rejeta imechemsha na mdau inno anavuta pumzi ili ipoe wakati akiwa njiani kuelekea kilele cha kibo na hatimaye uhuru. hapo anasema nusura aachie ngazi maana hewa ilikuwa finyu na miguu ilikuwa haitaki kutembea, baada ya kupiga mguu kwa masaa sita tokea gilman's point.
mdau inno alikuwa ni mmoja kati ya wafanyakazi 10 wa daily news na habari leo waliokwea mlima kilimanjaro majuzi katika kuadhimisha miaka miwili ya gazeti la habarileo.
stori kamili na picha kibao za shughuli hiyo pevu zinaandaliwa. kaa mkao wa kula...
kama hamyawezi haya mambo bora mkae nyumbani
ReplyDeleteAkae nyumbani ili iweje? kazi kukatisha tamaa watu tu.
ReplyDeleteHongera kaka kwa zoezi zima.Tia hamasa kwa wengine pia wakapande mlima Kilimanjaro na kujionea wenyewe kwa macho barafu juu ya mlima ili hali uko tropical.
Next time nita wajoin.
Mh! Mbona kuna mchanganyiko wa mambo humu?? Mana Gilman's point ni karibu na kileleni na ni mwendo wa saa tano tu toka Kibanda cha Mwisho Kibo hut, na unaondoka Kibo hut usiku mh!! hebu tupate ufafanuzi. Pia Uhuru peak na Kibo peak ni kitu kimoja
ReplyDeleteMsikatishe tamaa watu. Natamani ningepanda huu mlima nikiwa bado na muda wa kuupanda. Sasa hivi majukumu mengi lakini sijakata tamaa bado na imani nitarudi nipande siku moja
ReplyDelete