
Napenda nikutumie picha hiyo kwa ajili ya kuiweka katika blog yako.
Hiyo ni picha wa wadau wa Mapambazuko Saccos Ltd,wakati wa mkutano mkuu wa mwaka,uliofanyika katika Ukumbi wa Holland -Msimbazi centre, dar.
Mapambazuko imetuwezesha sana wanachama wake kwa kutoa mikopo ya muda mrefu na mfupi.
Saccos hii ilianzishwa mwaka 2002 ina wanachama 270 ,na mpaka sasa imeweza kutoa mikopo ya kiasi cha Tsh.392,527,219=
Kauli mbiu ya Saccos hii ni : Changia Ukopeshwe.
Kweli hiyo Saccos kiboko-mavazi kama Jangwani, hivi wako wapi hawa jamaa.Madega anawafahamu.
ReplyDeleteNapenda kujiunga na Saccos hii.
Mambo si mambo kwa maantiki hii nadhani nataka nijue,ilipo Saccos hiyo.Lakini shaka langu kubwa ni hiyo jezi- kwani muonekano wake ni wa Ki- Jangwani tupu,wakati mie nipo mtaa wa pili wa Msimbazi.Jezi zibadilishwe nijiunge.Au mfadhili mkuu wa ... kapita hiyo Saccos.
ReplyDelete