jiji la addis ababa
nguo zenye nakshi za kitamaduni ziko bwelele tena kwa bei poa. birr 20 tu umevaa. hapo dola moja ya kimarekani ni sawa na birr 10. kwa madafu utajaza mwenyewe
sehemu ya wafanyabiashara wadogo wadogo kama pale ubungo
vijana wengi wamejiajiri kupiga viatu dawa
addis tambarare
sehemu za uswazi
mandata wao hupiga kombati kama hivyo


punda nao si haba uhabeshi ambako ni miongozi wa wanaongoza kwa ufugaji barani afrika. hapa ni maeneo ya soko kuu ambalo ni kubwa kuliko yote afrika.
kila kona ujenzi wa majumba unaendelea. kwa nyuma ni kanisa kuu la orthodox ambapo wahabeshi wengi ni waumini
uswazi karibu na taun
kwa miundombinu wenzetu wako mbali
obama anauza kama njugu uhabeshi
teksi zao karibu zote ni aina y lada za kirusi

vekesheni bila ya ze fulanazzz ya jamii huwa haijatimiagi...
ukichoka kukata shingo na mabega unakwenda tam tama kula mayenu katikati ya addis ababa
kajishopingi ka kiushkaji. wenzetu mteja ni mfalme

wenyeji ni wakarimu na hupenda kudumisha utamaduni kwenye lanchi ya usiku ama dina ya mchana
wanja la wenzetu si mchezo
kajivekesheni ka uhabeshi kameisha najirudia zangu kula vumbi bongo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. kwa mbali nakaona ka ze fulanaz!

    ReplyDelete
  2. Hakuna mpango huko! Boea urudi tuendeleze libeneka. Mtu gani una-access blog mara moja kwa siku mbili huko!!?

    Bongo tambarare tu. watu wengi wabishi bila sababu!

    ReplyDelete
  3. Nilizania huko mlikwenda na private jet? ahhhh bwana vacation yote hiyo

    ReplyDelete
  4. ze fulanaaaz inaonekana hehe leo imegeuka shati la tai,hehehe kama umeishiwa njoo vumbini.

    ReplyDelete
  5. Hivi anayekupiga hizi picha kila siku uko ughaibuni ni nani?

    ReplyDelete
  6. nivizuri kama unajuwa bongo tunakula vumbi

    ReplyDelete
  7. dah,hio style ya kuchovya kwenye bakuli moja la mchuzi watu wote kwa mkono bado ipo tu?kipindupindu ndio maana hakiishi afrika,

    ReplyDelete
  8. WENZETU MTEJA NI MFALME, KWANI KWENU BONGO MTEJA NI ADUI? MBONA UNATURUDISHA NYUMA MICHUZI???

    ReplyDelete
  9. Kaka Michuzi wadau wa Trondheim (Norway)tunakuomba basi uje na huku ukipata kavekesheni maana unaambaambaa tu mara ujerumani mara...Ahsante sana kwa blogg hii maana nisipofungua hapa siku yangu haijakamilika.Umetuunganisha na unatuma yote yanayoendelea home.Udumu!

    ReplyDelete
  10. Mh. bro. Mithupu kulikoni umetusikitisha wana blog ya jamii kwa kitendo cha kurudi pekeyako na kumuacha kijana wetu Ivo Mapunda mahala pasipo na dalili za kukuza kipaji chake labda abadilishe fani na aanze kucheza ngoma za kutikisa kichwa make hapo kwa muonekano wa kawaida no challenge.

    CHANGARAWE

    ReplyDelete
  11. Wenzetu wana ndege, marubani, mafundi, na kila kitu chao.

    Walianza zamani na wanaruka mabara!

    Viongozi wetu waache uchu: Taifa kwanza; achaneni na biashara na hali mnalipwa na umma. Wakati upo wapi wa kufikiria cha umma, kama siko kuibia umma!

    Tuwaheshimu! Walitusaidia sana kukarabati videge vyetu mwanzoni mwa kuanguka kwa East African Airways, huku tukitarajia ugeni mkubwa sana wa kimataifa, la sivyo tungeaibika sana!

    Majirani (eti watani wa jadi) wakatupiga vikumbo!

    ReplyDelete
  12. unaposema unarudi bongo kula vumbi, unataka kutuambia huko ethiopia hakuna vumbi?

    ReplyDelete
  13. Uwanja nje tu hyuo. hauna lolote! Kaa wetu tu. Ndani kumejaa vichangu kibao vinauza nguo mle. Ukiingia kichwa kichwa utaona vinakuonyeshs matiti, ati vinasema .. this is yours..,, give me 100usd! Sasa huko mitaani inakuwaje?! Ila uzuri bila ubishi, ni vizuri sana kwa shape na sura.

    ReplyDelete
  14. Hayo wabongo wenzagu mambo hayo mnayaona Ethiopia ni chi ambayo haina kitu ukichukulia rasimali lakini angalia hatu walivyo ipiga hatua kimaendeleo impression tu ya airport inakuonyesha watu walivyo develop kwa kiasi fulani siyo mambo ya kwetu eti Mwl. Nyerere intern. airport jamani hii ni aibu sana, basi kama hatuna uwezo wa kujenga uwanja mpya basi huu tulio nao tujitahidi kuutunze.. . ...intern airport haina hata vyoo ...maji hayatoki ,harufu mpaka kwenye sehemu ya checking...tunakalia longo longo ohooo.....ohoooo huku(EPA) wahindi na majambazi wa kitanzania wanajichotea mabilioni ya pesa instead of utilise the small income we have to develop our country...tunabaki ohoo watani wa jadi wametupiga kisigino , wao wako serious different with Tanzanian leaders ......
    anyway bongo tambarare mijuzi endeleza limbekene...
    Mdau wa Kamachumu...

    ReplyDelete
  15. kwanza no matter what fulana idumu

    pili hapo mnapokula pamoja huyo mtu anakuangalia na jicho hilo sijui ile michapati yao ulikua unaimaliza yote au unamaliza mboga?

    tatu pamoja na njaa yote ile huko ethiopia lakini jiji lao is a breath taking

    nne kweli bongo mteja sio mfalme kabisa. Ukienda bank, posta, hotelini na kwenye maduka ya nguo wahudumu wanadengua sana. Wanavyokutreat ni kama umeenda kuomba kumbe bila wewe wao wasingekua hapo.

    ReplyDelete
  16. Tuache uwongo Kaka Michuzi. Kwa kweli kama sikosei nafikiri TZ ndio nchi ya mwisho kwa maendeleo katika nchi za Afrika mashariki. Nimefika Adis, Kampala, na Nairobi kwa kweli tuko nyuma saana. Hata Mogadishu na shida zao hatujawapita hata kidogo, yaani Bongo tuko nyuma kishenzi. Hivi wapi tunapokosea?

    ReplyDelete
  17. Majitu mengine bwana. Huwaga nashindwaga kuyashangaa kabisa! Maana yenyewe ni mshango tayati. Sasa wewe ANNON nNov 23 11:50pm hapo juu kuona hizo picha za Addis Ababa basi umeshaona kuwa Ethiopia imeendelea sanaa! Hizo slums karibu na mji hujaona ati!? Kwani hizo barabara alizoonyesha Michuzi zina tofauti gani na zile za Bandari-Mbagala na ile ya Ubungo-Mwenge pamoja na zingine kibao!?

    Kwa Taarifa yako, picha alizopiga Michuzi ndizo best kwa Ethiopia. Angeenda mitaani au miji mingine ungekaa kimya kabisa. Usiangalie kitabu kwa rangi yake bwana!

    Tanzania tuko juu juu sana sana kwa kila kitu. Ila nyie hamtaki tu!

    ReplyDelete
  18. uhabeshi hakuna dili mwaya wasingekua wanatorokea kwao kuja kubanana na sie pale kariakoo au kule kasumulu na tunduma mbeya...asilimia kubwa ya wahamiaji haramu wanaokamatwa hapa bongo ni wahabeshi na wasomali sasa kama kwao kungekua mswano wangekuja huku..we have to be proud with our nation sio tunakandia tu kila la kwetu shida zipo kila mahali duniani hatukuona new orlens kule kwa kina obama?

    ReplyDelete
  19. bora urudi kwenu huko hakuna mpango sasa soko kuu la afrika kuna punda wanaochafua mazingira...we umeona punda walau hata kwenye soko la kule waliya unayoingoza ya tageta...bongo tambarare mwayaaa..

    ReplyDelete
  20. duh,,,hahahaha teh teheeee ze fulanazzzzzz heee michu ivi ni kweli ni iyoiyo au unazo dazeni??
    ila michu nshakushtukia ukiwa na totoz izo lzm ukomenti kiaina,,duh ujikazi???
    ndo mana shingo umeilegezaaa juu-juu hahahaaaaa
    what birr 1=$10????????heee tshs???uwiiiiii
    ilo koti na ze fulanaz apo umetisha wa'hlai.
    annon ulouliza nani kampiga pic,,,ni my waifu wake make siwezi amini asafiri vekeshen zooote izo bila mamsapu ni hatari

    ReplyDelete
  21. Hilo kanisa kweli disaini ya israeli au arabuni, mbona ya hapa yako kama ya magharibi? Kwani umagharibi unahusiana vipi na imani?

    ReplyDelete
  22. Nilipita ethiopia miaka 1990s kuelekea xxxxx,kusema kweli hakuna kitu cha maana hata hapo "Hadithi ya Baba" ni upuuzi mtupu.Nakumbuka kipindi hicho hicho kiwanja cha ndege kilikuwa bado kinajengwa.Walikuwa wanatumia kiwanja cha Zamani pembeni kidogo nadhani wengine mnakijuwa,nilikwenda chooni hata kukojoa niliacha palikuwa na toilet paper zilizotumiwa zimetapakaa kwenye sakafu(Huu sio uongo wala kuwapaka wahabeshi)Najuwa airport ya Bongo ilivyo ovyo na chafu lakini sio sisi peke yetu hata hawa "light skin/good hair" nao wachafu kinoma.
    Pili hivi hawa jamaa hawaagizi magari mapya. Miaka yote magari yao ni yale 1970's-1980. Ina maana wanashindwa kununua magari ya 1990's - present? Kwa hili tumewapiga bao kuuuuuuubwa,Dar kila kukicha ni mandinga mapya bwana sio kama hawa wahabeshi.
    *Ina maana wenye magari ni wachache au barabara(miundo mbinu) yao ipo juu kuliko sisi?
    Duh Magari yanahesabika.

    ReplyDelete
  23. ETHIOPIAN AIRWAYS IS INTERNATIONAL AIRLINES. WE TRAIN MOST ENGINEERS FROM EAST AFRICA TO SERVICE THEIR PLANES. WE BRING HOME OVER 1 BILLION DOLLARS A YEAR BECAUSE WE ARE 4 MILLION ABROAD.WE HAVE A LONG WAY TO GO BUT YOU CAN'T COMPLAIN THAT OUR COUNTRY IS DIRTY WHEN YOURS IS THE SAME. WE ARE ALL DEVELOPING COUNTRY AND BEG EUROPEANS TO SURVIVE DAY TO DAY. JUST CHECK YOUR GOVERNMENT BUDGET SINCE INDEPENENCE. MANY OF YOU WOULD NOT HAVE AFFORDED TO GO AND CLAIM FAKE ASYLUM IN EUROPE IF IT WASN'T FOR THE FACT THAT OUR PLANE FARES ARE MUCH CHEAPER THAN EUROPEAN CARRIERS OR EMIRATES. THINK BEFORE YOU CRITICISE. YOU DON'T EVEN HAVE ENOUGH UNIVERSITIES THERE, JUST GOOGLE ETHIOPIAN UNIVERSITIES AND COMPARE THEM WITH EAST AFRICAN, LET ALONE TANZANIAN UNIVERSITIES.

    GABRE HALASI, Ph.D

    (MY GRADUATE STUDENT, (HE WANTS TO BE ANONYMOUS) WANTED MY OPINION ON THIS MATTER. HE IS TEACHING SWAHILI TO ME, WE ARE TEACHING HIM CIVIL ENGINNERING IN OUR UNIVERSITY OF ADDIS ABABA).

    ReplyDelete
  24. Dear Mr. Michuzi,

    I can see that you really enjoyed our country. Please come again soon.

    I have compiled some interesting statistics for Tanzania and Ethiopia for the pleasure of your educated readers.

    All figures are 2007.
    Sources: CIA The World Factbook and www.theeconomist.com


    Kind regards,
    Dr. Halasi
    Addis Ababa


    Ethiopia Tanzania

    GDP (PPP) $56.05 billion $51.07 billion

    GDP - real growth rate: 11.1% 7.3%

    GDP - per capita $700 $1,300

    Budget: revenues: $3.231 billion revenues: $3.561 billion
    expenditures: $3.594 billion expenditures: $3.785 billion


    Public debt: 44.5% of GDP 19.6% of GDP

    Exports: $1.288 billion $2.227 billion

    Imports: $5.165 billion $4.861 billion

    Reserves of $ & Gold $1.294 billion $2.91 billion

    Debt - external: $2.621 billion $4.382 billion

    Exchange rates: birrs (ETB) per US dollar - 8.96 (TZS) per US dollar - 1,255

    Telephones (cell) 1.208 million 9.358 million

    Telephone (landline) 880,100 165,013
    Military expense: 3% of GDP 0.5% of GDP

    Education expense: 6% of GDP 3.2% of GDP

    Literacy: total population: 42.7% total population: 69.4%

    Life expectancy at birth: total population: 54.99 years total population: 51.45 years

    Infant mortality rate: total: 82.64 deaths/1,000 live births total: 70.46 deaths/1,000 live births

    Population growth rate: 3.212% 2.072%
    Population: 82,544,840 40,213,160

    HIV/AIDS (Alive) 1.5 million 1.6 million
    HIV/AIDS (Died) 120,000 160,000

    Area: total: 1,127,127 sq km total: 945,087 sq km

    ReplyDelete
  25. We Anon wa November 25, 2008 10:25 AM, naona una ujinga typical wa kibongo. Hivi kuwa na maendeleo nchini ni mpaka uwe na magari mapya? Tuache uwongo Ethiopia wanatupiga chenga ya mwili katika miundo mbinu, kama uwongo tafadhli Michuzi nikosoe. Nilikuwa Adis mwezi uliopita kikazi lakini ukweli lazima usemwe, hawa jamaa pamoja na shida zao zote wametupiga chenga katika miundo mbinu. TZ kweli bado tuko nyuma hata Uganda na Kenya zimetupita ki-miundo mbinu. We Michuzi na mimi hatutambiani, umetembea sana barani afrika tafadhali kama nadanganya hapa nikosoe. Wabongo lazima tukubali ukweli msipende kubishana tu for the sake of arguing, huo ni ujinga. Nyie kazi kubishana wenzenu wanasonga mbele. Kuna jamaa alisema alikuwa Ethiopia miaka ya 90 na uwanja wao ulikuwa hovyo. Wao waliona vile wakajirekebisha kwa kujenga wanja la kisasa ambalo Bongo hatuna, wana maji na vyoo vinaflush, kuna air condition mle ndani lakini Bongo hii kitu hatuna. Vyoo vyetu haviflush na uwanjani (inside) kuko too hot hata air conditoin hakuna. Je huu ni uwongo? Acheni upuuzi! Bongo tukoo nyuma sana kimaendeleo we angalia mpaka Rwanda inatupita siku hizi, na sisi tuko pale pale. Kila kukicha magorofa yanaporomoshwa kiholela bila mpangilio wowote wa jiji, mvua ikinyesha tu, mavi yanafurika mitaani. Come on you guys...get a grip.

    ReplyDelete
  26. Anony 8:57 pm hapo juu, nadhani unataka kumjibu wa 2:09, kwa kuwa 10:25 ni Mhabeshi na haongelei magari.

    Lakini, naakuunga mkono vile vile, Bongo maneno mingi na nchi nyingi kama Rwanda zitatupita tu kwa kuwa sisi ni wavivu. Mpaka China atujengee kiwanja kwa mfano, kilikuwa kinaoza. Leo tunapiga kelele sana kama vile tumejenga wenyewe.

    Kuhusu eapoti yetu, nchi nyingi zinapanua eapoti kutokana na biashara inavyokua, lakini yetu iko pale pale, haijabadilika kabisa. Nadhani kitu muhimu Tanzania hatujui ni kumfurahisha mteja. Kenya wameshapanua yao, na nchi jirani nyingi wanafanya hivyo pia.

    Tukienda kwa IPP media kusoma habari, utaona kuwa haijabadilika pia. Huwezi kusikiliza redio yao wala kutoa maoni yako. Website imekaa vile vile na kuna habari chache tu zinazobadilishwa kila siku. Je, hatuna wasomi wa Sayansi ya Komyuka hapo IPP au ni uvivu tu?
    Hata Balozi, japokuwa yuko bize na shughuli za kikazi na vekesheni, ameweza kubadilisha websiye yake mara kwa mara kuiimarisha. Labda IPP iimpe dili ya kuifanya iwe imara kidogo. Iangalie hio IPPMedia halafu nenda http://www.eastandard.net ya Kenya, utaona jinsi tulivyo nyuma sisi kimaendeleo. Yaani The Standard inaghara sana utafikiri unasoma BBC.

    Tanzania tusistuke kama tutapishwa kiuchumi na Rwanda au Burundi hivi karibuni. Tuamke jamani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...