Home
Unlabelled
kp leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Hata mimi nawashangaa waTZ. Wanadhani mtoto huwa anazaliwa na kuanza kukimbia bila kwanza kuzoea kukaa, kutambaa, simama dede, kuanguka na kujigonga pua kidogo,kutembea na hatimaye kukimbia. Kuna watoto wengine huweza kukimbia mapema na wengine huchelewa. Kuna sababu nyingi zinazochangia hapo, sio lazima tu house girl au mama ambaye anamsaidia huyo mtoto ndiye mwenye makosa. Uwoga wa mtoto, mazingira, hali ya uchumi n.k
ReplyDeleteLazima tuanze kujifunza kukosoa kwa kutia moyo na kujenga (constructive critisism)badala ya kukatisha tamaa.Timu ikifanya vizuri tusifie, ikifanya vibaya tujiulize kwanini imefanya vibaya na tufanye nini next. Bila hivyo tutaendelea kubadirisha makocha kila kukicha kama wafanyavyo simba na watani zao yanga.
Mdau
Cardiff
Kushinda na kushinwa ndiyo sehemu ya mpira. Watanzania tunakuwa watu wa ajabu sana tunapoanza kurusha mabomu ya lawama kwa kocha m-Brazil Maximo. Lazima inapotokea mambo hayajawa sawa tunalubali. Maana siku chache zilizopita Maximo alikuwa lulu. Leo Maximo mbaya. Je timu gani ambayo haijawahi kufungwa hata goli moja au kupteza mchezo hapa duniani??? It is disappointing. Tukubali matokeo hayo ya kombe la Challenge kwamba timu haikufanya vizuri na tuvute soksi kwa ajili ya mashindano mengine yajayo.
ReplyDeleteMdau wa Oslo, Norway
Sisi ni mabingwa wa kuponda tu!
ReplyDeleteHamna kizuri kwetu
Bora uwaeleze KP...Huo ni ufisadi katika mpira,kuitelekezatimu baada ya kufungwa!!!
ReplyDeleteKuna mbongo mmoja anaitwa Kisiju, huo ujumbe unafanana sana na yeye kwa asilimia mia moja. Wabongo siku zote tunajufanya sisi tuko sawa ila makosa yanafanywa na wenzetu, tabia moja mbaya sana kwa sababu inakuwa vigumu kuyasahihisha makosa yetu kutokana na ujuaji uliotuja kwenye vichwa vyetu, kaka Masoud Kipanya hongera sana, hilo ni boonge la katuni lililobeba booonge la message.
ReplyDelete