Naam ndugu,nimevutiwa sana na ushairi huu,nikajikuta nami beti zinanijia ingawa ni mara ya kwanza.
1.Mchi huu mchi gani, Mzee watutatiza,
Bora uweke hewani,tupate nalo kukwaza,
Bado tupo gizani,wa lukange na vigwaza
Mchi huu mchi gani, Mzee watutatiza,
2.Kukatika na kupinda,nilipi lilo kukuta,
Kwa michuzi naye pinda,wote wajaa utata,
Wa mbagala na kitunda,bado hatujakupta,
Mchi huu mchi gani, Mzee watutatiza,
3.Hili kwetu ni ajabu,mchi wako kukatika,
Bado sijapata jibu,hali hiyo kukufika,
Lazima kuna sababu,hebu punguza wahaka
Mchi huu mchi gani, Mzee watutatiza,
4.Wezekana uliruka,ukatwanga vya wenzako,
Waka amua kuvuka,mpaka nyumbani mwako,
Ili upate umbuka ,utwangapo kinu chako,
Mchi huu mchi gani, Mzee watutatiza,
5.Au labda ni maradhi,mwilini yameingia,
Muombe mola hafidhi,akujaaliye afua,
Hapo tapata hifadhi,ya maradhi kufifia,
Mchi huu mchi gani, Mzee watutatiza,
6.Nilipofika tamati,beti zimeniishia,
Nakutakia bahati,si majuto kujutia,
Uje pona kwa wakati,utimize yako nia,
Mchi huu mchi gani, Mzee watutatiza,
-Mdau Mullah

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Habari yako kaka Michuzi,

    Kwa kuwa nimekuwa mfuatiliaji wa blog yako kwa siku nyingi, nimepata wazo la kuanzisha blog itakayokuwa ikijadili mada mbalimbali zinazohusiana na maarifa ya utambuzi.
    naomba unisaidie kuwajukisha na wengine kwa kupitia blog yako hii maarufu, kuwa kuna mtoto amezaliwa katika jamii ya wanablog hapa nchini, mtoto huyo anitwa utambuzi na kujitambua.

    Tembelea: www.kaluse.blogspot.com

    naomba kuwasilisha.

    ReplyDelete
  2. huo sio mchi ni mtwangio wewe twanga usichoke... hata TOT walishaiimba hiyo nyimbo

    ReplyDelete
  3. Mwendo mbaya uache vinuni kutangatanga
    kucha zako uzifiche ukiuona mpunga.
    wakatiza kwenye vinu nawe hujui kutwanga,
    akili yako ni changa mambo umeyavuruga,
    wala hujui kutwanga mpunga unaumwaga.

    Ulitwanga usifiwe ili uzidi kuringa ,
    kusudi unikomoe niwe katika wajinga
    unapita kwenye vinu nawe hujui kutwanga,
    akili yako ni changa mambo umeyavuruga wala hujui kutwanga mpunga umnumwaga,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...