Mh.Balozi ,
Napenda nikutumie picha hiyo kwa ajili ya kuiweka katika blog yako.
Hiyo ni picha wa wadau wa Mapambazuko Saccos Ltd,wakati wa mkutano mkuu wa mwaka,uliofanyika katika Ukumbi wa Holland -Msimbazi centre, dar.

Mapambazuko imetuwezesha sana wanachama wake kwa kutoa mikopo ya muda mrefu na mfupi.

Saccos hii ilianzishwa mwaka 2002 ina wanachama 270 ,na mpaka sasa imeweza kutoa mikopo ya kiasi cha Tsh.392,527,219=
Kauli mbiu ya Saccos hii ni : Changia Ukopeshwe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kweli hiyo Saccos kiboko-mavazi kama Jangwani, hivi wako wapi hawa jamaa.Madega anawafahamu.
    Napenda kujiunga na Saccos hii.

    ReplyDelete
  2. Mambo si mambo kwa maantiki hii nadhani nataka nijue,ilipo Saccos hiyo.Lakini shaka langu kubwa ni hiyo jezi- kwani muonekano wake ni wa Ki- Jangwani tupu,wakati mie nipo mtaa wa pili wa Msimbazi.Jezi zibadilishwe nijiunge.Au mfadhili mkuu wa ... kapita hiyo Saccos.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...