Mojawapo ya chaguzi ambazo zimekuwa na mvuto wa muda mrefu ndani ya CCM ni ule uliofanyika mwishoni mwa juma lililopita ambapo Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM (T) alipatikana.
Mshindi huyo si mwingine bali Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe. Sofia Simba. Safari ya ushindi wake ilikuwa ni safari ambayo wachache wako tayari kuipitia. Ilikuwa ni safari ambayo unapofika mwisho inabidi ujiuliza ulianzaje safari hiyo.
Hivyo KLHN ilipata nafasi ya kuzungumza naye kwa kirefu kuhusu ushindi wake huo na hasa kutupa mwanga kuhusu kile kilichokuwa kinaendelea kati yake na mpinzani wake katika uchaguzi Mhe. Janeti Kahama.
Pamoja na hayo tumemuuliza maswali ya kutaka kujua kama kweli Rais Kikwete ndiye aliyemtaka agombee na kama ni kweli hotuba ya Rais Kikwete kwenye ufunguzi wa uchaguzi ilikuwa ni ya kumpa mkono wa baraka ili achaguliwe. Pamoja na hayo tulitaka kujua zaidi kuhusu UWCCM utakuwaje chini ya uongozi wake?
Sikiliza mahojiano hayo ambayo yanapatikana kwenye
Mshindi huyo si mwingine bali Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe. Sofia Simba. Safari ya ushindi wake ilikuwa ni safari ambayo wachache wako tayari kuipitia. Ilikuwa ni safari ambayo unapofika mwisho inabidi ujiuliza ulianzaje safari hiyo.
Hivyo KLHN ilipata nafasi ya kuzungumza naye kwa kirefu kuhusu ushindi wake huo na hasa kutupa mwanga kuhusu kile kilichokuwa kinaendelea kati yake na mpinzani wake katika uchaguzi Mhe. Janeti Kahama.
Pamoja na hayo tumemuuliza maswali ya kutaka kujua kama kweli Rais Kikwete ndiye aliyemtaka agombee na kama ni kweli hotuba ya Rais Kikwete kwenye ufunguzi wa uchaguzi ilikuwa ni ya kumpa mkono wa baraka ili achaguliwe. Pamoja na hayo tulitaka kujua zaidi kuhusu UWCCM utakuwaje chini ya uongozi wake?
Sikiliza mahojiano hayo ambayo yanapatikana kwenye
Kwa maoni au mawazo tuandikie
mhariri@klhnews.com
Unaweza kusikiliza pia hapa:
Title: KLH News Episode: Mahojiano na Mhe. Sofia Simba
Unaweza kusikiliza pia hapa:
Title: KLH News Episode: Mahojiano na Mhe. Sofia Simba
/entry/2009-01-13T19_47_49-08_00
Enjoy!
Mhariri
Halafu huyu mwenyekiti mpya wa UWCCM,Waziri Simba nimesoma mahojiano yake na nyie naona kama vile ni mtu wa kujisifia mno,sasa hili sidhani kama ni jambo zuri kwa kiongozi kama yy,na kama ataendelea hivyo basi sidhani kama itakuwa na mwisho mzuri kiutendaji hiyo UWCCM,kwani kushinda kwake ni maana kwamba wapinzani wenzake ni wadhaifu mno kama yy anavyosema?je ni kweli hawakuwa na elimu kama yy anavyoisifia,mara ooh degree ya pili ni mechukua marekani...thtz damn!!! Kwa sababu kashinda anajifanya hana bifu na wenzake,wakati kulikuwa na majungu mengi tu kipindi cha kampeni.inaonekana ana kasumba flani,Anyway namwombea kila la heri kwenye safari yake ya huo uongozi.
ReplyDeleteHuu ni mtizamo wangu baada ya kumsikiliza Mwenyekiti mpywa wa UWCCM, Bi Simba.
ReplyDeleteKama mwanasheria, kiongozi na mwanasiasa, nilitegemea mahojiano yaliyotulia, majibu yenye kina na staha, na heshima kwa wagombea wenzake.
Vile vile nilitegemea majibu yenye mtiririko uliopangiliwa.
Lakini nimeshtushwa na mahojiano hayo.
Kwanza Mwenyekiti ni mtu mwenye kupenda kujisifia na kurudia rudia kuonyesha yeye ni bora. Angeweza kuongea mara moja na akaeleweka hasa alipozungumzia elimu yake.
Pili.. ameonyesha dharau kwa wagombea wenzake, na kama ningekuwa napiga kura, kwa kumsikiliza hivi, nisingempigia kura.
Kwenye majibu, amekuwa akijibu swali moja, hajamaliza anarukia kitu kingine, na mbaya zaidi anatia na jazba kidogo.
Kama haujasikiliza, sikiliza utasikia mwenyewe.
Kama huwa anasoma maoni hapa kwa michuzi, namshauri awe akiongea kwa taratibu na kwa mpangilio, itakuwa rahisi kueleweka, kufikisha ujumbe kwa njia bora na kwa heshima zaidi.
Elimu ya Masters siku hizi ni kawaida,watu wengi wanayo, hivyo akumbuke kuwa si msomi kiasi hicho.
Kama ana uzoefu kama anavyosema... basi atumie uzoefu huo kutenda.
Kama yeye ni mtendaji, kiongozi, mwanasiasi mzuri, asihofu, kwani tutajua kwa kuona anavyotenda na anavyoishi kwa ujumla.
Chaupele
Huyu cheaman wao duh, ye anaona walisoma ndo zaidi? hii kasumba ya walisoma vs wasiosoma ni mbaya sana. Hatutofika popote kama tutaanza kutengeneza utengano kwa misingi ya elimu. Ni ubaguzi kama ulivo ubaguzi wa rangi, jinsia, na mengineyo. UWT mnalo
ReplyDeleteMheshimiwa Balozi na Mkuu wa Wilaya, nimeyasikiliza mahojiano hayo. Nimemsikia Waziri Simba akieleza jinsi alivyoelimika kuwazidi wapinzani wake. Kwa maoni yangu, kuna tofauti kati ya kusoma na kuelimika. Kama ni kusoma, mimi nimesoma sana, ila naamini kuwa kuelimika ni pamoja na mtu kuyatambua mapungufu yako. Nilitegemea Waziri Simba ajibu masuali aliyoulizwa, lakini majibu yalikuwa haba, na masuali yamebaki yanaelea hewani. Badala ya kuzingatia masuali, anaongelea vitu vingi, na pia anamwongelea mpinzani wake. Kwa mfano, suali la wazi kuhusu rushwa katika uchaguzi hakulijibu. Alivyoulizwa kuna nini huko UWCCM ambacho kinawavutia watu wagombee, au kwa nini yeye aligombea, napo hakuzingatia suali. Vile vile, sikupendezwa na jinsi Waziri Simba anavyotumia maneno ya kiIngereza katika mahojiano ambayo yalikuwa katika lugha ya kiSwahili. Je, anategemea wanawake wa Tanzania, au Watanzania kwa ujumla, ambao asilimia kubwa hawajui hayo maneno au misemo ya kiIngereza, watamwelewa? Nilipomaliza kusikiliza mahojiano hayo, nilitikisa kichwa na kusema kuwa kazi bado tunayo.
ReplyDeleteShe seems to be very arogant of herself. Kweli na mimi nimesikiliza anavyoponda wenzie na kujisifia yeye mwenyewe yaani mpaka inaboa. Ohh nina Masters ya Marekani! Oh mimi ni lawyer, Oh nina uzoefu kuliko Janeth Kahama, Oh mimi ni waziri hivyo nitatumia nafasi yangu kuinua akinamama. Oh Maranda hajasoma, mwizi? Anageuka yeye kuwa mahakama?? Is that the type of leaders we want?? She is useless. Hiyo wizara ya akina mama na watoto ilimshinda, wizara ya utawala bora hakuna kitu kinachoeleweka huko. Je hiyo UWTCCM ataiweza na majigambo yote hayo? Nadhani hafai kuwa kiongozi wa umma. Alitakiwa awe tu kwenye NGOs ambako huwa utaratibu wake sometimes huwa hauleweki. Lakni kwenye civil servants au kwenye kutoa huduma I think she is not fit.
ReplyDeleteAnyway hao ndio viongozi wetu.
Mdau
She ignant, arogant and full of herself. She thinks that UDSM and masters ya US is all want women need bongo.
ReplyDeleteShame on you mama Simba and watch your tone because in the long run you breaking up CCM.
All I can say is "Time will tell" na huo uwenyekiti wako kama hautaota mbawa kutokana na hizo kauli zako za kipumbafu.
mh simba, mdau mmoja amesema sawa, umesoma lakini hujaelimika, na kutokuelimika kwako ni jinsi unavyojibu maswali kwa kuparamia, hupangilii, huconcentrate na kutoa jibu muafaka, kuendelea kumponda mpinzani wako wakati uchaguzi umeshaisha na wewe umeibuka kidedea, kumbuka kampeni chafu zilitawala kotekote, kwa msomi na asiyesoma, unaporingia usomi tunatumaini kuwa kwa kuwa waziri wa utawala bora, usingethubutu kutinga nyumba ya kulala wageni siku ya jumapili na gari la serikali kujinadi !!
ReplyDeletehalafu sifa zako ziimbwe na wengine usijisifie sana, natumaini UWT itakupa miaka 5 tu aingie mtu aliyemaliza kidato cha nne anayejua uhamasishaji na ushirikishwaji !! sofia alianza kama katibu muhtasi ndipo akajiendeleza ambayo ni mafanikio makubwa lakini nadhani huitumii elimu yako vizuri , president elect Obama katika kujinadi hajawahi kusema nichagueni kwa vile nilisoma Havard... food for thought SIMBA WA YUDA
Ukweli ni kwamba, Janeth Kahama ni wa mwaka 47, na huyu Sophia shule ameenda, period. Wabongo tuache kutetea mambo ya usawa usawa hata kwenye suala la elimu! kama mtu amesoma, mi sioni kwa nini asiseme kwamba amesoma, sasa mlitake anyamaze, wakati kiukweli kwa kutumia turufu hiyo ya kisomo ilikuwa inamuongezea chances za kuchaguliwa?
ReplyDeleteWe anon 4:21 pm usiwe arrogant kama huyo mama Simba. Issue hapa sio elimu, issue ni kuelimika; tumewaona kina Bush wenye shule za Yale na Harvard lakini wamefanya nini? hafadhali hata ya high school graduate.
ReplyDeleteNaheshimu sana shule, ila pale inapotumika arrogantly then inakuwa sio shule ni upumbavu sio ujinga
Anon 4:21 aka Mwanakijiji.
ReplyDeleteKwa nini unatetea low standards?. Pole sana najua mheshimiwa kakulaumu, huenda yeye alijua kuwa utaandika tu aliyosema na si kuya-podcast. Next time uwe unawaambia kuwa utarusha mahojiano ili waongee kwa kufikiria sio kuongea kama wapo kwenye viti virefu.