Katika StarTV hivi sasa kuna mchezo unaoitwa SETO ambao unamwezesha Mtanzania kujinyakulia MAPESA kibao kila siku. Mchezo huu unarushwa kila siku ifikapo saa 7:45 USIKU(Saa mbili Kasorobo) na huwa wa dakika kumi.
Ili kushiriki wadau wanatakiwa kutuma neno SETO kwenda 15777 na watapewa namba zao za kujisajili kuingia kwenye DRAW na ifikapo usiku namba hizo zitachezwa kwenye DRAW na mshindi kupigiwa simu. Imagine unaweza Ibuka na Zaidi ya Shs. 2Million kila siku unachotakiwa ni kutuma SMS nyingi kadri uwezavyo KUJISHINDIA. Mdau anaweza tuma Neno SETO wakati wowote hata mchana ili usiku namba yake ichezeshwe. Imagine na mwaka mpya huu Mdau ujishindie Milioni hizo si mambo yatakuwa mazuri?
Mchezo huu huendeshwa na kampuni ya Selcom Gaming ikutumia Television ya StarTV.

Mgori Juma Tumaini
Marketing Manager
Selcom Group Limited
P.O. Box 20656 Dar es Salaam, Tanzania
Tel: +255 22 212 5015
Fax: +255 22 211 4998
Mob: +255 787523152
Email: tumaini@selcomgroup.net

Jimmy Kabwe mzigoni
Ushindfwe wewe tu, anasema Jimmy Kabwe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Tanzanian man arrested with drug capsules in stomach aboard Ethiopian Airlines

    WIC

    More than 109 drug capsules were found in the stomach of a Tanzanian man who was traveling from Tanzania to China on the Ethiopian Airlines.


    Medical Director of Hayat hospital Dr. Behailu haile told WIC on Thursday that the individual was admitted to the hospital as he collapsed while aboard. Accordingly, bunches of capsules, containing around 15 grams drug each, were detected in the stomach of the individual, while he was diagnosis at the hospital. Dr. Behaylu said that the individual was unconscious while admitted to the hospital as some of the capsules were burst in his stomach. So far 109 capsules of drugs were taken out of the stomach of the individual with medical treatment, he added. The medical director also said that it is not possible to confirm whether the individual, who was unconscious for more than two days, would survive the accident or not. Federal Police Commission Crime and Forensic Investigation Main Department Head, Chief Inspector Asamnew Harka said on his part said that the department is investigating the matter to identify the type of the drug and the identity of the individual. Federal Police Crime Prevention and Control Main Department Deputy Head, Commander Tsegaye Woldehiwot also commented that the case was unique as the number of the capsules concealed in the stomach of the individual is very large.

    The Federal Police are making all efforts to prevent such cross border crimes, he said, and called on the public to stand with the side of police.

    24/10/2009 Addis Ababa

    ReplyDelete
  2. hii michezo inapigwa vita sana hapa ukerewe kutokana na kupanga matokeo pamoja kuzibana kampuni zinazoendesha michezo bado OFCOM wameshindwa kwa hiyo watanzania nawashauri ndugu zangu muwe wa angalifu sana siku ingine watu wata pozi kama washindi...
    mdau uk

    ReplyDelete
  3. wizi mtupu!

    ReplyDelete
  4. Huyu Jimmy ni mtangazaji mzuri sana wa vipindi hivi nilimfurahia sana kwenye kipindi cha bongo star search, umahiri wake hufanikisha na kufurahisha vipindi sana.

    ReplyDelete
  5. wewe anon wa kwanza hapo juu acha kupost mambo yasiyohusu picha. picha inaeleza kuhusu michezo ya kubahatisha wewe unaweka mambo ya madawa yakulevya. kwanini usianzishe blog yako ukaweka hayo maelezo yako ili watz wasome? acha ushamba unapoteza umuhimu wa mada na kuleta mada nyengine ndani yake.

    kuhusu huo mchazo wa seto kwa maoni yangu michezo hii inawafanya watz waache kuhangaikia maisha na maendeleo yao na kuwa bize katik kutafuta maisha kwa njia ya mkato. ni michezo ambayo inalemaza na kudumaza uwajibikaji na jitihada za wananchi kujiletea maendeleo. badala ya watu kuwa bize katika kazi huwa bize katika kutuma sms nyingi zaidi ili huenda wataibuka washindi.

    nadhani umefika wakati sasa serikali kuipiga marufuku michezo hii mabayo ni njia za watu wachache kujitajirisha kwa kutumia migongo ya walala hoi.

    ReplyDelete
  6. jamani mimi nina swali
    hivi huyu Jimmy Kabwe yuko wapi siku hizi (i mean anatangaza bado redioni?) nauliza hivyo kwa maana moja, kuna mtangazaji wa KISS fm wana fanana sana sauti na anajiita JK nikadhani ile JK ni Jimmy kabwe..... nikagundua anasema JK stands for JOHN KORAN, sasa nashindwa hata kuelewa ndiye JIMMY KABWE au wanafanana SAUTI???? naombeni msaada wadau......

    ReplyDelete
  7. Jamani hivi Jina halisi la Jimmy Kabwe ni lipi? Nasikia hilo jina ni A.K.A yake.

    ReplyDelete
  8. anony wa 11:56am sijui nitaonekana mmbea ila kabla sijaondoka bongo nilisikia akiitwa jumanne kabwela..lol..na hiyo ni a.k.a na wewe wa anony mwingine jimmy sasa anatangaza bahati nasibu tbc na morning show magic fm..ni hayo tu nawaachia waosha vinywa

    ReplyDelete
  9. kamari, ubebaji unga, bahati nasibu za kuwanasa watazamaji wa TV kwa masaa n.k ni lazima zithibitiwe maana watu watakuwa hawana fikra mbadala za kufanya kazi ili kujipatia kipato.

    Annony wa kwanza Addis pia shukurani kuifahamisha blogu ya jamii jinsi njia za mkato kujipatia fedha zilivyo na madhara yake.

    Waendeshaji bahati nasibu pia wawe chonjo wasije wakaleta 'addiction ya pesa za mchezo' kwa kuwatahadharisha wachezaji wasipoteze pesa nyingi, ambapo chance ya kubahatika ku-wini ni 1 kwa millioni 1,000,000.

    ReplyDelete
  10. sina hakika kuhusu jina, ila jaribu
    JUMANNE KABWELA...tehe heh ehee

    ReplyDelete
  11. Huyu Jimmy Kabwe ndiyo alikuwa DTV miaka ile na Marehemu Amina Mongi (RIP)? By the way, michuzi una picha yoyote ya marehemu tukumbushane?

    ReplyDelete
  12. Hu Wiziiiiiii Mtupu! hakuna yoyote atayeshinda hapo hapo kwao au wanatafuta mtu wanampa Sh 100,000 then aseme kashinda milioni Tanzania ina Watu milioni ngapi wenye Simu? waki tuma SMS zao jamaa wanajipatia zaidi pesa kwahiyo hawatoshindwa kumpa 100,000 then aseme kashinda mamilioni janja ya nyani hii ndio tabia wanayoifanya Zain Mobile wale jamaa wa Mkuu wa wilaya ya nanihii Uongo? basi atabana comment hahaha.

    ReplyDelete
  13. Hakuna kitu kinachoitwa WIZI MTUPU hapa. Ninachofahamu huwezi chezesha michezo hii bila kibali cha Serikali na kama kungekuwa na WIZI MTUPU!! Basi serikali isingetoa VIBALI. Mimi nashauri Watanzania tushiriki kwani huwezi jua, Dunia zilizoendelea zinafanya sana mambo haya kuna Jackpot/PowerBall na michezo kibao na watu hujishindia. Mtanzania jaribu bahati yako kwani huwezi jua lini unaweza ibuka mshindi. By the way huyu Jimmy anaitwa Jumanne Kabwela na nasikia anatangaza akiwa NJE Ulaya. Hapa Tanzania kuna Television gani inaweza kuwa na Studio nzuri kama hizo. Tuache maneno tujaribu bahati tuma neno SETO kwenda 15777

    ReplyDelete
  14. wajinga ndio waliwao: mchezo huu ni kama mengine uliyopo nchi nyengine. anaepoteza pesa ni mwenye tamaa ya pesa za haraka haraka. kila ukipeleka text inakugharimu kiasi fulani, kati ya hizo percentage fulani inakwenda kwa wenye huduma ya simu walio na deal na tv inayorusha huo mchezo, percentage inakwenda kwa tv inayorusha na percentage ndogo inakwenda katika kuchangia zawadi ya mshindi!

    sasa tizama kwanza watu wangapi tanzania kwa tamaa zao wanatuma text kila usiku? tena wala sio moja, na wote wanagombania zawadi moja tu kwa siku! probability ya kushinda ni too high, na kila siku usioshinda unamtajirisha mwenye tv na simu maana wao ndio wanaopata malipo ya uhakika kila mtu anapotuma text.

    ReplyDelete
  15. hahahhaaaaa
    ebwanae huu ni kulemaza fikra watu za asiefanya kazi na asile,shiiiida kweli hii
    watu mna utani na majina ya watu?hahahaaaa ati JUMANNE KABWELA teh
    inankera saaana hii mcichezo asa wale wa mitandao ya simu,,nyambafu sana
    kuna siku niliwatolea watu uvivu eti mtu kakazana atua sms weee atajirike na voda,zain,tigo,ivi hamna ata basi kitu cha maana kufikiria tu?adi zee zima lilo-mature eti asubiri lori la mwk nyerere

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...