MWANDISHI wa habari wa siku nyingi,Bw.Jimmy Elias(41)amefariki dunia juzi asubuhi katika Hospitali ya Amana,Dar es Salaam,baada kuugua kwa takribani mwezi mmoja.
Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu, Richard Mwaikenda, Jimmy alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa homa ya matumbo na alikuwa akiendelea na matibabu nyumbani lakini alipozidiwa alipelekwa Hospitali ya Amana kwa matibabu zaidi.
Mwili wa marehemu unatarajia kuagwa leo mchana saa sita nyumbani kwake Kiwalani Bombom na baadaye kusafirishwa kuelekea katika kijiji alipozaliwa Ngana,wilayani Rungwe mkoani Mbeya tayari kwa mazishi yatakayofanyika Jumapili.
Hadi mauti yanamkuta alikuwa Meneja Mauzo wa gazeti la Ngurumo za Simba na jarida la StarSport tangu yalipoanzishwa.
pia katika kipindi cha uhai wake aliwahi kuandikia magazeti ya Dar Leo(zamani Majira Jioni)na Mfanyakazi.
Ameacha mke Bi.Mary Katendele na watoto watatu ambao ni Boniface,Jackson na Staford.
Katika uhai wake alikuwa mpenzi mkubwa wa mpira wa miguu ambapo alikuwa ni mwanachama hai wa Klabu ya Simba.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU JIMMY MAHALI PEMA
PEPONI.
AMEN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Burian KAka Jimmy nakukumbka ndo mlinipokea Business Timeskipindi hicho. Pole kaka Mwaikenda
    Mungu ailaze mahala ma peponi roho ya marehemu Jimmy

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...