JK na balozi wa china nchini Mhe. Liu Xinsheng wakiangalia mchoro wa jengo linalotarajiwa kujengwa jijini dar litalojulikana kama julius nyerere convetion center wakati walipokutana ikulu
mchoro wa jengo la julius nyerere convention center linavyoonekana kwa ndani
kwa nje



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 57 mpaka sasa

  1. haya ndio tunaolipa Kodi tunakasirikia mambo ya ufisadi hii nchi tumeipigia kura sio serikali watufanyie kitu ni wananchi tuifanyie kitu serikali tunaifanyia mengi ila wanatugeuka. Vitu vya kufunguliwa Tanzania ni viwanda hasa mikoani si haya majumba ya kifisadi ya mikutano bwana mikutano yenyewe kila siku sign tu kinachoendelea hakionekani. Wananchi wakiona majumba wanaanza mmeona Dar-es-salaam kama New york kama New York vipi mijumba tu imesimama kinachoendelea kikazi hakuna. Fungueni ma viwanda na ma office yenye maelekeo kwa wananchi wa watanzania na East africa kwa pamoja.

    ReplyDelete
  2. Ingekuwa vyema sana majengo haya yakajengwa pembezoni mwa mji wa D'salaam hii itasaidia kupunguza mlundikano wa watu katikati ya mji na usumbufu wa usafiri nyakati za asbh na jioni.
    Kibamba au Kigamboni au mbweni kunahitaji kujengwa majengo ya namna hii.Tukusudie hivyo Mr Michuzi na kwakuwa wahusika wanafuatilia Blog yako basi taarifa imefika.

    ReplyDelete
  3. Mkuu misupu, ni wazo zuri sana hasa ukizingatia gharama ambayo nchi imekuwa ikiingia pale kunapokuwa na mikutano mikubwa ya Kitaifa na Kimataifa. Lakini ingependeza sana kama design ingezingatia ukumbi kuwa multipurpose nikimaanisha uweze kutoa fursa kwa shughuli za burudani pia.

    Tumeshuhudia jinsi ambavyo tamasha (concert) mbalimbali zinavyokosa mvuto kwa kuandaliwa kwenye kumbi zisizo na sifa kama vile Miss Tanzania kufanyika Leaders-club. Nilidhani Serikali ingeliangalia hili maana yaweza kuwa chanzo kizuri cha mapato na pia huduma kwa wananchi wake. Juzi JK aliwaahidi wasanii push toka serikalini, nadhani kuwajengea ukumbi wa kisasa ingechangia kuinua sanaa ya Tanzania kwa kiasi kikubwa sana.

    Ni hayo tu mkuu,
    Johnshaaban.

    ReplyDelete
  4. MASWALI LA MSINGI SANA,FAFANUZI?:
    1.ivi kwanini mnafupisha jina la mwalimu???KAMBARAGE liko wapi?mbona serikali mna akili nzito ivi wageni ndo wanatuamulia watamkeje?mboni wezetu ao majina ya viongozi wao magumu ata kuandika wanayaenzi.
    sielewi kabisa ktk hili,mnaboa sana
    2.dar mnalijenga wapi hili looote jengo??city centre tena au nje ya mji,kibamba,kibaha bunju nk.msitubane tena apa mjini jamen mana dar hakuna hewa asili tena na viyoyozi tu.
    bullshit

    ReplyDelete
  5. Hii ndiyo tanzania yetu bana.Tunajenga nchi yetu kwa kufaidisha wageni.Nina imani kabisa kuna wabongo waliokwenda shule wenye uwezo wa kubuni,kuchora na kujenga jengo kama hili.Lakini cha ajabu dili limepelekwa kwa wachina.Hapa wabongo watakuwa wapiga zege,watandika nondo na waosha tools.Makandarasi wote watakuwa Machinki.Kina MANKA na wenzake waliosemea akiteki wanahaha kutafuta ajira/dili kama hizi lakini machinki wa aina zote wanakuja kusunda pesa zetu na kutimua.
    Mgeni karibu bongo ufaidike.Nasema karibu sana bongo.

    ReplyDelete
  6. michuzi sijui umekuwaje siku hizi! Taharifa zako ni fupifuuuupui kha!

    ReplyDelete
  7. Safi Sana wenzetu wa China, Whats the difference btn "Center" and "Centre" mai inglishi izi noti richabo Misupu, Thenksi!!

    ReplyDelete
  8. KWANINI WACHINA WATUJENGEE MAJENGO YETU? SISI TUMEKUWA WAFALME KAMA WAARABU WENYE MAFUTA? HII INAOUA LOCAL BUILDING INDUSTRY.

    ReplyDelete
  9. KWANINI WACHINA WATUJENGEE MAJENGO YETU? SISI TUMEKUWA WAFALME KAMA WAARABU WENYE MAFUTA? HII INAOUA LOCAL BUILDING INDUSTRY.

    ReplyDelete
  10. liwekwe nje ya jiji kidogo basi sio mnarundika kila kitu katikati ya jiji mosongamano utazidi kuwa mkubwa.
    NISAMEHE US BLOGGER KWA MAONI YANGU KAMA SERIKALI TAYARI INAMPANGO WA KUFANYA HIVYO LOL.
    mdau "cha mtu mavi"

    ReplyDelete
  11. Kila kitu kinaitwa NYERERE aah this is too much now, Sabasaba sasa unaitwa NYERERE, Barabara NYERERE road, Uwanja wa ndege wa DSM nao NYERERE na shule zinazotumia jina hilo ndiyo kibao na huo Mjengo nao Utaitwa NYERERE nahisi itafika wakati watu watapotea maana ataambiwa aende sehemu fulani ye ataenda nyingine sababu ya kufanana Majina.
    Mi naona now is too much

    ReplyDelete
  12. MKUU WA WILAYA NAKUOMBA UWENDE KWA MHESHIMIWA RAIS UKATUOMBEE SISI WATU WA TANGA HILO JUMBA LA MIKUTANO LIJE LIJENGWE KWETU.

    ReplyDelete
  13. MKUU WA WILAYA NAKUOMBA UWENDE KWA MHESHIMIWA RAIS UKATUOMBEE SISI WATU WA TANGA HILO JUMBA LA MIKUTANO LIJE LIJENGWE KWETU.

    ReplyDelete
  14. kumbi za mikutano tanzania zipo. jengo hili litagharimu mamilioni. kama ni kuweka kitu kwa kumbukumbu ya nyerere (nadhani zipo tayari za kutosha) kwa nini kusijengwe vitu vya kujivunia tanzania? kama apatikanaji wa maji safi vijijini na mijini, umeme wa uhakika, what about shule na college zenye vifaa vya kisasa na kamili kwa ajili ya kuelimisha vizazi vijavyo? au vipi hospitali za kisasa? kila siku watu tunapiga harambee kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa sababu tanzania hatuna uwezo au vifaa vya kufanyia matibabu. nyerere kapigania nchi hii ili mtanzania awe na maisha bora, majengo hayatasaidia kitu, elimu, maji safi, mazingira bora, huduma bora za afya haya ndio ya kuzingatiwa na kuoiganiwa nchini tanzania.

    ReplyDelete
  15. alouliza tafauti ya centre na center ni kuwa kuna tafuti ya spelling baina ya us english na uk english, kuna maneno mengi tu yanaandikwa tafauti baina ya nchi hizi.

    ReplyDelete
  16. Aliyesema kila kitu nyerere ni kweli ila mie namuunga mkuno wa mwanzo tujenge viwanda jamani na kama majengo kama haya tujaribu kupunguza foleni jengeni nje ya mji wa DSM. na mwengine na muunga mkono tujaribu na sie kutafuta WACHORAJI wenu tusiwasubiri WACHINA hawa WACHINA wanaingia kwa GIA zao tu ili waje kufanya mambo yao nchini tuwe makini jamani misaada ya bure tutaumia. tufanye wenyewe na ma Office yaanze kujengwa nje ya mji kupunguza foleni kwani kazi zitaenda tu si fax na mail tu mawasiliano si ndio muhimu? jengeni viwanda sasa ndio tutawaona mnawajali wananchi wenu wa chini. Mdau Songea

    ReplyDelete
  17. aaa..aaa ndoto za mchana zinaanza kama ifuatavyo..


    SERIKALI YA CHAMA TAWALA CCM BADO INA DHAMIRA YA KUAMIA DODOMA..

    kwa mjengo huu nakubaliana nao si unaona kitu kinaenda kujengwa Dodoma..

    Dude kama hili lingepelekwa kusini mwa nchi yetu lazima lingesaidia kunyanyuka huko au lingepelekwa singida,shinyanga au Kagera etc kila kitu dar

    tutafika tu

    ReplyDelete
  18. Mtanzania haimsaidii kitu kuwa na majumba kama haya, mtanzania kwa wakati baada ya mika 47 ya uhuru hahitaji ufahari wa majumba.
    Kama mtanzania kwa wakati huu ufahari ninao uhitaji ni:-
    1.elimu bora
    2. huduma bora za afya
    3. huduma za mawasiliano za kuaminika.
    4. usafiri wa uhakika wa baharini, angani na ardhini hususan treni.
    5. Ajira njenje
    6. usalama wa mali zetu na maisha
    yetu
    7. majengo bora ya shule na college
    8. hudumu bora kwa wazee wasiojiweza
    9. maji safi nchini kote tanzania
    10. umeme wa kuaminika

    ReplyDelete
  19. Mdau uliyeuliza tofauti ya center na centre zote zinamaana Moja lakini CENTER NI AMERICAN ENGLISH NA CENTRE NI BRITISH ENGLISH, source:-

    1: http://dictionary.reference.com/browse/centre

    2: http://dictionary.reference.com/browse/center

    so usichanganyikiwe na tafsiri...

    Pili naunga mkono mdau wa kwanza kusema kwamba Badala ya kujenga majengo ya kifisadi kwanini pesa hizo zisiwekezwe kwenye maswala ya muhim kama Hospitali na viwanda ili kuongeza waajiriwa na hiyo itasababisha mzunguko wa pesa kuwa mkubwa kwa masikini na wasio na ajira... Naamini ukifanya jitihada watu wa hali ya chini kuwa na pesa za kutumia uchumi unakua sana kwasababu watazitumia kuinua sekta nyingine muhim kama uzalishaji, masoko tiba nk... maskini wakinunua samani, mbao itauzwa zaidi, na maseremala watapata pesa, wakijenga nyumba viwanda vya sementi vitainuka zaidi kwani watazidisha uzalishaji, wakiumwa wataweza kujilipia matibabu na madaktari na wauguzi watapata kula yao na wauza madawa wataendelea... lakini pesa ikiwa kwa wachache wa juu wanaweka benki riba inakwenda ulaya...na matumboni mwa wachache...

    Tatu, hivi nchi haina wasomi mpaka kila tenda iwe chini ya wachina??? (barabara, majumba, madaraja nk) Ajira zinaenda kwa wageni na wazawa wanabaki kuwa wabeba zege tu..?? aibu jamani hii...Au ndio misaada tunayopewa na wachina masharti yake ndio haya tuwape tenda za kutujengea nk..?? mmh... ! i dont think so lakini ndio kama inaelekea kuwa hivyo...

    All the best.

    ReplyDelete
  20. serikali ingefanya la maana wangejenga maviwanda watu wakapata ajira, ndio maana ujambazi na wizi unazidi nchini kwetu kwa sababu watu hawana ajira, mimi sisaport hilo banda la mikutano kwani wananhi waliokuwa hawana ajira haitawasaidia zaidi ya ufisadi tu utakaofanyika kwenye hivyo vikao, wala sifurahii, kuna viwanda vingi tu kwetu hamna wangevumbua nini cha kufanya mnapendezesha jiji wakati wenye mji wanahangaika its not fair

    ReplyDelete
  21. Jengo ni wazo bora kw a Dar mji mkubwa usio na ukumbi wenye hadhi inayofanana na jiji. Hata hivyo ingefaa pawe na nafasi ya kundeleza kwa kwenda juu - ghorofa; hata huko baadae, kwani kwani kutumia ardhi yote hiyo bila nafasi ya kwenda juu katika hali ya dar kiuchumi sio muafaka. Natumai pia kwamba chini kuna nafsi za kuegesha magari. Hongera

    ReplyDelete
  22. Tanzani kuna adui njaa, adui malaria, maskuli hayana zana za kusomeshea, mahospitali hakuna vitanda wala zana za upasuaji seuze madawa, umeme ni wa mapande mapande, maji safi hakuna, usafiri ni mbovu, mkulima hana zana za kuhimili kazi yake. badala ya kutumia pesa zote hizo kunufaisha watanzania wengi tunajenga jengo ambalo watanzania wengi hadi tunakufa hatutoingiza mguu, kumbukumbu gani hiyo kwa mwalimu? jengeni miradi ya kumsaidia mtanzania kuinua maisha yake. tunahitaji ajira, tunahitaji kuondowa umasikini, hatutofanikiwa kwa kuwa na jengo la mikutano lakini tutafanikiwa kama tuki invest katika kuelimisha jamii na kuipa umbele teknolojia.

    ReplyDelete
  23. huko ndo mavijisent yatatumika bila mpangilio hata mbeba kokoto atanunua bmw kama kawaida ya inch yetu.sisi tunataka maendelo ya inch na sio lijumba linalo tumika kwa mwaka mala moja.

    ReplyDelete
  24. Mimi nimefurahishwa sana na hili...mpaka leo hii jamani nchi yetu miaka 40 na tangu uhuru hakuna ukumbi wa mikutano wa maana...
    Sasa tunaomba wafikirie na kujenga maana sio kukarabati airport yetu.Jamani airort ukifika tabu ukiondoka tabu...hivi kweli airport escalator moja saa nyingine mtu unakua umechoka na safari mizigo mingi inakubidi kupandisha ngazi.
    Vyoo vya airport jamani...vinanuka mikojo sana...South Africa tu pale Oliver Tambo airport kubwa na wanainvest na biashara kibao na bado wanaikarabati,same as cape town.Sitaki kuikandya nchi yangu lakini kama wao wanaweza kwa nini sisi tushindwe,saa zingine ukiwa unarudi wale watalii wanauliza what should I expect from Tanzania....huna hata cha kusema...zaidi ya Mt.kilimanjaro,zanzibar,serengeti..

    ReplyDelete
  25. Acheni longolongo wabongo kwanza inabidi mjisikie aibu kwa jiji kama Dar kutokuwa na facilities kama hiyo. Huo ukumbi unapaswa kujengwa Kigamboni uende sambamba na daraja na hotels (e.g. Golf Resorts)na ofisi kwisha. Mambo ya Mbezi, mbweni sidhani kama ni convinient

    ReplyDelete
  26. Swala la ukumbi wa concerts nathani sekta binafsi inaweza kuuungana pamoja na kujenga sehemu yenye makaburi ya Wailes inaweza kutumika kama walendugu zetu walilala pale watahamishwa na ni strategic spot wenyenazo waangalie hilo

    ReplyDelete
  27. Je, lilikuwa ni moja ya mipango ya bajeti ya sijui mwaka gani?

    Katika hotuba yake ya Des 30 Ddodma hakusema tutajenga jengo hilo!

    Haya mawazo ya ki-zimamoto ndio maana bajeti yetu inakwenda kombo!

    Hapo kuna kitu cha kawaida kama 10-15% kwa atakayetia saini malipo.

    Mchina akikataa, mtia saini atasema ongeza hizo zangu kwa gharama ya malipo...walipakodi watanipa tu!

    ReplyDelete
  28. KAKA MISUPU ILO JUMBA LA KIFAHALI KIKWETE AKATUWEKE KIGAMBONI,LITAPENDEZA SANAAAAAA,NAMAANISHA KIGAMBONI KUNA NAFASI NA LIWEKWE KAMA IKULU YETU ILIVYOJENGWA,YANI PEMBEZONI MWA UFUKWE WA BAHARI YA HINDI!KIGAMBONI SI MCHEZO,NI PAZURI SANA,KULE NDO LIWE JIJI!KIKWETE NAAMINI ANAWEZA KUIFANYA DAR IWE KAMA NY CITY,JIJI LA GHALAMA KWA WAFANYA BIASHARA!

    ReplyDelete
  29. Ama kweli wajinga ndio wali wao.Majumba makubwa kama hayo yawekwe mahali kama Arusha ili wageni wakija kuyaona wanavutiwa na kwenda kwenye mbuga za wanyama na kuona desturi za asili kama za kimasai na kufanya watu wa sehemu hizo kupata kipato.Kujenga Dar ni sawasawa na kufungua Ukumbi mpya wa mavituz.Lakini kwa ufasaha zaidi ingekuwa bora kama hawa Wachin wangechora michoro na kujenga Shule, Hospital na Training school na kama haiwezekani basi hata kiwanda kimoja ili watu wapate ajira.Hatuna pesa na Uchumi ni mgumu kwa sasa kwa hiyo tutumie vizuri pesa tulizonazo kwa kuwapatia ajira wabongo.

    ReplyDelete
  30. At least sasa Dar es Salaam kwa mara ya kwanza itapata ukumbi wa mikutano wa ,aana na kisasa kabisa.

    Wadau ambao wanapinga ukumbi wa mikutano usijengwe, hao nadhani hawako sahihi kwani ujenzi wa ukumbi huo utaajiri watanzania. Pili, mikutano ni sehemu ya utalii, ni vyema tukawa na ukumbi ambao utaweza ku-host mikutano mikubwa ya kimataifa. Tanzania itafaidika kwa kwa kuandaa mikutano hiyo katika njia mbalimbali. Kwa mfano nakumbuka wakati wa Mkutano wa Ukimwi Dunia uliofanyika Kampala Uganda ambao ulihudhuriwa na washiriki wapatao 2,000 waganda walifaidika na mapato ya yokanayo na malazi, usafiri, chakula nk. Hapa kwetu nadhani wale waliokuwa Arusha wakati wa Mkutano wa Sullivan wanaweza kutueleza faida za kuwa na kumbi za mikutano.

    ReplyDelete
  31. Kwani lazima upewe jina la kiongozi ndio uonekane uko patriotic? Kwani wakisema Dar Es Salaam Konvenshen Centre kuna nini? Na halaf pia unajemgwa wapi? Kariakoo,Posta,Ubungo,Mwenge,Mbagala ama wapi? Tushachoka foleni na mlundikano..!!Wakajenge huko Tegeta Au Mbezi Kuu Au Mbagala japo hakujakaa kikazi za ofisi ofisi ila watafute sehemu nyingine not huku mjini...

    ReplyDelete
  32. Ni kweli inauma kuona elimu ya wabongo haitumiwi katika miradi kama hii,lakini mkumbuke kwamba kuna masharti yanayotolewa kabla ya mkataba.
    Si mnakumbuka uwanja mpya wa taifa?
    China walichangia kiasi fulani cha pesa lakini kwa masharti kuwa wataleta kampuni yao ya ujenzi.Kwa hiyo si ajabu kuwa hapa mbinu ni ile ile.
    Angalia ujenzi wa barabara na misaada ya Japan,it is always KONOIKE au KAJIMA;Sweden na SKANSKA JENSEN!
    Anyway,tusubiri data zaidi.

    ReplyDelete
  33. ~~~~ Kipaumbele ~~~~
    Tungetoa kipaumbele kwa elimu. USDM na IFM vina shida ya kumbi za mihadhara na semina. Maktaba zao zina upungufu wa nafasi za kusomea.


    Mijengo kama hii ingetatua shida au kero. Kumbi za mikutano zimejaa. Kukia na halaiki tutenda Nesho, Ngurudto AICC nk. tayari kuna kumbi Royal Palm, Kempiski na pale DICC (PPF).

    ReplyDelete
  34. Point kweli hizi uliyosema haya ya chini.

    1.elimu bora
    2. huduma bora za afya
    3. huduma za mawasiliano za kuaminika.
    4. usafiri wa uhakika wa baharini, angani na ardhini hususan treni.
    5. Ajira njenje
    6. usalama wa mali zetu na maisha
    yetu
    7. majengo bora ya shule na college
    8. hudumu bora kwa wazee wasiojiweza
    9. maji safi nchini kote tanzania
    10. umeme wa kuaminika

    Kukutania mikutano kokote pale hata hall liwebaya si vibaya muhimu hayo juu tu. tuanze kuwatumia wasomi wetu sasa sio kusubiri kufanyiwa au kupewa pesa kula baada kusaidia mahitaji wanaohitaji. Wabunge kama mnaona Comment za wadau kaziongeleeni Mbunge wetu Issa michuzi fikisha ujumbe.

    ReplyDelete
  35. Nimeona watu wengi wameilaumu serikali kujega hilo jengo, jina la nyerere kutumika mara nyingi na pia wqachina kufanya hiyo kazi ya ujenzi. Kama kumbukumbu zangu bado ziko sahihi, nakumbuka niliwahi kusikia kupitia serikali ya kwamba hilo jengo litagharamiwa na wachina wenyewe kama msaada kwa Tanzania (bure siyo mkopo)na kama njia ya kumenzi mwalimu. Nadhani kama ndivyo hivyo basi hakuna haja ya kulalamika kwa nini tunaongeza kumbi za mikutano badala ya viwanda na kwa nini wachina ndiyo wachore ramani pamoja na kujenga. Mwenye pesa ndiyo ameamua nini afanye na nani afanye. Kama maelezo yangu siyo sahihi, wadau mnaweza kuongezea mnayoyajua kuhusu nani anagharamia huu ujenzi. Hongera china kwa msaada wenu.

    ReplyDelete
  36. kwa mawazo yangu ikiwa unajengwa gani mjini ni upuuzi mtupu. angalau wangeujenga mbagala, au hata morogoro. kama ni hapo downtown barabara za kuhost mikutano ya kimataifa ziko wapi?

    Pili ni wachina tu ndio wanajua kujenga. elimu ya mlimani na chuo cha ardhi inafanya nini ? Hatuna makampuni ya kujenga siye wenyewe mpaka wakachukue tu wachina? Halafu mnalalamika wasomi wakitoroka nchi na kuzamia nchi za nje kuosha vibibi na elimu zao.

    It is sad kwa vile mimi sikusoma chuo kikuu bongo lakini ninajua watu wenye degree ya udactari, cpa ya chuo cha njiro etc wamekuja huku baada ya elimu na wanafanya kazi kwa nursing home na nyumba za matahira. I know kazi ni kazi lakini just imagine elimu yote waliyonayo hawaitumii ipasavyo

    ReplyDelete
  37. Kweli, kama kweli Dodoma ni makao makuu ya serikali kwa nini hili jengo lsijengewe huko? Dar pamejaa!! Mlundikano uliopo sasa hivi ni mkubwa sana sijui viongozi wanafikiria wapi????

    ReplyDelete
  38. Nyie mnataja mbagala au wengine wanasema Mtwara na Lingi au Morogoro sithani kama mnafikiria juu ya infrastructure zilizoko huko ukumbi kama huu unahitaji hotels pia tena 4-5 stars imagine kuna AU summit maraisi wa nchi 53 za Afrika wanakuja utampeleka nani Mbagala? huko Mbagala kwanza ni slum pili hakuna usalama Mbwa Mwitu kila mahali huu ukumbi ujengwe Kigamboni. waweke daraja na kwa vile Kempinski washanunua ardhi huko watajenga Hotel na za mjini pia zitatumika kipindi cha mikutano

    ReplyDelete
  39. Hiv ninyi mnaotaka wasomi wtu wajenge hilo jumba la mikutano mnafikiria sawasawa kweli? Mimi ninataka mnijajie nani wa kufanya kazi hiyo, msomi gani?
    Kama wao wanauwezo wanashindwa nini hata kubuni baskeli?
    Tusofananishe China na Tanzania. Siku za nyuma tulikuwa tunapewa misaada ya kutengeneza barabara na kuwapa wazalendo watengeneze, matokeo yake tulitengeneza tope barabarani badala ya barabara. Mwisho wafadhili wakasema basi tutawasaidia lakini tutaleta makampuni yetu yafanye kazi. Na kweli walau tumeona sasa barabara mbalimbali nchini zimejengwa kwa kiwango cha lami.
    Hebu fikiria barabara ya Chalinze-Segera-Tanga tungempa mzalendo ingekuwaje kama siyo balaa? Hao wazalendo mnaowataka wanashindwa kutunza soko la samaki la ferry? aibu iliyoje. Yule mkandarasi mtanzania aliyepewa barabara ya kujenga huko kusini nadhani Minjingu (naweza kusahihishwa) barabara hajengi na pesa ameshaT#*%#...
    Kuhusu hilo jengo wachina wanatoa pesa yao wenyewe hakuna pesa ya bajeti ya serikali wala nini. Angependa hiyo kazi ifabnywe bna makampuni ya kitanzania, lakini hakuna ambaye anaweza kufikia ujenzi wa kiwango cha juu kama wao waliotoa msaada.
    Juzi-juzi hata kumbukumbu hazijafutika wataalam wa kizalendo wamejenga jumba hapo kisutu limeanguka na ninasikia kuna jingine liko upande. Jengo linajengwa la ghorofa kumi zege inapandishwa kwa karai, jamani tusitaniane kabisa kwenye mambo serious.
    Bottom line Dar es Salaam inahiitaji ukumbi wa mikutano ambao hauna. Msifananishe ile parking lot ya pale PPF Tower eti ni ukumbi wa mikutano, No, Diamond Jubilee haiko kwenye standard kwa mikutano hata ya EAC. Mnakumbuka wakati wa SADC aibu tuliyoipata.
    Kumbi nyingi za Dar ni nzuri kwa sherehe za harusi tu na wala siyo mikutano kwa maana ya mikutano mikubwa ya kimataifa.

    ReplyDelete
  40. Watu manalalamika tu hapa. Kabla mtu hujampa mradi mkubwa inabidi umpe mradimdogo aonywenye kama anaweza kazi. Miradi waliopewa wazalendo ni upuuzi mpu. Wewe utajengaje barabara ya lami leo na baada ya miezi 3 inaanza kubanduka hapa kabla magari hayajaanza kupita. Wizi tu umejaa watu wanaiba hadi kokoto wanaweka mchanga. Kama kuna mtu hapa ambaye atanipa angalau mradi mmoja waliopewa wazalendo na ukafanikiwa kwa ufanisi nitafuta kauli yangu.

    ReplyDelete
  41. Issa,

    Washauri hao watu wako (Serikali) maana na wewe wamekuweka kwenye kamtandao kao kuwa Jengo kama hilo lijengwe pembezoni mwa mji na kama wame-upgrade barabara ya Banana-Ukonga hadi Mbezi Lous kuwa Main Road basi wajenge huo mjengo maeneo ya Kinyerezi, Kibamba au Kibaha !!!!

    Ila walivyo utasikia wanajenfa katikati ya Jiji au kuelekea Bagamoyo !!!! Dar es Salaam Mpya itapatikana vipi kama wataendelea kujenga majengo mazuri katikati ?

    Issa waambie wenzako hao si unakaa nao meza moja ?

    Blogger (a KOP)

    ReplyDelete
  42. Kwa wote mliotuma mawazo yenu, kwa kuwafahamisha:
    Jengo hilo hatulipii hata senti, ni "zawadi" toka kwa Serikali ya China, na wameamua wenyewe kujenga ukumbi ambao utamuenzi rafiki yao na baba wa taifa letu JK Nyerere.Huu ndio mkakati mpya wa China kwa nchi za Afrika kuliteka kiuchumi bara letu. Wamefanya mambo kama haya kwa nchi nyingine za Africa kujenga majengo, kutoa misaada mikubwa, na nchi za ulaya zimeanza kuilalamikia China kuwa inatafuta kujiimarisha katika bara la Afrika kwa kutoa rushwa. Kwa vile wanajenga wao, wanalipia wao na wameamua kuchagua jina na mahala wanapotaka kuonyesha "upendo" wao kwa waTanzania.
    Kwa wanabeza jina la JK Nyerere kuwekwa kila mahali, ni watu wasiojali historia ya nchi yetu. Tembelea USA, kuna barabara 14zenye jina George Bush, 32 za Ronald Reagan,na vivutio zaidi ya 100 vinavyomhusu George Washington rais wao wa kwanza, ukienda China Mao yupo kila mahali, ukienda Uingereza malkia yuko kila kona ukija South Africa, Mandela ameanza kuonekana kila kona, hakuna dhambi kumuenzi Nyerere hata mara 100 kwani tangu ameondoka hakuna rais anayeweza kulinganishwa naye japo kwa sehemu.

    ReplyDelete
  43. Maoni yote ya wadau yamegusa CCM, Nyerere na nini kinachihitajika haraka nchini kwa maendeleo ya baadae. Hamna hata mmoja aliyegusa swala la Wachina kutupa fedha Afrika. Wanataka kura zetu Umoja wa Mataifa. Pia wanataka madini yetu ili waendelee kujijenga, uchumi wao unakua kuliko wote duniani na nchi bado inahitaji madini hata ardhi. Korea kusini amenunua ardhi madagascar ili ilime na kuchukua chakula kwao. Wachina wanashindana na Brazil na India kutafuta madini, vyuma na kadhalika, huu sio urafiki wa upande mmoja tu bila masilahi, sasa hivi wanatupa hela kama takataka Afrika ili wawe marafiki na Afrika na wafanyabiashara wao wapewe kazi za ujenzi (Konoike wa Japa yupo bongo miaka 20) na kupewa leseni kirahisi kwa kutumia urafiki huu wa kujenga majengo mawili matatu kwa kila nchi za kimasikini. Pia wanajua baadae tutanunua magari yao, kompyuta zao na vifaa vya ujenzi na kijeshi. Tutawasaidia pia kupinga mada ambazo hawazipendi Umoja wa Mataifa kama haki za binadamu, uhuru wa Tibet na Swala la Taiwan.
    Hii yote ni siasa sio urafiki. Wana trillion moja dola katika benki yao, yaani bilioni 1000, sambamba na Japani, kutoa milioni 20 au 50 sio kitu kwao.

    ReplyDelete
  44. We unaesema kila kitu ni nyerere unataka iweje,au wakuweke wewe?Watu wanaangalia mtu na reputation yake ndani na nje ya nchi.Wengi pamoja na Wachina wanamtambua nyerere sio hao unaowataka wewe.
    nahisi kuna msaada fulani hapo toka china ndo maana wanafanya hiyo kazi

    ReplyDelete
  45. We unaesema kila kitu ni nyerere unataka iweje,au wakuweke wewe?Watu wanaangalia mtu na reputation yake ndani na nje ya nchi.Wengi pamoja na Wachina wanamtambua nyerere sio hao unaowataka wewe.
    nahisi kuna msaada fulani hapo toka china ndo maana wanafanya hiyo kazi

    ReplyDelete
  46. Sasa jengo hilo la JK Nyerere litajengwa mtaa gani ?

    ReplyDelete
  47. Mimi ningependa kuwekeza pesa zangu kwenye huo mradi wa ukumbi.

    Je ni mradi ambao unahitaji wabia? Niwekeze hela zangu kwa kununua hisa hapo?

    Naomba msaada kwa mwenye taarifa zaidi.

    ReplyDelete
  48. Afadhali na Dar kuwe na conversion center sio Arusha tu. . . jamani nikitaka kutoa tangazo kwenye hii blog nafanyaje kaka Michuzi? sina outlook inashindikana kutuma email

    ReplyDelete
  49. CENTRE NI CENTER KAMA ILIVYO THEATRE NA THEATER, PIA COROUL NA COLOR ZOTE NI SAHIHI KIINGEREZA CHA MAREKANI NA UINGEREZA

    ReplyDelete
  50. nyie mnaosema tunajengewa "bure kwa urafiki" nyie kina nani kwanza?
    watu mlio karibu na serikali ktk mradi huu,au nani kaawaambia ni bure tamko katoa nani ilo kupitia serikalini??
    mana hatujawai kusikia katika bajeti yoyote ya bunge.sijasoma magazines siku nyingi,imeandikwa gazeti gani la lini?

    ReplyDelete
  51. 1. Nani anaegharamia ujenzi?
    2. Kama ni Mchina kwa nini? Anatupenda sana au ???!! MMhh!!
    3. Utajengwa wapi??
    4. What is the business case for center?
    5. Je iko wapi Cost-benefit analysis ya hiyo center? Maana ukimuomba mchina atakujengea ili mradi anapata free access kwenye raslimali fulani au amwage watu wake bongo. Hakuna bure siku hizi. Kawaulize Zambia, DRC
    6. Huo mchoro zaidi ya kuwa Jengo una manzari gani ya Kitanzania? Naunga mkono kabisa wanaouliza ni kwa nini wabongo wasipewe tenda ya kubuni mchoro huo??
    7. Nani atajenga?? Obviously ni mchina je asilimia ngapi lazima ijengwe na macontractor wa nyumbani?
    8. Je ni asilimia ngapi ya material lazima inunuliwe Tanzania??( Na sio kwenye maduka ya Import)

    ** Wanaosema tujenge viwanda wana maana viwanda vya kufanyia nini?? Maana ni rahisi kusema jenga kiwanda lakini inabidi utoe mfano ili uonyeshe nini unachokijua si kusema tu kiwanda. Pia nani ajenge? nani amiliki? nani aendeshe? Kizalishe nini? Kwa nini unaona kiwanda kinahitajika mahali hapo?

    Haya jamani
    Mungu iokoe Tanzania
    Mzawa

    ReplyDelete
  52. Miaka 20 iliopita nilisoma data za Tanzania, ukaonyesha ni nchi ya kimasikini sana. Nikasoma tena leo, mgonjwa bado hoi na waeleweke kama atapona.

    Watanzania tunajidai sana kama matajiri. Wachina na matajiri wengine wanatusaidia kila siku kwa kuwa ni masikini wa kutupa. Nenda kijijini utaona umasikini, usikae tu mjini. Watu wanateseka sana nchi hii. Tushukuru tunajengewa na Wachina, ho cost analysis sijui na maswala mingine yasubiri tukipata utajiri wenyewe. Hii sio pesa yetu.

    ReplyDelete
  53. Kwanini kila kitu 'Nyerere' jamani wabongo wenzangu?? Nakuunga mkono sana mdau uliyechangia hili mwanzo..It's too much sasa, we need to change, hata kama ni kumuenzi, hii inaonesha ukosaji wa ubunifu..Kuna unsung heros kibao wamefunikwa na hii kasumba ya 'Nyerere' kwa kila kinachojengwa bongo.

    ReplyDelete
  54. I think imekuwa tooo much na jina la nyerere sasa ,kila kitu ni nyerere, sawa tu mpa credit baba wa taifa na nafikiri its enough na jinahilo tayari airport,bara bara,uwanja vimeshaitwa nyerere,nafikiri pia ni vizuri serikali iangalie kutumia majina ya wazee wetu wengine pia ambao wamechangia mchango mkubwa kujenga taifa letu,we must remember nyerere hakufanya kazi yote peke yake,there were other people who helped him to get us where we at!

    ReplyDelete
  55. Ulaji mwingine huooooo, Sijui utabatizwa jina gani yarabi tusaidie waja wako twaangamia.

    ReplyDelete
  56. Huyu Anonymous wa Jan 23 saa 7.22am anakera kabisa. Hawa ndio wale wanaofikiri misaada ndio itatuendeleza. Ana mawazo ya yule chifu nimemsahau jina aliyepewa gagulo akasaini kutoa ardhi yake.
    Umejuaje wewe kwamba hawa wachina wanatujengea bure???!! Kwanza kwa mapenzi gani walionayo kwa Watanzania watujengee bure???!! Unafuatilia mambo wanayoyafanya huko Zambia, Kongo, Sudan na kwingineko???!!!

    Fungua macho ndugu yangu usije ukawa kama wale Nyerere aliosema wanabadilisha vipande vya Almasi wakapewa vipande vya chupa.
    Hakuna vya bure siku hizi na ukipenda vya bure angalia vizuri jijini hapa Darusalama???!!!
    Open your eyes and think for God sake!!!!
    Mzuwa

    ReplyDelete
  57. Anony 1:52 una pressure kali, huoni najaribu kusema nini, au huwezi kufikiri vizuri. Analytical skills zako ni ndogo sana.

    Mimi napinga sana kusaidiwa kila siku tangu uhuru, siamini kabisa kuwa hawa wachina wanatusaidia kwa kuwa wanatupenda au wanampenda Mwalimu. Wanataka mali zetu na Un support hasa JK sasa ni bosi wa AU, inasaidia kuwa rafiki yake kisiasa.

    Nilikuwa natoa maoni yangu kuhusu wadau hapa wanavyotaka kujua kiasi gani watanzania watapewa kazi, sijui cost analysis na kadhalika. Nasema sisi ni masikini, na huu ni msaada, lakini wadau hapa wanajidai kama vile Tanzania sio nchi masikini duniani inayotegemea misaada kuishi tangu uhuru. Hivi sasa tunadaiwa bilioni 8 tangu miaka 10 sasa au zaidi na bajeti yetu inategemea misaada ya nje kulipa gharama zetu. Wachina wamefilisi huko Zambia kama unavyosema lakini sisi tunachekelea walivyotujengea treni ya Tazara na uwanja wa Mpira. Tusijidai kabisa, hatuna tofauti na mgogo anayeomba samora ili aishi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...