ALIYEKUWA MKUU WA UTUMISHI NA UTAWALA WA BENKI KUU AMATUS JOACHIM LIYUMBA (KULIA) NA MENEJA MRADI WA BENKI HIYO DEIOGRATIUS DAWSON KWEKA WAKIWA K
MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI YA KISUTU MCHANA HUU KUJIBU MASHTAKA MATATU YA KUTUMIA OFISI VIBAYA NA KUSABABISHA HASARA YA DOLA 153,077,715.71 (SAWA NA MADAFU KAMA 221,197,299,20.95 HIVI) KATIKA UJENZI WA ZIADA WA BENKI KUU (TWIN TOWERS). WASHTAKIWA AMATUS JOACHIM LIYUMBA (NYUMA, SHATI LA BULUU) NA DEOGRATIUS DAWSON KWEKA, WAKIPELEKEWA MAHABUSU BAADA YA KUSOMEWA MASHTAKA YAO MCHA HUU KATIKA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI YA KISUTU DAR.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Bado mamalao

    ReplyDelete
  2. Bado wakubwa wa Uwanja wa Ndege wa Nyerere sasa tukitoka huko Tanesco.

    ReplyDelete
  3. Huo ni uonevu kwani walikuwa wapi? Nchi inamaliasili kibao mfisadi kibao lakini hakuna kinachoendelea.

    ReplyDelete
  4. tunaanza kwenda sawa sasa

    ReplyDelete
  5. ALUTA CONTINUA, ISIJE IKAWA LONGO LONGO TU.

    ReplyDelete
  6. Du!! hata EPA ni cha mtoto. Jamaa wamegawana USD 153,077,715 halafu tunamsumbua Rais kuwenda kutuombea misaada nje. Fedha tunazo tena za kutosha. Tatizo tunadekeza ufisadi kwa kile kinachoitwa 'rule of law', Watu kama hawa wanatakiwa kupigwa risasi hadharani ili kusafisha jamii na kuweka uadilifu. 'rule of law' baadaye, tukishawekana sawa.

    ReplyDelete
  7. MHESHIMIWA NAOMBA UPIGE MAHESABU UPYA, INAELEKEA HISABATI INAKOROFISHA KIDOGO.

    ReplyDelete
  8. Huyu si ndio yule bwana huko nyuma aiwahi kushtumiwa kuwanunulia wanawake wa Dar magari mekundu?

    ReplyDelete
  9. Huko BoT baado kazi nzito! Sio hao pekee. Wako maofisa wengi tu wanaishi kwenye mahekalu ya mamilioni Masaki, Mbezi, Obay na kwingineko!Wanaendesha magari ya kifahari, baba lake, mama lake, watoto na driver lao!!! Ukiiuliza eti ooh wamekopeshwa na BoT! Nani kawaambia BoT inaruhusiwa kukopesha fedha za walipa kodi ili watumishi wao waishi kama vile wako peponi wakati wadanganyika wanakufa kwa kukosa shs 500/- za kununulia wake zao gloves wakati wa kujifungua??!! Kwa niniwatumishi BoT waishi maisha ya juu kuliko sie wafanyakazi wengine wa Serikali? Kwani wao wanazalisha nini cha zaidi?? Fanyeni pia uchunguzi wa mali za wafanyakazi wengine wa BoT, mtajionea ya Firauni

    ReplyDelete
  10. HIO PESA ILOTUMIKA KUJENGA HILE MINAZI MIWILI HILINIMALIZA SANA.ALAFU WANATUPIGA MCHANGA WA MACHO KWAMBA HAWA NDIO WAMEHUSIKA KWENYE DILI? HA HA HA HA NAIPENDA NCHI YANGU LAKINI SIO SERIKALI YANGU.
    mda "cha mtu mavi"

    ReplyDelete
  11. SIKU HIZI KILA MTU NI HAKIMU.

    Itabidi tufungue mahakama binafsi ili tutoe ajira kwa wale mabingwa wa kutoa hukumu kabla ya kusikiliza kinachoendelea.

    Anon wa January 27, 2009 5:57 PM bado una mawazo ya "enzi za mwalimu"

    ReplyDelete
  12. Lazima tuwe na mahali pa kuanzia katika kupambana na ufisadi uliokithiri kwa watumishi wa UMMA na PA kuanzia ndiyo hapa. Nadhani kasi na ari hii ikiendelezwa kwa kipindi kirefu, wananchi tutaanza kuwaelewa viongozi wetu watakapo tuambia uchumi wa nchi yetu umekua na siyo uchumi kukua mifukoni mwa wafanyakazi wezi tu. Kazeni buti katika kuwasafisha mafisadi kwani wapo wengi sana katika taasisi na ofisi za serikali. MUNGU awalinde na awape ujasiri wa kuifanya hii kazi kwa uadilifu ili isije kuwa ule msemo ''SAFARI MOJA HUANZISHA NYINGINE''

    ReplyDelete
  13. SIO HAWA,,NI SEHEMU NDOGO SANA,,
    wamechukua kiduchuuuu kwa "kupitisha mafaili"
    ni basi tu tufanyeje tumeajiriwa yan ukiwa signatory ni ishu jamen..

    wapo wenyewe humo.Sikizeni kesi ya KAGODA hahahahaaaa nacheka kwa hasira kali sana ktk hili.
    Jehovah na ataingilia kati tuliomba sana na adi yule "mkubwa" wa mwisho atapohukumiwa

    ReplyDelete
  14. ndugu zetu wa kaskazini mwa tanzania hamkosekani katika kesi hizi;
    kina komu ,lema,kweka ,richmond,kiwira,wizara ya viwanda, fedha

    ReplyDelete
  15. MSHITAKIWA MWENYE TAI NI NDUGU NA TABU LEY?
    NAOMBA JIBU?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...