Pichani juu ni mmoja wa walezi akiwa na watoto wa Makalala. Picha ya chini wa kwanza ni Rogger mgeni kutoka bongo, wa pili ni dada Malaika mwanzilishi wa kituo cha Makalala, wa tatu ni Anko Chibby mwenyewe, wa nne Ivani mdau mkubwa wa Makalala, wa tano Rafaeli mdau mkubwa wa Makalala. Siku hiyo ilikuwa ya kuwa pamoja kwa ajili ya Makalala.
Mdau Baraka Chibiriti ambaye hivi karibuni alikuwa vekesheni bongo baada ya kuchanga karata kwa sana huko ughaibuni ambako kwa sasa ndio anakoishi, kati ya mambo aliyoyafanya ni kutembelea kituo cha watoto Yatima cha Makalala huko Iringa, ikiwa ni jitihada za kuwatunza na kuwaenzi watoto ambao wamepoteza wazazi wao kwa njia moja au nyingine.


Chibiriti hakuishia hapo tu bali amewafungulia globu mahususi ya watoto hawa nia ikiwa ni ku "Creat Awareness" kwa jamii popote ilipo kusaidia kwa hali au mali watoto hawa ambao wanahitaji faraja na kuishi kwa upendo kama watoto wengine.

mtembelee
http://www.makalala-chibiriti.blogspot.com/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Uncle Chibby, kaka mfano wako ni wa kuigwa na napenda nikupongeze mkuu... Pia napenda nimpongeze kaka Michuzi kwa kuwezesha watu kama sisi kufahamu movement yako through mtandao wake wa kutisha!!

    Jamani waTz hii ndio inaitwa mifano ya kufanya kwa vitendo ari na nia ya kuwawezesha na kwasaidia wale waliokuwa hawana bahati kama wengi wetu!

    Mola azidi kuwaongezea ninyi na wote wenye nia na pia utendaji wa anga hizi.

    Ramadan Kareem!!!

    ReplyDelete
  2. Mwanangu nimekukubali maana watu wengi wakioa wazungu hawakumbuki nyumbani kabisaaaa!!
    Tunahitaji watu kama nyinyi,mwingine angejifanya hataki tena uafrika ndo wanavyofanyaga wapumbavu wengine.
    HONGERA SANA.

    ReplyDelete
  3. mambo ndio hayo....naona motivation ni kali...huyu akitoa mablangeti na mwingine kituo.....
    kweli tutafika ....tuuuuuu....na wengine msikate tamaa pole pole ndio mwendo

    ReplyDelete
  4. Mbona sasa watu hawasemi kuhusu Chibiriti?
    watu kusema wenzao hata bila kuwajua

    ReplyDelete
  5. yan km hawa watoto wa MAHENGE,,Iringa ni hamu yangu sana nipate upenyo nisaidie pale ngaa watoto wachache
    tatizo ukikutana na awa viongozi wanasiasa kila mtu ataka ulaji kwanza kabla ujaingia kazini,,,JAMANI WANABOA WANAUDHI WAWEZA PIGA MTU
    yan hawa watoto wamekua mtaji kwa wengine
    hongera kaka

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...