Salama Brother Michuzi?Hivi karibuni nami nilikuwa VEKESHENI huko kwa wakwezo Kampala, nikapiga picha hiyo ya "vipanya" vikiwa vimejipanga kiajabu pale maeneo ya Nakasero, nikashangaa hicho cha katikakati kabisa sijui kitatokaje hapo kikishajaa.
Nilijaribu pia kumtafuta "binti yetu" ili nimuongezee pesa za matumizi (maana alikubondea kuwa ulimpunja), lakini sikuweza kumpata
"Vipanya" vya Kampala vina fujo sana.
Mdau,
Perez
------------------------------------
asante mdau perez kwa salamu na picha. ila kwa binti yetu hawaruhusu mtu ambaye si mzazi wake kumuona. na poketi mane nimeshampelekea za ziada. asante kwa usamaria wa mashaka
-michuzi


Habari ya kazi kaka MICHU, NAOMBA MNISAIDIE WANABLOG, HIVI KWA NINI WAGANDA TUNAWATA WAKWE ZETU? NA KENYA WATANI WETU?
ReplyDeleteAhsante mdau Perez.Umenikumbusha mbali sana.Mwaka 2005 nilienda kutembelea jiji la Kampala,yaani hivyo vipanya vilikuwa kero kwangu hasa nyakati za asubuhi na jioni,vipanya vinakata njia yoyote iliyo rahisi,halafu kuna vipikipiki vya kubeba abiria vinaitwa 'visekido' navyo ni vurugu,kero tupu.Jiji lote la kampala mimi binafsi sikulipenda mpangilio wake.
ReplyDeleteBalozi Michuzi hayo uliyataka Mwenyewe.Unaona sasa watu wameshaanza kuzengea.Mtadharishe Binti yetu, maana wengine watajifanya Rafiki yake Baba
ReplyDeleteNemfurahi kweli kusikia umempelekea binti yetu pesa za matumizi kwani inaonyesha umesikiliza maoni ya sie wazazi wenzio kuhusu hao wasamaria mashaka!!! Hehheheehee! Tena umeweka wazi hawaruhusi watu wasiemjua huko, maana hata picha za wazazi ziko getini kwenye buku la wageni!(Hapa najaribu kuwakatisha tamaa 'wasamaria' wengine)
ReplyDeleteMh Balozi Baba Mamou! bora umeshtuka....huo kweli ni usamaria wa mashaka, teheteeee.
ReplyDeleteJamaa alikuwa anatafuta gia ya kukuingia tu ivyo vipanya geresha.
Tehe teh tee!
ReplyDeleteSawa Bro. Nimeshakufaham.
Tehe teh tee tee!
waganda ni wakwe kwa vile tuliwakomboa enzi zile za Idd amini dada na wakenya ni watani kwani ni kama simba na yanga...hatuwezi kukaa chungu kimoja!
ReplyDeleteWa Tz na Wa kenya...wote ni wajuaji!!
Anon wa kwanza kabisa:
ReplyDeleteWaganda ni wakwe zetu maana Bro Michuzi ameowa huko, si unajua Michu ni kaka yetu wa hiyari? (Ila mwanae ni mwanae, msijitie maanko mnaenda kutoa misaada shuleni, tumewashtukia)Teh teh
Brother Michu
ReplyDeleteIlo tu nililijua. Unajua watu wengine husitaje binti au dada yako mbele yake, kweli wanafanya kweli. Vizuri hukuwapa e-mail na mwonye hasijiingize kwenye mitandao ya marafiki wanaweza kumvie uko. Hii picha ya vipanya kweli alikuwa anatafuta gia.
Jiadhari siku nyingine kuwatambulisha familia yako. Hawa si watu
DUH KWALI JAMAA LIMEENDA MPAKA UGANDA!!!
ReplyDeleteMNAJUA KUVIZIA!!1
Ha ha haaa! Huyu jamaa ni Professional. Yaani kafikiria weeeee, akaona dawa ya kumwingia Michuzi hapa ni kumpelekea Picha, halafu unachomeka issue ya kumwona "uncle". Safi sana! Umenikumbusha enzi zangu kabla sijaoa, mambo yetu yaleeeee. Unabisha hodi nyumba wanauza kuku, unajifanya mteja kumbe unazengea Binti wa watu. Unamwambia muuza Chips ukitaka kuku nione!
ReplyDeleteKENYA watani wa jadi sijui why, ila UGANDA wakwe sababu Kaka Michuzi mkewe ni mtu wa huko-UG.
ReplyDeleteKaka uliyeletea hiyo picha ya Kampala, naomba nikukosoe, hapo sio Nakasero...Nakasero ni soko kuu la Kampala ambalo lipo kilomita 1 kutoka hapo Taxi park, eneo hilo linaitwa Owino...ni hayo tu!
ReplyDelete