Mdogo wa marehemu Pama (DULLAH) aliyeshika Jeneza baada ya kushiriki katika kuosha mwili,tayari kwa kufanya maombi ya pamoja. Blog hii kwa niaba ya uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Italy na watanzania wote unatoa salaam za rambirambi na pole kwa familia ya mzee Shakur,pamoja na kuwa msiba huu ni wetu sote.Pia shukrani,rambirambi na pole kwa mdau wetu Dullah kwa kuondokewa na kaka yako,uongozi wa jumuiya umeridishwa sana na ushirikiano wako wa karibu katika kipindi hiki kigumu cha msiba,tunamuomba Mungu akupe wewe pamoja na familia yote uvumilivu.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA ,DAIMA ATAKUMBUKWA NA WADAU WA HAPA ITALY NA SEHEMU ZOTE ANAZOFAHAMIKA. AMIN!!
Mwenyekiti wa jumuiya akiwa na Sheikh Bin Rajab tayari kwa kuanza maombi na dua kwa marehemu.

Watanzania kibao jana walikusanyika kuaga mwili wa marehemu PAMA aliyefariki siku ya tarehe 5/01/2009.
Pichani watanzania wakiwa katika dua ya pamoja iliyoongozwa na Sheikh Maulid Bin Rajab ambaye ni sheikh wa jumuiya ya Watanzania Italy aliyeongozana na viongozi na wajumbe wa Tawi la jumuiya ya watanzania kutoka MODENA. Mwili wa marehemu utaondoka Rome siku ya jumanne tarehe 13/1/2009 kupitia Amsterdam kwa ndege ya shirika la KLM, na unatarajiwa kuwasili nyumbani Dar kwa mazishi siku ya jumatano 14/01/2009 saa 22:40. na ndege ya shirika la KLM namba 569.

(KWA PICHA NA HABARI ZAIDI: http://www.tnzncommunity.blogspot.com





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mwenyezi Mungu iweke roho ya marehemu pahala pema peponi.Poleni sana ndugu,jamaa na marafiki wote wa marehemu.

    JAX

    ReplyDelete
  2. poleni sana ndugu na jamaa wa marehemu sisi watanga wa hapa cape town south africa tumesikitika sana kutokea kwa msiba huu tunatoa rambi rambi kwa watu wote wanaohusika na msiba huu hasa kule nyumbani tanga hakuna kijana yeyote msafiri asiye mfahamu huyu Pama na yeye amewezesha vijana wengi kusafiri nchi za nje kutafuta maisha kwa njia moja au nyingine tunaungana na watu wote kwa msiba huu mkubwa sana poleni jamaaa wote mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu

    ReplyDelete
  3. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, AMIN

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...