nahodha wa yanga yusuf bana akijaribu kumthibiti zamoyoni mogella 'golden boy' huku muhidin cheupe akivijari pembeni katika mojawapo ya mechi za watani hao wa jadi. mwaka huu wanacheza oktoba 26 na sidhani kama kuna mdau anayeweza kutabiri nani atashinda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Hi Michuzi.
    Hiyo picha imenikumbusha mbali sana. Ahsante kwa kumbukumbu nzuri.
    Sasa endapo timu ikasusia mechi kwa kuogopa kipigo na kusingizia mgao itakuwaje? TFF mna kazi kwelikweli. Sisi yetu macho na masikio.
    Mdau wa Soka, Dar.

    ReplyDelete
  2. michuzi bwana unapenda kuuliza swali wakati jibu unalo inakuwaje? Yanga na Simba nani atashinda? Jibu = Simba. Simba hata akiwa mbovu vipi ila ni Simba jike hata akiwa hana njaa atamla tu Yanga kitoweo awape wanae Azam. Simba atampiga yanga 3-1 huo ndio utabiri then utahesabu waliopatia utabiri.

    ReplyDelete
  3. Enzi hizo unaona Uzi wa Simba huo unangara ukiushika hauchaniki unateleza mambo ya Puma hayo hahaaha Zamoyoni mogela kipindi hiko mie mdogo nikisikia the Champs najuwa simba ndio jina lao jengine the champs kumbe kiengereza hiko cha kusema mabingwa hahaaha raha sana.

    ReplyDelete
  4. Hahahaa Yanga kumbe walikuwa na Sponsor hahaah Sponsor gani hao michuzi? Simba wana Puma ila Sponsor kiraka hahaha ila Simba ndio ilikuwa Timu ya kwanza kama mnakumbuka Kuwa na jezi yenye majina nyuma then Duwa Bin Said akaleta ushangiliaji wake wa kuiga ulaya kujilaza kwenye majani majani yetu makavu na chokoaa unachubuka raha sana kwetu tanzania.

    ReplyDelete
  5. KWANZA KABLA HATUJANUNUA TIKETI
    TUNAOMBA TUHAKIKISHIWE TIMU ZOTE ZITAFIKA UWANJANI.
    MI NISHAINGIA WOGA SIKATI TIKETI HADI NISIKIE MPIRA UMEANZA MAANA KUNA TIMU HAICHELEWI KUKIMBIA UWANJANI..

    NADHANI HADI HAPO USHAJUA MSHINDI NANI MZEE WA NANII

    ReplyDelete
  6. ISSAH UNATUKUMBUSHA MBALI SANA NAOMBA KILA KUKICHA UWE UNATOA PICHA ZA AINA HII ILITUKUMBUKE TULIPOTOKA PLEASE.USISAHAU KUWAPA POLE MAN U ,ANGALIA IMARATI TUNAVYOKANDAMIZA -Mdau TX

    ReplyDelete
  7. Duuuh wachezaji wazamani walikuwa mijitu ya miraba minne, HIVI unaweza kuwalinganisha na sijui akina Cannavaro wa bongo???au sijui Tegete???mmmh.
    Mcheck Yusuf Athman Ismail "Bana" anavyomkabili Zamoyoni Mogella "Golden BOY" na huku Muhidin Cheupe akicheck kwa umakini.Mpira zamani, sasa hivi ni madolidoli tuu.
    HABARI NDIYO HIYO

    ReplyDelete
  8. Hivi hizi timu enzi hizo walikuwa wanalipwa na haya makampuni ya vifaa vya michezo kama wadhamini au walikuwa wanajivalia tu jezi na kutangaza makampuni hayo bure, na siku hizi je ni hivyo hivyo kutangaza kwa bure au mambo yamebadilika? wachezaji wa zamani walikuwa na shape na miili ya mpira si hawa wa siku hizi.

    ReplyDelete
  9. KAKA MICHUZI HII NI 1985 NGOMA DROO 1-1 YANGA NDIO WA KWANZA KUPACHIKA BAO KATIKA DAKIKA YA 13 KUPITIA KWA SAID MRISHO"ZICO"BAADA YA OMAR HUSSEIN KUMTOKA THOBIAS NKOMA(MAREHEMU)nA kUMPATIA ZICO WA KILOSA ALIEMTUNGUA KIRAHISI OMAR SALEH"SUPER OMBOKA"ZIKIWA ZIMESALIA DAKIKA 2 KABLA YA MAPUMZIKO MUHAMMED 'BOB'CHOPA(MAREHEMU)ALIWANYANYUA VITI WAPENZI WA LUNYASI BAADA YA KUMALIZIA GONGA SAFI KATI YA JOHN DOUGLAS NA MALOTA SOMA NA KUMTUGUA JOSEPH FUNGO MPAKA MWISHO YANGA-1 SIMBA-1 SIMBA WALIONDOKA BAADA YA WIKI KWENDA CAIRO KURUDIANA NA AHLY YA HUKO NA KUCHAPWA 2-0 KATIKA KOMBE LA WASHINDI BARANI AFRICA
    ASANTE KWA HAYA
    MDAU WA SOKA LA BONGO
    SHEBBE EL JEIZAN
    chimoahmed@gmail.com

    ReplyDelete
  10. Duuuh mdau Shebe sikuwezi una kumbukumbu kali sana.safi sana mazee endeleza libeneke.
    Cha chandu - UK

    ReplyDelete
  11. Mdau Shebbe we kiboko. Ulikua unaandika hizo kumbukumbu au zipo kwa head. Ahsante sana-

    ReplyDelete
  12. Bwana Michu unauliza vikoi unguja SIMBA 2 YANGA 0 MDAU JAMES. HOLLAND

    ReplyDelete
  13. aisee izi kumbukumbu zimeandikwa ktk makumbusho yetu ya Taifa Tz??
    au ndo mdomo tu??
    uyu jamaa shebbe atusaidie awape wizara izo kumbukumbu adhimu na adimu ziandikwe,,ndo mana wazungu walitu-brainwash,,hatutunzi maandishi
    cjui kuna kidudu gani ndani ya ngozi hii,,,,,,jaza

    ReplyDelete
  14. Wadau mmeiona hiyo buti ya Mtaalamu Muhidin Cheupe?
    Hiyo upande mmoja alivaa safari buti siku hiyo, Bob Chopa aliona moto, kiatu mtu kilikuwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...