
Mshiriki wa Tanzania kwenye Shindano la Big Brother III, Latoya Lyakurwa (pichani), anatarajiwa kurejea nchini leo Jumanne baada ya kuwa mtu wa kwanza kutolewa katika jumba hilo.
Akiongea Jumatatu jioni na kipindi cha Jahazi cha Clouds 88.4FM kinachongozwa na Kepteeeeeeeein Gadna G. Habash, Latoya alisikika akisema ushindani jumbani mle ni mkali na kwamba washiriki hubadirika kama kinyonga kadri siku zinavyoenda.
Alisema ule ni mchezo na kuna kushinda ama kushindwa na kwamba haikuwa lazima historia ya mafanikio ya kina Mwisho na Richard ijirudie kwake, kwani kila kitu kinapangwa na Mungu.
Latoya alielezea nia yake ya kuwa mtangazaji katika TV endapo kama atapata shavu hilo, na kwamba yu tayari kuhamishia makazi yake Dar toka A-taun alikokuwa akiishi siku zote.
Aidh, amedaiwa kuponzwa na vitu vitatu ndani ya mchuano huo unaoendelea nchini Afrika Kusini, kwa mujibu wa http://www.bongocelebrity.com./
Globu hiyo inayotamba kwa kunadi mselebriti wa kibongo popote walipo duniani, imesema kitendo cha Latoya cha ‘kukandamiza malavidavi’ na Ricco wa Angola ni pointi ya kwanza ambayo ilimuondolea sifa ya kuendelea kubaki ndani ya mjengo.
Pointi ya pili ni pale aliponaswa na kamera akila denda na Moris wa Uganda, wakati huo huo mara kadhaa akawa anachojoa mbele ya wenzake, tabia ambayo haiendani na maadili ya Mtanzania na Muafrika kwa ujumla.
Kufuatia hali hiyo, Latoya atatakiwa kuwaomba radhi Watanzania kutokana na kuchafua ‘hali ya hewa’ ndani BBA ambayo ilisafishwa vizuri na Mwisho Mwampamba mwaka 2003 na Richard Bezuidenhout mwaka jana.
Pamoja na hivyo Jumamosi iliyopita, Latoya alionesha uzalendo wa kutosha kwa kuzifagilia baadhi ya kazi za wasanii, Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’ na Joseph Haule ‘Prof. Jizze’ ambazo zilionesha kumpagawisha kwa sana.
chumba maalum walimowekwa na Tawana wa Botswana wakati wakisubiri mmoja wao kutoka, akiweka CD zenye nyimbo za wasanii hao na kucheza kwa hisia.Mbongo huyo ambaye kwa upande mwingine alionekana kama amekumbuka nyumbani alianza kupagawa na ngoma za Mwana FA, ikiwemo inayotamba hivi sasa, ‘Bado Nipo nipo’, kisha akabadilisha na kuweka CD yenye nyimbo za Profesa Jay, kitu ambacho kilimfanya apandishe mzuka zaidi wa kucheza na kuimba, hasa aliposikia kazi kama ‘Hapo Vipi’, ‘Ndivyo sivyo’ na ‘Nang’atuka’.
Pamoja na mabaya yote aliyoyafanya mjengoni humo, http://www.bongocelebrity.com/ inampa ‘big up’ za kutosha Latoya kwa kuonesha uzalendo huo wa kuzifagilia na kuzipa promo kazi za Wabongo wenzie.
Wakati huo huo, mshiriki kutoka Kenya, Sheila anaendelea kupeta kimapenzi na Takondwa ‘TK’, kitendo kinachowafanya washiriki wengine wakae wakinong’ona juu yao.


DADA ZETU WANAHITAJI MAOMBI ILI WAWE NA MARINGO (ATITUDE{NYODO}] SIFURI. SIFA KUU YA UZURI SIO SURA. NI JINSI UNAVYOENEKANA KUJALI WENGINE, KUHESHIMU. UZURI NI UTUMWA SIO UBABE.ONGEA NA WATU KWA FURAHA NA UCHANGAMFU. KUMCHEKEA MTU SIO KIJIRAHISISHA BALI NI KUFURAHIA UUMBAJI WA MUNGU. HAPA NILIPO WAKINADADA UNAMUONA SIKU YA KWANZA UTAFIKIRI MNAJUANA TANGU MKIWA VIDUDU.
ReplyDeleteKweli Sura sio Tabia, ila twende juu chini kama ametolewa sababu mbaya na huyo mkandamizaji naye atolewe inayo kuja then watu wakae vizuri kwanza big brother ingetolewa sio sifa ya waaafrica bora mtafute kipindi cha elimu au Sanaa watu wanakaa pamoja. mtu ukiwaweka watu kwenye hali ile mnategemea nini?
ReplyDeleteLatoya hakuwahi kulikoroga kama alivyofanya Richard, huyu dada alionyesha ushindani tangu siku ya kwanza hivyo ilikuwa ni lazima apigiwe kura ya kutoka BIG alijua hilo na ndio maana alimpa nafasi ya upendeleo wa kumuweka penthouse. na hayo makosa matatu wanayodai ni kinyume na maadali ya mtanzania mimi sijui ni yapi wakati Richard alifanya zaidi ya hayo na aliiibuka mshindi. Hayo makosa ni mtizamo tu wa mtu anaejifanya mchambuzi mzuri wa maadili na asiejua hata kanani za mchezo wenyewe. kama malavidavi ni moja ya kosa basi Richard leo asingekua mshindi. na vp kina Lerato ambaye mpaka sasa kajipatia mpenzi wa kudumu? na pia watanzania tunasahau kuwa bila Tatiana kumuokoa kaka yetu leo yeye asingekuwa mshindi.Richard alipigiwa kura ya kutoka mara 4. Mfumo dume umetawala kwa watanzania wengi na kuona alichofnaya Richard ni sawa na Latoya si
ReplyDeleteo sawa.just because she is a woman!!!!!.eti kosa jingine kukiss na Morris?? mbona Lucilee alikiss na TK na hakutolewa??? huyu mchambuzi mbona hakuwahi kuandika kuhusu FINGERGATE YA RICH NA UFUNEKA??? je hayo ni maadili ya kitanzania?????.
HIO PROGRAM NZIMA SIO UTAMADUNI WA MTANZANIA WALA MUAFRIKA.HAKUNA KITU KIZURI WALICHOFANYA RICHARD NA MRISHO AMBACHO KIZURI .WOTE KUNDI MOJA .
ReplyDeletesababu za kumtoa hazina msingi wowote.kama walivyoeleza wadau walionitangulia,washindi waliopita wa hiyo BBA walikuwa wachafu kuliko story ya huyo binti.
ReplyDeleteninachoelewa ktk TV shows kama hizo,yule mwenye kuonyesha ushindani mkali ndiye atakayekuwa adui wa wengine.na mara kwa mara huwa wanatolewa mapema.kwa bahati mbaya sijawahi kuangalia hayo mashindano ya BBA hivyo siwezi sema sana.ila tu kwa habari za kina Mwisho na Richard,nadhani huyu Binti ana nafuu sana tu.labda waTZ watachonga sana sababu ni mwanamke.
aombe msamaa kwa kuchafua hali ya hewa...nyooo kwa vile yey eni mwanamke au....aliyofanya richard is nothing right wakati yeye richard alikua na mke na bado hamna mtu alisema amechafua hali ya hewa...lakini msichana basi aombe radhi....simjui huyu lakini ningekua mimi siombi radhi yeyote...mchezow enyewe hauna hata maadili ya kiafrika sasa iweje yeye ayaanzishe?
ReplyDeleteNasupport comment ya hapo juu sifikiri kama amefanya lolote baya zaidi ya kutumia strategy yake ya mchezo. Nafikiri waafrica wote wameshiriki kumvote out hata jirani zetu wakenya ili kuwapa chance wawakilishi wao waliopo bado kwenye mchezo. Kwani huyu dada (latoya) alikuwa kwenye hiyo dumpster for one week na mwenzake anatoka Botswana ambaye maadili yake uchafu wake mara kumi mabaya kwa huyu wa Tanzania na bado Africa wakampa support huyo wa Botswana na kumrudisha kwa kuwa waliona ushindani wake siyo sawa na wa latoya (was TZ). Eti wanasema amechezea emotions za Morris. Yeh right! Give it a rest... Hamna cha msamaha kitu awe mwanamke au mwanamme show hii imeanzishwa nchi za Ulaya na maadili yote yanaendana na nchi za ulaya sasa kusema maadili ya kiafrica katika hii show ni kutokuwa na hekima...
ReplyDeleteLatoya naona hakutazama BBA II aliyoshinda Richard. Angekuwa ametazama asingechemsha mapema hivi.
ReplyDeleteRichard alikuwa underground sana siku za mwanzoni. Hutakiwi kuonesha makucha yako mwanzoni la sivyo kila mtu atakuona tishio watakutoa.
Pole Latoya.