Mwanamuziki Alikiba amevunja rekodi ATLANTA kwa kuwa mwanamuziki wa kwanza kutoka Africa mashariki na kati kufanya show Marekani Iliyofana na kujaza watu (zaidi ya 1000).

Show hiyo iiloandaliwa na vijana machachari wa Takeover Dj's, ilifanyika siku ya ijumaa 11/28/08 kwenye ukumbi mkubwa na maarufu Atlanta wa "THE DREAMZ."

Alipoulizwa anajisikiaje kufanya show kwenye ukumbi huo ambao kwa kawaidia unatumika na masuperstar kama MARY J BLIDGE, P.DIDDY NA JAYDEE na kufunika, kama kawaida yake Alikiba alimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumpa uwezo na pia washabiki wake wote waliojitokeza kumsupport na kuahidi atamaliza tour yake kwa nguvu huko

OAKLAND CA 12/05
SEATTLE, WA 12/06
na
DALLAS TEXAS 12/13.

WATANZANIA WOTE MNAOISHI HAYA MAENEO TUNAWAOMBENI MJITOKEZEE KWA WINGI ILI TUENDELEE KUMSUPPORT KIJANA WETU.

ASANTENI NA SIKU NJEMA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. oh please..umemuweka jaydee kwenye list ya superstars wa states kama diddy na mary j??? come on now...

    ReplyDelete
  2. WATU ZAIDI YA 1000, AMETIA FORA, MMMMMMMMMMMM!!! 1000?

    ReplyDelete
  3. hivyi huyo ally kiba wanamlipa fresh kweli au ndo wanamtumia tuu kutajilisha watu then yy mwenyewe ajijui?? michuzi embu try kuuliza per show wanamlipa how much!!

    ReplyDelete
  4. Wee mshamba anony wa kwanza, Jaydee here refers to Jermaine Dupree (producer and recording artist)

    ReplyDelete
  5. watu 1000?sio kweli mbona hamjaonyesha picha mgepiga picha tuone hao watu buku, hii ni fix.
    hii ni advert watu waje wengi kwenye maonyesho mengine

    ReplyDelete
  6. HABARI HIZI NI UZUSHI MTUPU.wameshaona wa2 wamemchoka huyo Ali Kiba sasa wanaleta usanii mwingine.
    Fridays Club Dreamz hawawezi kuwaachia ukumbi kwa ajili ya huyo Ali Kiba hata kiduchu.kwanza kwa pesa gani ambayo mngewalipa??na pili hao wa2 weusi na wasivyoijua lugha ye2 si wangedai REFUND??teh teh teh
    kama alikuwa Dreamz ATL labda kwa huzuru binafsi na sio kupiga show.
    PLZ STOP blah blah blahaaaaaaaa.

    kama vp tuwekee uthibitisho wa pix akimwaga radhiiii.tena ktk hizo pix yale maplazma walau mojawapo lionekane.hahahaha

    ReplyDelete
  7. wajameni sasa mnaomba waTZ wajitokeze kumsapoti Ali Kiba au waje ili mpate "vijisenti vya kulipia bili zenu?".pumbuzeni porojo za "uwana-siasa".kama sapoti alishapata alipokuwa mgeni miezi 4 iliyopita.hivi sasa hana kamba tena mguuni..he's on the loooooose.........
    anyways,mlio jirani na maeneo hayo pelekeni sapoti zenu.

    ReplyDelete
  8. Jermaine Dupri anafupishwa JD sio Jaydee kwa hiyo hata wewe anony wa 250pm usijifanye unajua saaannaaa!! Jamaa anashangaa mataa na madaraja na magorofa ya Marekani tu akahadithie Kigoma kwao basi..!! Hawampi cheddar wala nini!! Ananuliwa vinguo akauze sura bongo...!! Ila dogo pumba tuu!!

    ReplyDelete
  9. funga kamba tupu, nasubiri malalamiko kwa walihudhuria

    ReplyDelete
  10. Ukipiga kwenye ukumbi ambao wamepiga masuperstar sio kuwa watu wamekukubali ni kwa vile waliupata kwa bei nzuri.

    Hamna hata watu wa USA 10% hapo sasa ukikubalika sio ukubalike na wakenya na wabongo tu bali na watu wote.

    Ni mtu muimbaji mzuri lakini kumfananisha na mary J, P diddy that is too much. Kwa hiyo walioingia hapo kwenye huo ukumbi siku hio nao unawafananisha na paris hilton, michael jordan, Don Lemon etc wote hao wameshaingia kwenye huo ukumbi pia

    ReplyDelete
  11. THATS NOT TRUE!!!!!
    Ilifanyikia katika ukumbi wa hoteli ya Ramada, tena hao maorginizers were sooo disorgized maana show haikuanza mpaka around midnite alafu mapolisi shut it down around 2 am...kila mtu alikuwa vey very disappointed in this show. Kama mnataka tumsupport, all you have to do is ask but dont tell no lies.

    ReplyDelete
  12. Jamani mwachieni dogo arudi kwao basi! Mpaka ifike mahali hamna mtu anakuja kwenye show yake ndio muone sasa basi! Na dogo mwenyewe hata hastuki.....

    ReplyDelete
  13. ninamtafuta ndugu yangu huko Texas Delton yeye ni Grolia na Floral Mochiwa please watu wa Mexico nisaidieni Grolia ameolewa na Marines polise na ninaskia ya kwamba yeye na nduye wanacafteira

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...