ABIRIA KIBAO WAMEKWAMA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA NYERERE HAPA DAR BAADA YA DEGE LA KLM LILILOKUWA WAPAE NALO KWENDA UGHAIBUNI ALHAMISI KUSHINDWA KUONDOKA KWA MATATIZO YA KIUFUNDI.
GLOBU YA JAMII IMEONA ABIRIA WAKIPELEKWA HOTELI MBALI MBALI ZA UBUNGO KWA DALADALA, NA USIKU KUAMKIA LEO WALIINGIA NDEGENI LAKINI BAADA YA MASAA KADHAA WAKAAMBIWA NGOMA BADO. WAKASHUKA NA KWENDA KUSHIKA MCHUMA TENA KUELEKEA UBUNGO.
HADI NAENDA KUPATA MBAAZI NA ANDAZI MTAA WA JIRANI HAPA NILIPO DEGE HILO LILIKUWA BADO UWANJANI, ILA WAHUSIKA WANASEMA ABIRIA WASIKONDE KWANI KUNA DEGE LINGINE LITAINGIA MUDA SI MREFU UJAO NA NDIO KUSEMA ZITAONDOKA NDEGE MBILI ZA KLM MCHANA HUU.
TUTAENDELEA KUPASHANA MAENDELEO KWA KADRI YANAVYOJIRI...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Hii ni kwa mara ya kwanza nafikiri tujifunze kwa wenzetu yaani sisi ATCL,maana pamoja na dege kukwama bado abiria wanapata huduma kama kawa.

    Nikikumbuka lile igizo la mahujaji ndio ninapochoka na ATCL.

    ReplyDelete
  2. Balozi wa Naniihii! Nataka kukujulisha kwamba ushanitamanisha Mbaazi na Maandazi asubuhi hii huku Toronto, Canada.Nilipokuwa nyumbani, nilikuwa napata vitu vyangu pale mtaa wa mchikichi karibu na Jamati la Kariakoo na pale mtaa wa Rufiji/Swahili. Pale kwa akina BAJETI. Ahsante, wacha niende nikatayarishe vitu.Huku hamna mama ntilie kwahiyo inabidii nikunje shati mwenyewe.

    ReplyDelete
  3. British airways na Swiss Air au Emirates rocks! KLM sucks! Ubungo na sio bahari beach!wamechafua jina lao.

    ReplyDelete
  4. Kutukana bure sio vizuri, kwani hao abiria wamepelekwa kwenye hoteli mpya ya Blue Pearl Ubungo, ambayo ni mojawapo hoteli bomba zaidi mjini. Pia umbali toka airport ni mdogo sana kuliko kupambana na mafoleni hadi huko baharini.

    ReplyDelete
  5. Ibanie hii Michuzi kama kawaida yako, Ila unabore sana unapo andika kutu serious halafu unaleta utani, kusema daladala ina maana gani? eti kushika mchuma,sijui umepewaje ubalozi wa Zain , uandishi wako una matatizo sana. hata ukibana umesha isoma .

    ReplyDelete
  6. i feel for the pepople on the plane lazima watakuwa wako hoi wanahamu ya kurudi nyumbani na wanaowahi shule na vitu kama hivo sema lazima kuna watu watakuwa wanafikiri wamerushiwa kipapai hapo hehehehehehe worry not technical difficulties happen y'all mbona uku watu wanakuwa delayed sababu ya snow maybe somethin hapened to the engines n they have to fix it..bora hawajaamua kuondoka kupeusha ajali au sio

    ReplyDelete
  7. wewe anonymous wa January 31, 2009 5:29 PM {British airways na Swiss Air au Emirates rocks! KLM sucks!} vipi? badala ya kusifia usafiri wako wa nyumbani wewe unakandia! kumbuka nyumbani ni nyumbani tu hivyo acha tabia ya kusifia vyawengine wakati vyakwako vibovu: Wewe ni M'bongo tu tena mweusi, si mzungu wala mwarabu! Pumbavu*

    ReplyDelete
  8. aisee nilifikiri ATC?naskia nayo imekwama pale KIA juzi tu apa!!jamen izi ndege taratibu sidhani kuna shujaa kama wa dege lilotua Hudson river USA,,,
    chonde bora KLM waliamua kulipumzisha na ingine yaja ingekua bongo mmmh!
    ata kama wakikaa wiki ni heri kwao tu,yanini ufe angani?mana zile parachutes uwa hazivaliwi kabisa na hazijawai muokoa mtu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...