vijana wa jangwani enzi hizo. hapo wa chini shoto ni jenerali juma mkambi aliyekuwa anapiga 'namba mkagha'. wadau saidieni majina ya wengine na kumubukumbu zenu basi....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Kaka Michu ni mimi Mdau mbegu nazi kama Babaangu Mzee mbegu, sasa basi hili chama hapa watani wetu walikuwa teja hata watuamshe Usingizini tulikuwa tunawapigalakini sijui huyo mtu wakuitwa Madega ametokea wapi anashindwa kazi ngoja mwenyewew nilirudi kuchukua Timu hilo, Unakumbuka enzi hizo? c c m, c c m, sasa basi nakupa majina toka shoto waliosimama, Charles Boniphace"mkwassa",next amenitoka kidogo,Hamis athumani "Kinye", Joseph Fungo, Ahmed Amasha "mwana Mathematician",Selemani o. jongo, Ishaka Hassan "Chuku,Ayoub Shabani nadhani wadau wanaweza kumfananisha na Ken Mkapa lakini wakati huo ken alikuwa nadhani yupo shule,waliochuchumaa toka shoto ni juma Mkambi"General" Athumani Juma Chama "Jogoo" Rajabu Tangale,Omary Hussein,Shabani Katwila,Charles Alberto,kama sikosei anafuataCharles mwanga, ebwana sura nyingine zimenitoka lakini anyway nimejatihidi, Ahsante sana wadau naomba mnisaidie pale niliposhindwa lakini nakumbuka hizo enzi line up ilikuwa, (1).Hamisi Kinye,(2)Rajabu tangale,(3).Ahmed Amasha (4).Selemani Jongo (5)Ishaka Hassan (6).Juma Mkambi (7).Shabani Katwila (8)Charles Boniphace(9)Rashid Hanzuruni (10) Omary Hussein (11) Ayubu Shabani "Nylon" wa mwisho kulia walio simama mtoto wa Kinondoni Muslimu Enzi hizo alikuwa akimpa sana tabu Daudi Salum "Bruce Lee" Full back wa Kulia wa Watani wetu

    ReplyDelete
  2. Waliyo chuchumaa kutoka kushoto wapili ni Athumani Juma Chama, watano ni Omary Husseni, Waliyo simama mwenye nywele ndefu ni Ahmedi Amasha.

    ReplyDelete
  3. Mdau wa kwanza umejitahidi lakini hapo kwa Tangare nadhani umekosea huyo niyanga damu Fred Felix Aluta Minziro. Wa mwisho waliochuchumaa ni Peter Tino. Watatu kutoka kulia walichuchumaa ni Alan Shomari nadhani alikuwa na undugu na Lila Shomari wa Simba. Na pia katika list nadhani umekosea kidogo. 1. Kamis Kinye 2. Fred Felix Minziro3. Ahmed Amasha 4.Ishaka hassan(Alan Shomari) 5. Athumani Juma Chama 6. Juma Mkambi7. Omar Hussein 8. Charles Bonniface Mkwassa 9.peter Tino 10. Abeid Mziba.11. Ayoub Shaban.

    ReplyDelete
  4. Namsahihisha mtoa maoni wa tatu, kwamba wa mwisho kulia waliochuchumaa ni Rashid Hanzuruni na sio Peter Tino, Tino alikuwa Pan African, alikuja chezea Yanga mwishoni mwa career yake baada ya Pan kuwa imeshuka daraja.

    ReplyDelete
  5. Mtani Mbegu kwa kukusaidia tu japokuwa mimi si Kwala naomba niwakilishe . kuanzia kushoto waliosimama 1Charles Boniface 2 Juma shaban 3 Hamisi Kinye 4 Joseph Fungo 5 Ahmed Amasha 6 Selemani jongo (miguu bata) 7 Isiaka Hassan 8 Saleh Hija na chini kuanzia kushoto 1 Mkambi 2 Athuman Chama 3 Charles Kilinda 4 Omar Hussein (Keegan) 5 Pass 6 Alan shomari 7 Charles Alberto na 8 Pass . mdau mbegu enzi hizo tajiri yenu ni Viran na mnavaa jezi za bobby soap hahahahahahaha. mdau Dege Leicester UK.

    ReplyDelete
  6. Mimi nadhani katika hii timu ndio kulikuwa wakina Mohamed Bob Chopa na Muhidini Cheupe. Huyo jamaa wa mwisho kulia sio Muhidin Cheupe? Na wapili waliochuchumaa sio Chopa?? nawakilisha

    ReplyDelete
  7. wote nyie hapo juu mmekosea baada ya Omari Hussein anaefuatia ni Issa Mohamed huyu alitokea Pamba ya Shinyanga,then Allan Shomari(mmasai wa Arusha) hana undugu na Lilla Shomari(Mnyaturu-Dodoma-RIP)anaefuatia Charles Alberto-RIP alitokea KMKM ya Zanzibar lakini ni mtoto wa Gerezani-Kariakoo na mwisho ni Rashid Hanzuruni alitokea Mtwara lakini ni mtoto wa Temeke.

    ReplyDelete
  8. mdau MBEGU UMEJITAHIDI LAKINI UMEKOSEA KIDOGO LINE UP,HIYO ILIKUWA MECHI YA MWISHO MWAKA 1981 YA SUPER CUP AMBAYO ILIJUMUISHA TIMU NNE AMBAZO NI SIMBA,YANGA,COASTAL UNION YA TANGA NA PAN AFRICA,YANGA ILISHAIFUNGA SIMBA 1-O(JUMA MKAMBI)KAUNGANISHA KONA YA AMASHA BAADA YA KUONEWA SANA NA SIMBA KAMA MIAKA 4 ILIYOPITA,MECHI YA MWISHO WALICHEZA NA PAN NA ILIKUWA 0-0.LIST 1 HAMIS KINYE 2 JUMA SHABAN(UNCLE J)3AHMED AMASHA,4ALAN SHOMARI(MORINGE),ATHUMAN JUMA CHAMA(JOGOO)6JUMA MKAMBI(GENERAL)7SHABANI KATWILA,8CHARLES BONEFACE MKWASA9RASHID HANZURUNI10OMAR HUSSEIN KEEGAN,11SALEH HIJJA.NDIO YANGA WAKATWAA UBINGWA MJI UKASISIMKA AKINA MAMA WAKAINGIA MITAANI NA KANGA ZA YANGA BAADA YA MUDA MWINGI KUZIFUNGIA NDANI.ILIKUWA RAHA SANA NAKUMBUKA NILIKUWA NA MIAKA 8.

    OCD.

    ReplyDelete
  9. Kumsaidia mdau wa hapo juu ni kwamba kwa listi hiyo cheupe alikuwa bado kuchezea Yanga na Mohamed Chopa hakuchezea Yanga kabisa alichezea Simba baada kutokea arusha alichezea kidogo cosmo kabla ya kujiunga na Simba.
    mdau Dege Leicester UK.

    ReplyDelete
  10. Nawapa pongezi wote wadau, Napenda kurudia tena kuhusu huyo bwana wa mwisho kulia waliosimama naombva mnielewe huyo anaitwa Ayoub Shabani "nylon" miguu yake ilikuwa inakutana kati alikuwa winger wa kushoto wa Yanga,Muhidini cheupe was very Young that time naomba mnielewewadau, pia naunga mkono kuwa Peter Tino Au Augostino Peter alikuwa African Sports Tanga enzi hizo, na Uncle Jay Juma Shabani alikuwa kashaacha mpira alikuwa jirani yangu pale Magomeni mikumi kwa Mzee Mpupua, Mtani wa Leicester utatoka tarehe 25 October? msije mkatoka Half time kama mlivyofanya mwaka ule mkadai Hafidh Ally anapendelea, pole mtani.Mdau Mbegu, Reading

    ReplyDelete
  11. NARUDIA TENA KAKA KAMA AWALI wakati hou Nilikuwa Na umri Wa Miaka 12 Na ilikuwa Taifa Na Hii ilikuwa Ndio Mechi ilioamua Nani Atakuwa Bingwa Wa Super League 1981 Kati Ya Wanandugu Wawili Dar Young african Na pan Africa Nakumbuka Mpaka Leo Ngoma mpaka Mwisho 0-0 Yanga Wakatangazwa Mabingwa Walimfunga Simba 1-0 CDA 2-1 Sare Na Pan African 0-0 Pan Wao Walimfunga Simba 2-0 Sare Na CDA 2-2 Katika Picha nawakumbuka wote kutoka kushoto Kwenda Kulia Waliosimama Charles Boniface"Mkwasa",juma Shabban,Hamisi Kinye,Joseph Fungo,Ahmed Amasha,Suleiman Jongo,Isihaka Hassain"Chukwu" Na Saleh Hija
    Waliochutama Kushoto Kwenda Kulia ni nahodha Juma Mkambi"General"Athuman Juma "Chama"Charles Kilinda(sasa hivi kocha Wa JKT Ruvu,Omar Hussein "Keggan"Issa Mohammed "Killer"Alan Shomari, Charles Alberto(Marehemu),Na Rashid Hanzuruni Kwa Maoni yangu Kaka michuzi Nadhani kikosi kilichokuwa Bora zaidi ni Kile Cha mwaka 1983 ambacho Hakikupoteza Hata Mechi moja katika iliokuwa Ligi Daraja La kwanza Tanzania bara Ambacho Kilikuwa na kina Marehemu Yusuph Bana,makumbi Juma,Abeid Mziba,Hussein idi,Moshi Majungu Juma kampala Freed Felex Minziro Na Ali Mchumila Walipoteza Mchezo Mmoja Tu Katika Ligi Kuu Ya Muungano Dhidi Ya Bao Pekee La Rashid Khamisi Wa Small Simba Lakini Ligi Kuu Tanzania Bara 1983 Walitoka Sare Na Tumbaku Ya morogoro mechi zote 2 Simba Mechi 1 Na MajiMaji 1 Hawakufungwa Zilizobakia Walishinda Zote ikiwemo Dhidi Ya Mtani Wajadi SSC toka Brazil Na Style Ya SAMBA na Diagnal Walifungwa 3-1 licha y kuongoza kwa Bao La Mapema La Marehemu Kiwelu Mussa "Super Kiwelu"Lakini Mwisho Wa Game James Kisaka Alirudi Nyavuni Mara tatu Boniface Mkwasa(la Kusawazisha)Makumbi Juma La 2 Na Omar Hussein Akapiga La Mwisho
    Mdau Wa Soka La Bongo
    Shebbe Jeizan.
    chimoahmed@gmail.com

    ReplyDelete
  12. michuzi tunaomba picha za kaunda kabla kapeti halijamwagwaaa na wao wakajenge uwanja pale msimbazi.

    ReplyDelete
  13. Wacha wee Yanga wanaweka kapeti pale kaunda?? Haya ! haya ndio maendeleo tunayoyataka!! Tupe mapicha ili tuamini

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...