rejeta imechemsha na mdau inno anavuta pumzi ili ipoe wakati akiwa njiani kuelekea kilele cha kibo na hatimaye uhuru. hapo anasema nusura aachie ngazi maana hewa ilikuwa finyu na miguu ilikuwa haitaki kutembea, baada ya kupiga mguu kwa masaa sita tokea gilman's point.
mdau inno alikuwa ni mmoja kati ya wafanyakazi 10 wa daily news na habari leo waliokwea mlima kilimanjaro majuzi katika kuadhimisha miaka miwili ya gazeti la habarileo.
stori kamili na picha kibao za shughuli hiyo pevu zinaandaliwa. kaa mkao wa kula...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. kama hamyawezi haya mambo bora mkae nyumbani

    ReplyDelete
  2. Akae nyumbani ili iweje? kazi kukatisha tamaa watu tu.

    Hongera kaka kwa zoezi zima.Tia hamasa kwa wengine pia wakapande mlima Kilimanjaro na kujionea wenyewe kwa macho barafu juu ya mlima ili hali uko tropical.

    Next time nita wajoin.

    ReplyDelete
  3. Mh! Mbona kuna mchanganyiko wa mambo humu?? Mana Gilman's point ni karibu na kileleni na ni mwendo wa saa tano tu toka Kibanda cha Mwisho Kibo hut, na unaondoka Kibo hut usiku mh!! hebu tupate ufafanuzi. Pia Uhuru peak na Kibo peak ni kitu kimoja

    ReplyDelete
  4. Msikatishe tamaa watu. Natamani ningepanda huu mlima nikiwa bado na muda wa kuupanda. Sasa hivi majukumu mengi lakini sijakata tamaa bado na imani nitarudi nipande siku moja

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...