WADAU WATUKUFU,
KAMA MNAVYOWEZA KUONA KATIKA TARAKIMU ZA HAPO CHINI KULIA KWENYE GLOBU HII YA JAMII, MDAU WA MILIONI 5 ANAKARIBIA SANA NA KAMA KAWAIDA MDAU ATAYEBAHATIKA KUWA WA MILIONI 5 ATAJINYAKULIA DOLA 500 KESHI KAMA ZAWADI IKIWA NI KWA HISANI YA DUKA LA ARISE BEAUTY SUPPLY
ILI KUWEZA KUSHINDA KWA KULETA USHAHIDI NI RAHISI SANA.
KWA WASIOFAHAMU NI KWAMBA PINDI UFUNGUAPO GLOBU HII YA JAMII, ANGALIA TARAKIMU ZA HAPO CHINI KULIA NA UKIKUTA 5,000,000 IPO HAPO UJUE WEWE NDIYE MSHINDI.
UNACHOTAKIWA KUFANYA NI KUBOFYA KWENYE KOMPYUTA YAKO MANENO 'Prt SC Sys Rq' AMA YOYOTE YANAYOHUSU KUNAKILI UKURASA, KISHA BOFYA KITUFE CHA 'start' CHINI SHOTO NA TAFUTA 'Paint' AMBAPO UTAKWENDA TENA NA KUBOFYA PENYE 'Edit' HALAFU NENDA 'Paste', NDIPO UKURASA WAKO UTAKUWA UMEUKOPI NA KUUBANDIKA KWENYE UKURASA HURU.
BAADA YA HAPO NI 'Save' NA HIFADHI UKURASA HUO SEHEMU UNAPOHIFADHI VITU UNAVYOPENDA KU-ATTACH KABLA YA KUMTUMIA MTU.
KISHA ANDIKA EMAIL KWA
NA ITUME UKIWA UMEWEKA JINA LAKO SAHIHI, MAHALI ULIPO NA IKIWEZEKANA HATA NAMBA YA SIMU ILI IWE RAHISI KUKUPATA. UKURASA UTAOTUMA UTAKUWA KAMA HUO HAPO JUU. SI VIBAYA UKAJARIBU SASA NJIA HIYO.
ENDAPO NJIA HII INAONEKANA IMEKAA KICHINA CHINA, UNAWEZA PIA KUTUMIA KAMERA YAKO, PIGA PICHA UKURASA HUO WENYE TARAKIMU 5,000,000 NA ITUME KWENDA EMAIL HIYO HAPO JUU.
MASHARTI NI YALE YALE
1. MDAU YEYOTE POPOTE ALIPO RUKSA KUSHIRIKI
2. UAMUZI WA JOPO LA MAJAJI NI WA MWISHO
3. HAKUNA KUKATA RUFAA
4. USHIRIKI KWA NJIA YA KANYABOYA HAUTOONA MWANGA WA JUA
NAOMBA KUWASILISHA
5. MSHINDI AMA MWAKILISHI WAKE ALIYETHIBITISHA ATAFIKA DUKA LA ARISE KUCHUKUA HIZO DOLA 500 NA KUPIGWA PICHA YA USHUHUDA
-MICHUZI
We Michuzi hebu rahisisha hayo maelekezo yako maana ni kweli yamekaa kichinachina kinoma!Mtu unaweza ushinde halafu upigwe bao kwa kushindwa kuelewa process. Naomba kuwaskilisha.
ReplyDeleteBro Michuzi,
ReplyDeleteShindano hili ni mazingaombwe matupu. Nafikiri huna watu ambao ni wataalamu wa mtandao. Upo kila uwezekano wa watu zaidi ya mmoja kuweza kupata namba hiyo.Last time it was proven that it was possible.Ulichokifanya ni kudispute baadhi ya entries na nyengine hukuweza kudispute.
Sasa bila shaka kwa kuwa watu wana shida ya hizo $500 basi utaweza kuwagaragisha unavyotaka lakini ukweli ni kuwa shindano lako sio fair hata kidogo.
Pia idadi ya hapo chini haiendani na idadi ya watu wanaoitembelea hii blog.Mtu mmoja anaweza akawa anaangalia blog yako na akawa kila baada ya muda anarefresh page na namba ikawa inabadilika.
Mimi sisemi kwa kuwa nna shida ya hizo hela lakini sipendi ninavyoona hakuna fairness.
Kama unataka kujaribu kuwa fair basi na kama unataka kuwepo ushindani wa kweli basi mimi nitapendekeza namna ya kupata mshindi wa kweli kweli.Pendekezo langu litaondoa vitu viwili:
1. (hili pengine usilipende) Kwanza litaondoa tabia ya watu kujaribu kila namna kuipeleka mbele namba ili ionekane wadau wanatembelea kwa speed kali. Kumbuka nilisema mwanzo kuwa mtu mmoja anaweza akaifanya namba iende haraka kwa tabia ya kurefresh.
2. Kitu cha pili katika pendekezo langu mimi kitaleta ushindani wa kweli na hakuna mtu ambae ataweza kudispute.Pia kitawafanya watembeleaji wa blog kufuatilia kwa makini habari na picha za kila siku za blog.
PENDEKEZO LA SHINDANO.
Unaweza kusema kuwa atakapofika mdau wa milioni 5 basi nitatoa shindano. Na sio lazima iwe mdau wa milioni tano inaweza kuwa wakati wowote.
Shindano wenyewe ni kuwaambia watu watafute picha kwenye blog yako yenye maelezo fulani au habari maalum. Wewe huna haja ya kusema mwezi ulioipost hiyo picha wala chochote.
Mfano:
Shindano letu ni kutafuta picha yenye noti ya milioni 50 ya Zimbabwe. au Tafuta icha inayomwonesha Waziri Mkuu wa Tanzania alipeana mkono na balozi wa Zimbabwe nchini Angola. au picha yoyote au habari yoyote ile.wewe ndie utaechagua bila shaka.Na hii haitaki utaalamu wa mafundi mitambo.
Atakaeiona mwanzo afanye vilevile kupiga picha screen kisha aitume kwako.Hakuna shaka yoyote utajua nani kaleta picha mwanzo na kama kaleta picha ambayo wewe uliisema.
Najua kuna watu watasema kusuhu timing. Lakini cha muhimu ni kusema nitaweka shindano ifikapo saa kadhaa za Bongo.Mfano nitaleta shindano ikifika saa nne asubuhi za bongo. Bila shaka saa hizo kuna ambao watakuwa wamelala, lakini kama wanataka kushiriki basi itabidi wawe macho siku hiyo. After all kuna watu wanakaa macho kutaka kufikia msdindi wa milioni tano.Lakini inavunja moyo kuona mtu kakaa macho kushinda baadae haoni namna haki ilivyotendeka.
Nahisi mfumo huu wa shindano utakuwa hauna malalamiko yenye msingi.Kwasababu kila email inakuna na saa na dakika na sekunde iliyotumwa.
Hii pia itachangamsha akili za wadau kuuma vichwa.Pia watakuwa wanasoma na kuangalia picha za kila siku kwa makini kabisa.Na sio mazingaombwe ya kurefresh page kila sekunde.
I hope wadau watachangia hili ili kuboresha libeneke ya blog na kuleta ushindani wa kweli na sio kiinimacho.
HIYO PROCESS NI YA KIJIMA MICHUZI NI UTOPIA KABISA NA KWA MTAJI HUO HATOPATIKANA MSHINDI HALALI KWANI NI MARA NYINGI TU NAFUNGUA BLOG YAKO NA WALA SIJAFANYA LOLOTE HIYO NAMBA IMESHABADILIKA MARA NYINGI TU, SASA IKITOKEA NIMEKUA WA 5000000 NA SIJAKOPI IMEBADILIKA NITAFANYAJE, EBU TAFUA NJIA YA KISAYANSI SI HII YA UJIMA, HUNA WATAALAMU WA IT? ACHA UJIMA.
ReplyDeleteWE mzee mbona si elewi jinsi ya kukopi ukurasa wote,fafanua vizuri.
ReplyDeleteEeeeh wandugu namna ya kukopi ukurasa ni kwa kubonyeza "Print scrn sys Rq" kwenye keyboard yako, kisha unafungua microsoft word halafu unakiliki edit kisha unapaste. It is as simple as that. Nimeona niweke sentenso ya kizungu vinginevo waosha vinya watakuwa hawana cha kusema.
ReplyDeleteSasa Mheshimiwa Balozi, shindano gani hilo linakuwaga na mshindi mmoja tu? Walau wangekuwa tatu bora basi.Haaahaaaaa!
ReplyDeleteMdau
Cardiff