viongozi wa simba na yanga na tbl wakitia saini mkataba wa udhamini hoteli ya moevenpick huku wakishuhudiwa na rais wa tff, leodegar tenga, mwenyekiti wa baraza la michezo kanali mstaafu iddi kipiungu, mbunge wa ilala mh. zungu. katika mkataba huo wa bilioni 3 kwa miaka mitatu umetolewa na kampuni hiyo kupitia kilaji chake cha kilimanjaro
wenyeviti hassan dalali wa simba (shoto) na imani madega wa yanga (kulia) wakipokea nyaraka za mkataba wa udhamini wa tbl kupitia kilaji cha kilimanjaro
mara tu baada ya kusaini mkataba yanga na simba walipokea kianzio cha milioni 25 papo hapo. juu bosi wa masoko wa tbl david minja akimkabidhi mwenyekiti wa yanga mfano wa hundi ya milioni 25. na chini bosi wa uhusiano na mawasiliano wa tbl maneno mbegu akimkabidhi mwenyekiti wa simba mzee hassan dalali mfano wa hundi ya milioni 25


meneja wa kilaji cha kilimanjaro mdau oscar shelukindo (pili shoto) akipozi na friends of simba
viongozi wa tbl na tff kwenye hafla hiyo
rais wa tff sir leodegar chilla tenga akiongea kushukuru tbl kwa uzalendo wao wa kuendeleza michezo. alivitaka vilabu vya simba na yanga kuwa na utamaduni wa kuheshimu mikataba ili kuwapa moyo wafadhili
bosi wa uhusiano na mawasiliano wa tbl maneno mbegu akitoa neno kwenye hafla
mwenyekiti wa baraza la michezo kanali mstaafu iddi kipingu akihutubia. pamoja na mambo mengine alivitaka vilabu vya yanga na simba kuwa mfano kwa kujenga timu za vijana ili kulea na kukuza vipaji na sio kutegemea kuchota vipaji vilivyotengenezwa na wengine kama ilivyo sasa
mfadhili mkuu wa yanga yusuf manji akifurahia jambo na rais mtaafu wa yanga francis kifukwe

wakiwa wamekula suti za bedi mbaya viongozi wa simba ndani ya nyumba. toka shoto ni mwenyekiti mzee hassan dalali, makamu wake omari gumbo na katibu mwenezi saidi rubeya
mwenyekiti wa yanga imani madega (shoto) akitaniana na katibu mwenezi wa simba saidi rubeya. hapo bila shaka ilikuwa ni kuonyana juu ya uwezekano wa kufumka bakola jangwani na msimbazi endapo pesa hizo za ufadhili zitatumika vibaya.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. TAHADHALI ZISIJE ZIKALAMBWA NA VIONGOZI TU, MUDA UMEFIKA MPIRA TANZANIA UWE PROFESSIONAL/WA KULIPWA KAMA TUNATAKA USHINDANI.

    ReplyDelete
  2. hivi bongo bwana, wale wanaojiita wadhamini wakuu mbona hatuwaoni hata kwenye picha moja? au ndio wameshapigw abuti? hawana chao katika tyimu hizi 2? hahahahahahaaa

    ReplyDelete
  3. Mimi naona wafadhili wengine inabidi wajitokeze kufadhili vilabu vinginevyo kwa saabu mpira si wa Simba na Yanga peke yake.

    ReplyDelete
  4. ....tatizo la hizi hafla zikifanyika wakati kilaji ilishapanda kichwani hubadilika na kuwa 'ghafla' na hivyo makubaliano yote yanayoafikiwa katika 'ghafla' hizo huisha 'ghalfa' mara baada ya hafla hizo pasipo utekelezaji kukamilika. naomba kwamba maamuzi haya hayatabadilika

    ReplyDelete
  5. labda niwe sikuelewa, lakini nilidhani kwa sheria za jumuia ya michezo kampuni moja hairuhusiwi ku-sponsor timu mbili (za nchi moja)zilizo katika daraja moja. naomba ufafanuzi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...