao, Wajihi Sheikh (pichani), jana.

Habari toka huko zinasema mwili wa marehemu umeshasafirishwa leo kwa ndege kuja Tanzania kwa mazishi yatayofanyika huko Zanzibar

Marehemu Abdulrahman Hassan Sheikh maarufu kwa jina la Wajihi Sheikh, ni Mzaliwa wa Zanzibar Tanzania na alikua mmoja wa watangazaji mahiri wa Deutsche Welle(DW).
Alijunga na Redio hiyo ya kimataifa miaka ya 1970 akitokea Moscow Urusi alikokua akifanya kazi na Redio Moscow .

Alisomea taaluma ya Kemia na na baadae kuingia sekta ya habari. Miongoni mwa vipindi alivyokua akivitayarisha na kawa ustadi mkubwa akiwa na DW na kuwavutia mno wasiklilizaji ni pamoja na makala za siasa, Afya yako , na matukio ya wiki barani Afrika.

Marehemu Wajihi Sheikh atakumbukwa kwa ucheshí na huruma. Alikua mtu wa msaada kwa watu naliyependwa na wengi . Alistaafu miaka minne iliopita na amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 69.

Marehemu ameacha mjane na watoto watatu.

Mola amlaze pema peponi

Amin

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. ama kweli kazi ipo poleni sana wafiwa lakini kweli duniani wawiliwawili nilijua kikwete enzi zake.

    ReplyDelete
  2. Huyu ni rais wetu enzi zake period!

    ReplyDelete
  3. innalilahi wa innalilahi rajiun

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...