Habari za kazi kaka Michuzi mimi ni (jina kapuni) mdau. Nomba usiweke jina langu naomba uitoe habari yangu baada ya kuisoma ya mwenzangu na kuona watu wengi wamemshauri vizuri.
Habari yenyewe inaanza mwaka 1998 novemba baada ya kuhamia Arusha tukitokea DSM baada ya baba yangu aliyekuwa askari jeshi kuteuliwa kuwa katibu tarafa mkoani Arusha na kuhamishia makazi huku,katika nyumba tuliyofikia alikuwa akiishi msichana moja anaitwa (jina kapuni)kabila ni Muarusha alikuwa akiishi na mama moja aliyeamua kumsomesha msichana huyo na kumsaidia kazi ndogondogo baada ya kutoka shuleni,sasa kipindi hicho mimi nilihamia nikiwa darasa la sita na kuhamia shule hiyo aliyokuwa akisoma msichana huyo yeye akiwa darasa la nne.
Kipindi hicho hakuna kati yetu aliyemtamkia mwenzake kuwa anampenda kwa kuwa bado tulikuwa shule ya msingi,mwaka 1999 baada ya kumaliza mtihani wa darasa la saba wao walihama katika kitongoji cha Sakina na kuhamia katika Kitongoji cha Majengo kwa kuwa mama huyo aliyekuwa akimlea alikuwa akinipenda nilimsaidia kuhamisha baadhi ya vitu na kuniomba nikalale kwake alipohamia nilifanya hivyo na kipindi hicho ndicho tulianza rasmi mapenzi yetu na Agness.
Baada ya kukubaliana nakuona kila moja mwenzake anampenda tulianza mahusiano naye mwaka 1999 desemba nikiwa mimi tayari nimemaliza darasa la saba na nikajiunga na kidato cha kwanza mwaka 2000 nikiwa kidato cha pili baada ya miaka miwili kuanza shule yeye akiwa darasa la sita tulishirikiana kimapenzi na kwa kweli nilimkuta na usichana wake ikiwa ni mara ya kwanza baada ya kukaa mika miwili pamoja.
Kwa kweli mapenzi yetu yalikuwa ni mazuri huku kila moja akijitahidi kumpenda mwenzake kwa nia ya siku moja kuoana na uhusiano wetu ulikuwa ukijulikana na wazazi wake wa kumzaa ambao nao tunaishi nao hatua chache kutoka tunapoishi sisi pamoja na mama yake mlezi.
Baada ya mimi kumaliza kidato cha nne mwaka 2003 nilisoma baadhi ya kozi hapa Arusha na mwaka 2005-2007 nilikuwa DSM nikisome katika chuo cha Royor college of Tanzania nikisomea uhandishi wa habari muda wote tulikuwa tukiwasiliana na kupeana ahadi nyingi ya baadaye kuja kuishi pamoja,na kipindi chote alikuwa anakuja nyumbani na anamsaidia mama yangu kudeki,kupika na kuosha vyombo yani kila mtu alikuwa akielewa uhusiano wetu.
TATIZO LENYEWE.
Baada ya kumaliza kidato cha nne mchumba wangu huyo aliamua kusome ualimu wa awali(chekechea)kwa muda wa miaka miwili na kipindi fulani akikaribia kumaliza chuo alikuwa akidaiwa ada jumla ya sh.laki moja na mama yake mlezi alimweleza kuwa kipindi hiki yeye hana fedha kwa hiyo amfuate mama yake mzazi amlipie ada hiyo naye mama yake hakuwa nayo ikabidi amweleze mama yangu ambaye alimpatia fedha hiyo na kwenda kulipa ada hiyo na kufanikiwa kumaliza lakini hivi sasa ndio wapo kwenye mitihani ya mwisho huku akiwa amepata field katika moja ya shule mkoani Kilimanjaro.
Msichana huyu kwa kweli ndugu zangu nilikuwa nampenda sana ni ilikuwa kuanzia mwakani tuanze kuishi pamoja kwa sababu ndio alikuwa amemaliza masomo yake. Tumeishi na msichana huyoi tangu mwaka 1999 akiwa ni mwanafunzi wa darasa la nne hadi leo 2008 novemba eti ndio ananieleza niachane nae kisa ni hivi.
Msichana huyo yeye ni Muarusha na kabila hilo huwa halitaki kuoana na kabila tofauti eti mama yake amemtishia kumlaani ili aweze kuachana na mimi wakati tangu muda mrefu wazazi wake walikuwa wakipinga na yeye alisema hawasikilizi.
Baada ya kupata nafasi ya field huko Moshi alikuja nyumbani siku moja nikijaribu kuongea naye anakuwa na hasira hakutaka kuongea na mimi kabisa sas kuna rafiki yake ambaye hupenda kumueleza mambo yake na yangu hata yale ya siri.
Nikawa nimestuka hali hiyo nilimweleza dada huyo ambaye huuza pombe katika kibanda na nyama ya nguruwe kuwa anayoyataka yatatimia kwa kuwa alikuwa akiongea baadhi ya mambo kinyume nyume kinachohusiana mimi na mchumba wangu tena mambo yenyewe yakiwa ni siri kati ya mcumba wangu na mimi.
Basi siku moja alikuja kutoka Moshi akamweleza rafiki yake huyo ambaye mimi nahisi ndiye mnafiki kuwa eti ana mazungumzo na mimi nilimfuta nyumbani kwao saa za jioni akaniambia ni kweli anataka kuongea na mimi lakini kwa muda huo alikuwa akitoka akielekea Ngaramtoni kwa rafiki yake nikaachana nae nikarudi kwa huyo dada na kumuuliza ni kitu gani anachiotaka kuongea Agness. Akaniambia kuwa eti anataka kuachana na mimi na alishamweleza kila kitu dada huyo na kesho yake aliporudi kweli akanielezea kusudio lake na nilipomuuliza sababu yeye alisema kuwa ameamua tu na kwa sababu ya mama yake kumkataza eti jamani baada ya miaka tisa nikiwa naye tena nilianza naye akiwa ni mtoto kabisa.
Lakini siwezi kuwaficha kitu chochote juu ya huyo binti ila nakumbuka mwanzoni mwa mwaka huu nilimuita msichana huyo chumbani kwangu ni ilikuwa ni kujaribu vipi kuhusu ahadi yake na mimi baada ya mambozii fulani nilimweleza kuwa nilikuwa nataka kuachana naye. Nilitingisha kibiriti. Kwa kweli alistuka sana na aliponiuliza ni kwa sababu gani sikumweleza kitu chochote na akaamua kuondoka chumbani kwangu na asubuhi ilipofika alinitumia barua kwa mdogo wake na ndani ya barua hiyo alikuwa amesema kuwa hawezi kuishi bila yangu hivyo ameamua kujinyonga na akasema tukio hilo atakwenda kulifanyia chumbani kwangu.
Kwa kweli nilimsihi sana asifanye hivyo na akanielewa baada ya kumwita na kuongea naye kuwa nilikuwa nataka kujua msimamo wake katika uhusiano wetu na alinielewa tukarudia kama zamani tena kwa upendo zaidi hadi kilichotokea hivi ajuzi.
Hivyo ndgu zangu wadau naomba ushauri wenu maana nimeshindwa kuvumilia kwa sababu ninampenda sana na tumeishi naye kwa muda mrefu tangu wote naweza klusema tulikuwa wadogo maana mimi nilikuwa ndio nimemaliza darasa la saba na yeye akiwa darasa la tano mwaka 1999 mpaka leo ameamua kuachana na mimi je?
Wadau nifanyaje???
Mdau A-taun

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 38 mpaka sasa

  1. Kilichunifurahisha ni mwanajeshi kuhamishiwa Arusha ili kuziba nafasi y akatibu tarafa, Hivi huyu ni praiveti au kopolo?

    Halafu humtaji mpenzio, twamjua ni AGNESI.

    Ila stori yoote ni ya kawaida na imewakuta wengi, haistui.

    ReplyDelete
  2. Go get a life!STUPID BOY!Sehemu ipi ya NO hukuelewa? N au O?

    ReplyDelete
  3. Ufanyeje!? Nawe Jinyonge Pia!

    ReplyDelete
  4. Michuzi,

    Acha kutuwekea hadithi za kitoto hapa.
    Hawa watoto badala ya kwenda shule wanaishia kufanyana darasa la sita halafu wanauliza ushauri. Kwa nini hawakuuliza wakati huo.
    Huyo kijana mwambie mwenzake amepata mambo ya kufurahisha kwa mwingine. Yeye zilipendwa.

    ReplyDelete
  5. Ok ngoja waosha vinywa waje kutoka maboksini halafu watakupa ushauri..

    ReplyDelete
  6. Achana nae. Kuna wakina dada wengi tuu utakaokutana nao mbeleni. Haya mambo eti mlikua nae tangu utotoni, achana nayo .. Get a life my brotha, hangaikia maisha kwanza.

    ReplyDelete
  7. sioni cha kushauri! ulikuwa na matatizo..umeyatatua!! sasa ..tufanye nini..mimi naona ni historia ya pwagu na pwaguzi!!

    ReplyDelete
  8. Hiyo royal college ulimazia au?
    Kama bado inabidi uhame maana uandishi bado ni finyu mmno. Au umespeshalaizi kwenye katuni na mashairi? Habari yako ina kichwa, kichwa, kichwa, na upuuzi mwingine mwiiiiiiiiiiiiiiiiingi. Kama wewe ndio utakuwa muandishi wa habari basi ndio maana habari ni finyu sana bongo. Tafuta ajira nyingine. Eboooooooo!
    Michuzi usiibane hii nakujua tabia yako ya kubania watu weye.

    ReplyDelete
  9. EBWANA HAINA CHOBO, UNABID UKAMATWE MAANA UMEKIAKA SHELIA KUTEMBEA NA MTOTO, 1,
    2) DEMU KAPATA ANAE MPA MAMBO MAZITO LABDA MJOMBA KAZ HUWEZ NDANI YA 18 ,SASA MTOTO KAPATA ANAE KWENDA MBAKA ANAPITILIZA NDANI YA 18-..........USISHANGAU UPOA MPYA MAANA NA MIMI NILIMREMBO MREMBO MMOJA AKANIPIGA KIBUTI NA SASA YUKO DALLAS, TEXAS KWA HIYO HAHAHAHA, CHUKUA MPYA MBONA WAKO KIBAO ILA MCHUKUE MTOTO WA KIKWAYA SANA SIUNAJUA MNGOMA NI SOO MTU WANGU

    ReplyDelete
  10. Wewe huna deal. Kwanza unatakiwa uende jela ulipofanya naye mapenzi akiwa darasa la sita wakati huo ulishafikisha miaka 18. Na sio hivyo ni haki yake kutoka huko nje kuijua dunia kabla ya kuamua kutulia na kuanza familia. Wewe unaonekana ni mtu controlling umembikiri na sasa unataka kummiliki maisha yake yote. wacha aonje huko nje na kama anakupenda atarudi. So far inaonekana sio hivyo, hivyo anza mbele

    ReplyDelete
  11. Mhhhhh Kwanza mlianza vitu vya wakubwa mapema sana. Sasa hivi hata mkitaka kuoana hainogi tena.....

    Pili wote mnahitaji kukua bado. Mnaonyesha kuwa wote ni watoto wadogo tu. Unatingisha kibiriti, anataka kujinyonga mbona mambo ya watoto wadogo hayo? Unatingisha kibiriti ukiwa ndio umeanza tu kumdate mtu miaka tisa bado unatingisha kibiriti ..... Ungekua umekua mambo ya kutingisha kibiriti hayapo tena mkishaaminiana unatingisha kibiriti cha nini tena....au kwa vile mlishaanza to do the deed a long time ago sasa hamna excitement yeyote kwenye mapenzi yenu sasa mnayapump kwa kutingisha kibiriti na yeye anachallenge back kwa kusema atajinyonga....


    Hebu kueni kwanza.... darasa la nne Duh mbona mlikua changu doa mapema hivyo?

    jamani kama kuna watoto wanasoma hii blog huko bongo someni kwanza muache mambo haya.....darasa la nne kweli mlikua mnajua protection yeyote? Mbona mnakua haraka siku hizi I can't imagine mtoto wangu akiwa na miaka nane aanze kufanya mambo haya....Wewe Agnes wewe......

    Michuzi usinibanie hii inabidi tuwape hawa watoto darasa kidogo. Sijui ni TV zinawaharibu siku hizi mbona enzi zetu hatukukua hivyo na haraka hivyo?

    I am telling you little gals trust me it worth the wait

    ReplyDelete
  12. Poor u, hata hujui kuandika jina la chuo chako halafu unajiita msomea uandishi?? Sasa ndugu, mnaanza ngono (maana wote hamjua mapenzi mpaka sasa) darasa la 4 na unafurahi kabisa kutusimulia utoto wako. Get a life Man na urudie sekondari tena unaweza kufanya vizuri maana naona ngono ilikuzuzua hata jina lako nahisi hujui kuandika.

    ReplyDelete
  13. ETI UNATINGISHA KIBIRITIIII...KIMEJAA KWA TAARIFA YAKO. WANAUME MKIPENDWA MNAJIFANYA WAJANJA. LABDA KACHOKA KUPIGA DEKI KWA MAMA MKWE INAFANYA MIKONO YAKE INAKUWA SUGU!

    ReplyDelete
  14. mie nakushauri kama kuna chuo kinafundisha fani ya ngono bora uende ukajiendeleze hapo, nadhani una kipaji cha ngono tangia udogoni, darasa la saba tayari ulikuwa na mke???, .... kama inauma zaidi jinyonge uume wako tu, kisha kisha utajua elimu dunia ni nini! acha kuharibu fani za akina michuzi, mwandishi gani wee unaandika habari hovyo hovyo kihivi?? au ndo uko field??, mpenzi jina kapuni, kisha mpenzi agness....

    ReplyDelete
  15. KAKA MICHUZI
    NI KWELI HII NI BLOG YA JAMII LAKINI UPUUZI KAMA ANAOUELEZA HUYU BWANA MDOGO HAUPASWI KUTUNDIKWA HUMU!!!!KWANZA INABIDI TUMSHTAKI KWA KUANZA KUMBAKA HUYO BINTI TOKA AKIWA DARASA LA SITA KWANI NINA UHAKIKA ALIKUWA HAJAFIKISHA MIAKA 18!!!
    PILI HADITHI ALIYOLETA NI YA KITOTO SANA AMBAYO WATU WAZIMA KAMA SIE HATUNA MUDA WA KUMSHAURI!!
    TATU NISIJENIKATUKANA BURE, TAFADHALI USITUBANDIKIE HADITHI ZA KUPUUZI KAMA HIZI!!!!KEROOOO NA ZINATUHARIBIA SIKU!!!!!!

    ReplyDelete
  16. huyu kaka anaboa. Yani story haina maana yoyote. Kaka mithu vitu vingine usiweke kwenye hii blog yetu ya jamii. Lingine baya zaidi ni kuanza mapenzi mkiwa watoto. Yani mnakera haswaaaa. Na bora kakuacha.

    ReplyDelete
  17. Jamani huwa mnachonga sana humu coz hayajawafika au unafiki unawasumbua. Pole kaka yangu, yape matatizo yako muda utapata majibu. Usiharakishe kufanya uamuzi. Time will tell you everything

    ReplyDelete
  18. Michuzi, what is this!! Hivi hii blog inaelekea wapi, how can you allow such a thing to be posted in your blog. As a matter of fact, you just lost me,

    ReplyDelete
  19. Me sijui nianzie wapi jamani, yani nimecheka sana..hii sio ishu!! halafu kwa jinsi ulivyoandika unaonekana ulivyo mshamba, demu atakuwa kachoka ile mbaya, kapata mtu fresh na majamboz ya kiutu uzima, hayo mambo yenu ya kitoto ya kufanya kwa kujifunza hayana deal, anon aliyesema umembikiri na unataka kummiliki ni kweli kabisa, get a life!! mbakaji mkubwa!! na hao wazazi/walezi nao ni wajinga sana, yani mmeacha mtoto wenu anangonolewa tokea darasa la 6 sijui la 4 na nyie mnachekelea tu!! watu wazima hovyooooo!!!!

    ReplyDelete
  20. MI SIAJAWAHI KUSOMA UTUMBO NA UPUZI KAMA HUU...HUU NI UPUZI MTUPU! NA ULIKUWA UNAFUKIRIA NINI ULIVYOKUWA UNAANDIKA ETI TUTAKUAMBIA POLE SANA KWA YALIYOKUPATA SIJUI FANYA HIKI NA KILE@!? 4GET IT! U KNOW HOW TO HANDLE UR RELATIONSHIP NDIO MAANA UKAANZA MAPEMA INABIDI UPEWE TUZO MANAKE SIO KAZI NDOGO MTUWANGU, NA HADI LEO BADO UNATAKA TUU HIYO NANII YAKE HUJAICHOKA?? BASI MWENZIO KAICHOKA YAKO NDIO MAANA ANAKUKIMBIA. USHONA WAPI MTU ANAKULA MBOGA ILE ILE KWA MIAKA 9, HAJUI UTAMU YA MBOGA ZINGINE AHHHH MWACHE AKAJITAFUTIE NA YEYE

    ReplyDelete
  21. eti amesomea uandishi wa habari!
    jamani tutafika kweli?

    ReplyDelete
  22. jamani wadau wa blog ya jamii mbona mnakuwa watu msio heshimu hisia za wenzenu? kijana ameomba ushauri kuhusu mambo yanayo msibu nyie mmeichia kumuandama kuwa ajui kuandika n'k. naomba kama mtu anaona awezi kutoa ushauri wake kwa sababu hadithi ni ya kitoto awachie wanaoweza kumshauri.
    hakika hii ni blog ya jamii maana kila mtu na mtizamo wake.

    kaka michuzi pls usibanie comment yangu.

    ReplyDelete
  23. Kwa kweli nashangaa huyu jamaa anaomba ushauri gani maana kama alianza mapenzi utotoni na hakuona haja ya kuomba ushauri, ushauri wa nini leo au kwa sababu maji yamemfika shingoni? Siku zote "The end justfies the means".Huo ndiyo mwisho wa mapenzi ya kitoto.

    ReplyDelete
  24. hehehe...naona watu wamekubania ushauri na kuamua kukuponda...hehehe

    Jaribu kuongea na mamake...yeye si ndo sababu? Ongea naye uone kwa nini hakutaki wewe. Familia ina sehemu yake katika mapenzi...na kila mtu anaipa 'value' tofauti. Wengine wanaweza kutosa ushauri wa familia na wengine hata siku moja! Ongea na mama na msichana mkae sehemu muelewani. Hapo hakuna kulala mpk kieleweke!

    mtoto

    ReplyDelete
  25. Jamani hii ndio karne ya 21 au vipi?mapenzi darasa la nne,dunia ya leo imekwisha.Enzi zetu mpaka unamaliza primary hakuna kitu kama hicho,hiyo secondary hata kama unampenda mtu mtaishia kutizamana tu basi.

    ReplyDelete
  26. hadithi inakuboa unaisomea nini? na bado tu unapata kutoa comment, mbona hivyo....kila mtu ana uzito katika maisha yake,inaonekana jamaa hakuwa na nia mbaya ila kama umeshindwa sio ndo muanze na kumtukana

    UNALOLIONA DOGO KWAKO, BASI KWA MWENZIO....kama hukulengwa leo ujue ipo siku...

    na hao wakujifanya wazamani sana, inamaana wenzi wenu wote mlipowapata kwa mara yako ya kwanza walikuwa umri gani....? 2kubali ni hali ya kibinadamu na wala sio mambo ya wenze2, kwani WHO THE HELL ARE THEY ANYWAY....!!!

    ni hayo tu...

    mdau, ukerewe

    ReplyDelete
  27. kama kawaida waosha vinywa wanatema cheche-wewe kama ulitikisa au tingisha utajua mwenyewe ila inawezekana na huyo demu wako uliyetaka tusimjue lakini ukamtaja ana kurudishia na wewe kukuona kama kweli unampenda,na kwa kuwa wote ni wachanga kwenye GAME inabidi utafute maisha kwanza na usugue msasa nje then utajua nini kimemkuta mwenzio.

    ReplyDelete
  28. WEEE MICHU
    SASA KUBANDIKA HII TAARIFA UMU UNATAKA TUCHAFUE HEWA NINI??MAMBO AYA YATUNDIKWA UTAMUNI KULEEEE,,,
    TUKIPOST MIJITUSI UMU UTASEMAJE AU NDO KAZI YAKO SIKU IZI KUDELETE MESEJI ZA WADAU???IL'HALI WATUPA IZI JUMBEZ ZA UCHOKOZI
    WATU WANA HAMU YA KUMWAGA MITUSI NA IZI STRESS ooohooooh

    ReplyDelete
  29. Michuzi TAMWA tumeamua kulala mbele na huyu jamaa. Tafadhari utuletee kesho kwenye ofisi zetu Anafanya Matusi darasa la SITA salaleeeeh! Come on!

    ReplyDelete
  30. DU! KIJANA INASIKITISHA KWA UWEZO WAKO WA KUJITAMBUA NA KUJILINDA KIUSALAMA KWA MATUKIO YA AIBU ULIYOFANYA-HATARI SANA MAANA UMEJITOLEA USHAHIDI MWENYEWE KUWA ULIVUNJA SHERIA;UKIPELEKWA MBELE YA VYOMBO VYA SHERIA UMEKWISHA!!! UTAUNGANISHWA NA WANAOENDELEA KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUSHINDWA KUTIMIZA WAJIBU WAO VYEMA ENZI HIZO!!!SHAURI YAKO....badala ya kutafuta jinsi kurekebisha maisha yako,unahangaikia ngono-fikiria kwa mapana,usituletee vituko vyako vya uswahilini;ujinga unavizia vizia tu badala ya kukomaa na kitabu!kama utaendelea hivyo,utakwama kaka. "we kalaga baho..."

    ReplyDelete
  31. Ushauri wangu ni kwamba ukimwi unaua!Bado nimtoto sana kujitafutia matatizo!Nenda shule ukatoe ujinga!

    ReplyDelete
  32. Du,,, nimefurahi huyu binti kukubwaga kwani amegundua kuwa muda wote taku mmeanza kufanya upuuzi ulikuwa ukimbaka, halafu kusema eti ni mama kasema waarusha hawaolewi na makabila mengine, bedwe umedanganyika, mie Muarusha nimeoa kabila tofauti na waarusha, dada zangu wengine wameolewa na wasio waarusha. Bro Mithupu tupe jia la huyu maumba mbakaji maama anastahili kuishia Segerea, nahisi ulimrubuni huyu binti halafu wasingizia mlipendana, stupid boy huoni haya kutueleza kuwa we ni mbakaji?.

    ReplyDelete
  33. haya mambo ya dunia, ngono tamu, lakini imeingia mdudu, kijana jihadhari sana, mtu akisema basi, ndo basi, tafuta duka lingine la kununua sukari, huwezi kumlazimisha mwenye duka akuuzia wakati hataki hata kama mteja ni mfalume.

    ReplyDelete
  34. isa huyo jamaa miyeyusho sana ye katikisa kiberiti demu kataka kujiua kamwomba radhi yakaisha na yeye si atangaze kufa tuone demu wake atafanyaje demu akikomaa poa tu amtafutie ishu nyingine poa kuliko yeye mwenyewe atatulia

    ReplyDelete
  35. jinga jinga jinga jinga x 100,000. Best advice, bei ya sumu si ghali sana,haswa ya panya. huwezi kuwa na brain kama hiyo halafu uendelee tu kuishi!what for?kwanza mbakaji,pili umesoma mpaka sijui 'royal' ya uandishi halafu usichoweza kabisa ni uandishi. tatu wewe mtoto wa katibu tarafa unajitangaza ungekuwa wa 'mzee wa vijisenti?' mwisho unashindwa na mwalimu wa nasari utampata nani tena! kwenda zako kafie mbele. nyambafu.michu usibane, lazima tuwafundishe hawa watoto jinga jinga jinga kwendaaaaa!umeniudhii!akili nyepeesssssiiiii kama unanawa!

    ReplyDelete
  36. Nawashukuru wote mlionipa ushauri wenu nakubali kuwa kuna walioshauri na kuna walionitukana lakini yote nayachukulia kama changamoto lakini nilichokihitaji nashukuru nimekipata na nilijua si wote wanaweza kunishauri vizuri,kuna baadhi wamesema nipelekwe Lupango kwa kubaka,wengine wamesema kuwa eti demu amegundua kuwa nilikuwa nambaka,kuna waliosema sijui hata kuandika jina la chuo nilichosomea pamoja na jina langu na ninaharibu fani za kina Michuzi kuna waliosema story yangu ni utumbo kuna walisema eti nipewe tuzo kwa kuanza ngono mapema wote nawashukuruni sana hususani kaka Michuzi kwa sababu nilimwandikia e-mail zaidi ya tatu ili aweke story yangu nisikie na wengine wanasema nini haya mambo yanatokea karibu kila siku nilichohitaji ni kupata experiance ya wengine juu ya mambo haya NAWASHUKURUNI WOTE KAMA KUNA WANAOPENDA KUENDELEA KUTOA USHAURI WAFANYE HIVYO LAKINI SI KWA KEBEHI>

    ASANTENI

    ReplyDelete
  37. Sasa kaka unahangaika nini???si uchukue kamba ujinyonge????unapoteza muda tuuuuuuuuu!!!!!!

    ReplyDelete
  38. IMEBIDI NIRUKE MOST OF THE ARTICLE TO GET THE POINT.... WANASEMA YOU CANT SOLVE YOUR PROBLEM UNLESS UMEADMIT NA UNAJUA TATIZO NI NINI..... YANI KAKA ULUVYOIVUUUUUUUUUUUTA HII STORY NDIVYO UNAVYOISHI THAT EXPLAINS WHY SHE LEFT YOU...LIVE HER ALONE AND FIND SOMEONE ATAKAYEKAA KUKUSIKILIZA WHEN YOU KEEP REPEATING YOURSELF....SHE IS A TEACHER SHE CANT LISTEN TO ALL THEM MAKELELE YA WATOTO AND COME HOME TO MORE NONSENSE...SORRY A GIRL KNOWS WHAT SHE WANTS AND THE FACT THAT YOU KNOW HER TANGU UTOTO AS NOTHING TO DO WITH IT ...ALL THAT TIME YOU WERE TALKNING WITHOUT LISTENING TO HER.... JIFUNZE FROM THIS

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...