Watu 15 wamekufa katika ajali zilizohusisha magari na treni katika mikoa ya Dar es Salaam na Morogoro, huku zikiacha majeruhi zaidi ya 20.
Katika ajali hizo mbili zilizotokea alfajiri ya kuamkia jana; mkoani Dar es Salaam, watu tisa walikufa papo hapo na wengine 10 kujeruhiwa katika eneo la Jet Club, Kipawa, barabara ya Nyerere wakati Morogoro, watu sita walikufa papo hapo na wengine 10 kujeruhiwa katika ajali ya treni la Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kati ya stesheni za Mzaganza na Kidete, Kilosa.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema jana kuwa ajali ya Kipawa ilitokea saa 10 alfajiri baada ya gari namba T 700 AFT aina ya Toyota Hiace ‘Kipanya’ lililokuwa likitoka Uwanja wa Ndege wa JK Nyerere, kwenda Tazara, kugonga lori namba T 452 ACP aina ya Scania lililokuwa limeanguka katikati ya barabara na kusababisha kifo cha abiria tisa papo hapo.
Aliwataja baadhi ya waliokufa kuwa ni Ally Issa (37), Michael Maujiro, Augustino Yohana, Elly Athumani, Alphonce Golesh, Machel Msagira (33) na John Steven.
Alisema maiti wamehifadhiwa katika Hospitali ya Amana wakati majeruhi 10 wamelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu.
Alisema chanzo cha ajali hiyo, ni mwendo kasi wa dereva wa Hiace ambayo ilikuwa na abiria ikitoka Machinjioni Pugu. Ilibainika kuwa gari hilo lilikuwa linafanya kazi usiku tu kutokana na muda wa leseni yake kumalizika.
Naye Ofisa Habari Msaidizi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), Mary Ochieng, alisema hali za majeruhi hao zinaendelea vizuri kiasi.
“Tunaendelea kuwapa matibabu … mmoja bado yuko ICU (chumba cha uangalizi maalumu) na tayari tumesharuhusu wawili,” alisema Ochieng jana mchana.
Waliolazwa ni Simon Sylvester (27), Eva Joseph (28), Kalunde Osambi (32), Zamoyoni Mongella (36), Joshua Jumanne (29), Alex Msuya (65), Emilly Steven (40) na Ratibu Abdallah (21).
Ajali ya Morogoro, ilitokea saa saba usiku wa kuamkia jana, ikihusisha treni namba 8828 lililokuwa likiendeshwa na Richard Mkude (38) kwa kushirikiana na Lucas Isaya, wote wakazi wa Morogoro.
Treni hiyo iliyokuwa na mabehewa manne, ilikuwa ikitoka Bara kwenda Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Reli, Yessaya Msigwa, alithibitisha ajali hiyo na akizungumza kwa simu akiwa eneo la tukio, alisema katika mabehewa hayo manne, moja lilikuwa la abiria, jingine tupu wakati jingine lilibeba mataruma kutoka Mpanda, Rukwa.
Alisema lilipofika Mzaganza, behewa moja la nyuma liliyumba na kufuatiwa na lenye abiria na yote kupinduka na kusababisha vifo hivyo na majeruhi hao waliokuwa wakitoka mnadani.
Kamanda Msigwa aliwataja waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni wafanyabiashara Said Pindupindu, Seif Bakari, Nassoro Mohamed, Jonas Lukanda, Abbas Kandaro; wote kutoka Wilaya ya Kilosa na mwingine mmoja ambaye jina lake halijatambuliwa.
Aliwataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo na kulazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa ni Hamisi Chamwitu, Seleman Mohamed, Sadik Monera, Esther Mbwambo na Asha Hamis wakazi wa Morogoro.
Wengine waliolazwa katika hospitali hiyo ni Edward Athanas, Aziz Seleman wote wa Dar es Salaam; Hamis Manyeleta, Hamis Selemani na Mecha Jackson wa Kilosa. Kamanda alisema marehemu wamehifadhiwa katika mochari ya Hospitali ya Kilosa.
Alisema kazi ya kutambua miili hiyo ilikuwa ikiendelea na hadi jana mchana, maiti watano kati ya sita walikuwa wameshatambuliwa na ndugu zao na majeruhi wanaendelea vizuri.
Chanzo:
Kwa kweli tumejaribu sana kuchangia maada hii ya ajali zinazoendelea kutokea Tanzania. Kwa nini Lowassa alijiuzuru na waziri anayehusika na wizara ambayo ajali zinatokea asijiuzuru? au hata mkuu wa Usalama barabarani asijiuzuru? Ninachotaka kusema hapa ni kwamba madaraka sio kutembelea tu magari ya serikali, na kula good time. Ajali zimeshatokea nyingi na ilitakiwa wahusika wakune vichwa na kutafuta njia ya kujaribu kupunguza ajali au hata kuzuia zisitokee kabisa mbeleni. Kwa mfano bodi ya mikopo imetangaza kuongeza madaraja ya kutoa mikopo na kuondoa ubaguzi wa daraja la kwanza na la pili kupata mikopo na pia watatoa mikopo asilimia mia moja kwa baadhi ya program kutokana na kipaumbele cha serikali. Sina maana kwamba wako sahihi ila ni kwamba wamekaa chini na kutafakari na kubuni kitu fulani ambacho watakitumia na kuona kama hakitapelekea kuendeleza migomo ya wanafunzi kuhusu mikopo. Lakini wizara na idara inayoshughulikia masuala ya Usalama barabarani imekaa kimya tu. Tunasikia pole tu kutoka kwa Mh.Rais. Sasa kwa nini wasijiuzulu na kuacha wengine ambao wanaweza kukuna vichwa wasiingie madarakani? Ni hayo tu, tumechoshwa na hili gonjwa AJALI bora hata ukimwi kuna condom na madawa ya kupunguza makali.
ReplyDeleteNi mimi mkereketwa...
swadakta anon wa kwanza,idara ya usalama barabarani jeshi la polisi(trafiki)naona liwajibike,mamlaka ya kutoa leseni za kuendeshea vyombo vya moto imepigwa sindano ya usingizi???yaani kula kodi zetu kifisadi hamjatosheka tu bado na kutuangamiza mnaendelea??kusema ukweli katika vitu ambavyo nina vilaani kwa nguvu zangu zote ni SERIKALI YETU YA TANZANIA YA CCM ILIOPO MADARAKANI,NI SERIKALI ILIOJAA VIONGOZI SELFISH NA WABABAISHAJI WAKUBWA SANA HAIPO MAKINI HATA KIDOGO WAAMBIE KUNG`NGA´NIA MADARAKA TU.KILASIKU NIMEKUWA NAJIULIZA "TUMEMKOSEA NINI MUNGU SIE HADI TUKAPATA SERIKALI MBOVU KAMA HII"
ReplyDeleteSHINDWAA ILI ROHO YA AJALI,,,
ReplyDelete