Bro Michu na Mjengwa
Nawatumia picha ambazo nilifanya utalii wa ndani sehemu mbalimbali wadau wengine nao wahamasike na utalii wa ndani.

Kwa kuanzia nimewatumia picha za kimondo kilichoanguka mbozi mkoani mbeya miaka mingi iliyopita.
Mdau wa viti virefu-Fredd.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Bwana Michuzi.

    Mi siku za nyuma nimeshawahi kuuliza swali kuhusu hivi Vimondo lakini sikuwahi kujibiwa. Sasa naliuliza tena.

    Hivi ni kwa nini hivi VIMONDO vyote vinavyodondoka huwa VINAANGUKIAGA PORINI au sehemu KUSIKO kuwa na MAKAZI ya watu?

    Kuna sababu yoyote ya KISAYANSI ya kuangukia huko maporini au ni MIPANGO YA MUNGU tu ili kuepusha maafa?

    Tafadhali wataalam wa mambo ya anga.

    ReplyDelete
  2. MIMI NINASHAURI, KWA KUWA SERIKALI HAINA SHUGHURI NA UTALII KUSINI HICHO KIMONDO WAKIHAMISHIE MOSHI AU ARUSHA KISHA ITANGAZE KUWA KIMEANGUKA HUKO KUTOKA MBEYA. WEWE SI UMEONA KIMONDO , KUNA DARAJA LA MUNGU.

    ReplyDelete
  3. Tatizo la serikali na watanzania kwa ujumla hatuko creative ktk mambo mengi. Hiki KIMONDO kingeangukia katika nchi za wengine hii sehemu ingekuwa ni ya kitalii.Eneo lote lingewekwa kitu ka CIRCUS PARK ambapo watu wangeuwa wanakuja kuangalia maonyesho mbalimbali.
    Mdau uliyeuliza kwa nini vinaangukia porini.Sidhani kama kuna sababu yoyote ya kisayansi inayosababisha kimondo kiangukie porini.

    ReplyDelete
  4. miaka mingi lini???
    afu utalii kusini hakuna kabisa wametuacha solemba,JK tumekukosea nini asa Iringa la lile mbunga la wanyama kibao why???

    ReplyDelete
  5. Mbona linaoneka jiwe tu ambalo watoto wanachezea?? It seems walilibatiza tu na hilo jina la Kimondo? It is just like other stones. Utalii gani wa kuangalia mawe? How are they sure kwamba lilianguka toka angani? Au ni hadidhi za alfa ulela!! Watupatie scientifc proof kwamba ni kimondo otherwise naona ni kudanganyana tu.
    Mdau

    ReplyDelete
  6. Anony wa 7:11 Naomba nikuhakikishie kwamba hicho kimondo sio jiwe ni chuma tupu na ukiangalia hapo pembeni kuna alama kama ya kukatwa.Waliokata hicho kipande walitumia masaa kukikata. Mimi sio niliyetuma hiyo picha ila nilitembelea hiyo sehemu 2002 na nikaona hicho kimondo. Tatizo letu ni kuwa watu wasomi wa mambo Astonomy ni wachache na sina hakika kama kuna mtanzania. Tunahitaji kujitangaza zaidi na zaidi. Hata hao watanzania walioko BBC nakadhalika hawana juhudi za kuitangaza Tz na wakati BBC dunia nzima wanaangalia. Sio Alfa ulela ni ALF LELA WA ILELA.

    ReplyDelete
  7. Mdau Perez inatokea tu vinahanguka hapo vilipo hakuna zaidi.Nimevisoma sana kwenye fani yangu ya Geology,na hicho kimondo tulikitemblea mwaka fulani tukiwa second yeae university of Daresalaam,usiwe na wacwac na majibu yangu.Swali la kizushi 'ni kwanini siku hizi havidondoki sana?',vyote ni millions of years ago!!

    ReplyDelete
  8. Hapo panajulikana kama 'Mbozi meteorite'

    ReplyDelete
  9. David Villa unadai vyote vilianguka millions of years ago???naanza kuingiwa na wasiwasi kama sio jiwe tu hilo kuna ushahidi upi kama kweli kilianguka ambao huo ushahidi unatakiwa uthibitishe kuwa pia ulikuwepo kabla ya BIBLIA na kabla ya YESU

    ReplyDelete
  10. Mdau hapo juu sisi kwa fani yetu huwa tuna dini zetu lakini wakati vitabu vya dini vinasema dunia iliumbwa na mungu sisi tunakataa KABISA tunaamini dunia haikuumbwa na mungu.Chukua muda kidogo browse kwenye googles kitu kinaitwa 'SOLAR NEBULA'.

    ReplyDelete
  11. Wewe anonymous wa Tarehe January 15, 2009 8:02 PM, unasema kimondo hicho ni chuma tupu. Mbona wakusanya vyuma chakavu hawajakichukua na kwenda kukiuza? Au kinaulinzi mkali!! Au wale wenye viwanda vya chuma kwanini wasiende kukichukua na kutengeza samani kama nondo na vipuli vya magai?
    Mdau

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...